Mwl Nyerere aliwahi kusema "hatuwezi kuwa na rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.
Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya rais au waziri mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida. Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.
Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu
Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je? anajua jinsi ya kututoa? Anajua anakotupeleka? Nimejitahidi kuangalia bunge ili nione labda mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi. Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!
Kaka acha UJUVI pasi na ujuzi
Je wewe unaamini kwamba nchi hii imewahi kuwa na mwelekeo, sera za kuweza kuleta maendeleo? Imewahi kuwa na viwanda, rasilimali?
Mbona leo tuko hapa...!??
Tukiendelea kuchota maji kujaza pipa lililotoboka, naamin, halitojaa haraka, hata likijaa maji hayatokaa yatavuja na kupotea
Ndio maana malengo na mipango yote ya nyuma imetufikisha hapa tulipo, pabaya
Angalia SERA , MALENGO,VIPAUMBELE, MIPANGO ya TAIFA Kwa kuzingatia ILANI YA CHAMA
JPM ameanza na kujenga mindset,uwajibikaji, ubinafsi, kupunguza ufisadi na rushwa.
Ndio Amana JPM anafikiri kutoa fursa kwa vijana zaidi watakaokuja na mindset mpya
Bora kesho wewe uamkie kwenye kufagia mitaro maana tulikupa GENERAL TYRE UMEFILISI.
Umesahau makapuni MATSUSHITA yaliyokuwa yanatengeneza Radio kama NATIONAL, PHILLIPS...?
Makampuni yaliyokuwa kama hayo nchi za wenzetu leo hii yanatengeneza Music systems, tv- flat screens, mafridge na mobile phones zikiwemo smartphone na vifaa vingine vya umeme.
Leo hii tunashabikia kununua ndege mpya tukawakabidhi wale wale CORRUPT, IRRESPONSIBLE MANAGEMENT tunataraji nini!?
Tatizo kuu la nchi hii ni UWAJIBIKAJI, USIMAMIZI,ili kuondoa uzembe, wizi,ubinafsi,upendeleo rushwa na ufisadi
Ndio maana tunashangilia utumbuaji, we are not stupid, we know the LOCKS is on the right truck,ukijikuta umeamkia mtaroni ujue wewe ndio wale wale mnaokunywa uji wa mgonjwa,
Sasa mnadai haki baada ya kushindwa kutekeleza majukumu yenu, . NYAMBAAAF
Aibu yao watendaji serikalini na watumishi waliotufikisha hapa
Aibu yao viongozi wa kisiasa(CCM) kwa kushindwa kusimamia watumishi na serikali zake
JPM usijaze maji pipani kabla ya kuziba matundu
jamani hili halihitaji usomi