Tumbua, tengua, teua !!
Tumbua, tengua, teua !!
Tunahamia Dodoma, tunahamia Dodoma !!
Viwanda, viwanda, viwanda !!
Nasema nahitaji Tanzania ya viwanda !!
Tutawafunga mafisadi, tutawafunga mafisadi !!
Tumbua, tengua, teua, rudisha !!
Wafanyakazi hewa, wafanyakazi hewa !!
Tutamwaga ajira tutamwaga ajira !!
Tumbua, tengua, teua, rudisha..
Daah, sijapenda kuandika hivi na sio kwa ubaya wowote, lakinii tujiulizeni maswali na tujenge hoja.
1. Tangu mwaka jana na tunaingia huu mwaka habari kubwa ni kutumbua na kuteua na sasa pia kurudisha waliotumbuliwa.
2. Mwaka jana 2016 vijana hawajapata ajira zozote ambazo zinatolewaga na serikali, japo tulisikia zingetoka nyingi.
3. Now maeneo mengi kumekuwa na ukame na sasa tunasikia usalama wa chakula ni mdogo.
4. Tangu huu mwaka uanze bei ya dola imepanda maradufu na hii inatishia hata mfumuko wa bei na ni hatari pia maana kama hili baa la njaa likiwa kubwa gharama pia za kununua chakula nje itakuwa kubwa maana dola inaenda juu.
5. Ukandamizaji wa aina mbalimbali pia tumeushuhudia na wa waziwazi.
Kama nakosea naomba mnisamehe, lakini binafsi nimekata tamaa kabisa kabisa, na sioni tumaini lolote huko tunakoelekea. Kwa kipindi cha mwaka mmoja tu, tumeshapoteza vitu ambavyo ilituchukua mda kuvipata.
. Mahusiano ya kidiplomasia na nchi za nje
. Umoja wa kitaifa unapotea sasa, ukabila unatamalaki tena wazi wazi.
. Tunashughudia viongozi wengi wenye viburi nao wanatamalaki.
. Mgawanyiko mkubwa ndani ya jamii
Kwa ufupi nahisi na naona tupo kwenye consolidation ya kupoteza dira siku hadi siku.
Ikibidi tusali sana watanzania wenzangu ili na hawa viongozi waone yanayotokea sio sawa na tunahitaji about turn ya haraka sana. Hatuendi vizuri kabisa.
#Busara_za_Naantombe_2017