Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Kwel kabsaa ni ujnga ulioje kuzuia demokras wawaache watu waseme ndio siasa haiwag likzo ndio maana aliekalia ikulu katokana na siasa utajengaje chama na kuvutia mwanachama wa mwenzako ahamie kwako mbaya zaid vyama vmeajlia watumish vnawalipa mshahara maanayake ni wabule sio bac wafute luzuku mpaka 2020!
 
Mimi mwigulu kwa kujenga hoja nakukubali sana Nilikusikiliza kipindi unatangaza nia nilikuelewa sana wewe na January makamba lakini Mwigulu anamapungufu ya kuona kwamba wapinzani sio Watanzania utafikiri wapinzani wametoka somalia kuja kua wapinzani Tanzania wewe Kama kijana unatia aibu sana kama waziri
 
Kweli kabisa.natambua Mh. Mwigulu Nchemba unasoma huu Uzi.
Mnachokifanya kwa wapinzani ni kuwajenga kupitia Jeshi la polisi na si kuwakomoa.
Mfano uimara wa kisiasa wa Lema Arusha ni kutokana na kazi ya Jeshi la Polisi. Pengine Lema angepuuzwa basi watu wangemuona mjinga
 
Mwigulu Nchemba, we ni kijana mwenzetu hivi hizi kamata kamata za watani wako kisiasa unazionaje. Vijana km nyinyi mnapopata nafasi za kuingia Baraza la mawaziri ni ushindi kwetu Vijana. Tegemeo letu kwa nyie vijana wenzetu ambao Mkuu amewaona lazima mlete changes..kuna haja gani wa kukamata kamata wapinzani/ watani au vyama mbadala wanapofanya mikutano. Waache nao wafanye mikutano. Mwigulu wewe bado unafuture kubwa ya kisiasa..!!
Ivi Braza unadhani kukamata wapinzani ndo inasaidia Ccm ipendwe. Ukikamata wapinzani unasababisha wanapata sympathy. Na hiyo ndo ilichangia lema kuwa mwanasiasa maarufu na strong.

Polisi imemjenga lema.

Kamata kamata inawajenga wanasiasa wa upinzani na kuwapa kiki sana. Kama kijana acha hayo mambo ..wakemee watu wako wa chini. Kama act wanafanya mikutano waache wafanye hata km wanasema kuna njaa what's problem...chadema kama wanafanya kampeni kipind hiki waachiwe tu.

Tatizo ccm mnatumika kuwajenga wapinzani kwa kutumia jeshi la polisi bila kujua. Wapinzani waachwe wafanye siasa zao. Waache washauri , wakosoe n.k. !! Unaweza dhani kuwakamata kamata ndo kuvunja upinzani unakosea mzee.
We kijana mwenzetu tunajivunia wewe. Chuki za kisiasa hazifai.
Nikupe mfano 1 mwigulu, unakumbuka sakata la Shehe Ponda. Mlipokuwa mnatumia magari na helikopta kumpeleka mahakami.mlivuta attention Nchi nzima na ponda akawa maarufu na muhimu..but leo baada ya kuanza kutumia gari 1 tu tena bila hata escort Ponda hasikiki tena.
Kaka kamata kamata wakina zito, lema, mara mbowe , lowasa..mnatengeneza uhasama tu. Na advantage wanapata hao mnaowakamata.
2025 ntaakuliza tena swali hili tena.

Mnawapa kiki wapinzani. Sympathy vote za bure.



Mhe nchemba chapa kazi wanooshe hao,bila hivyo nchi haitaendelea .
 
Mtoa mada upo smart sana.
Ni kweli jeshi la polisi linawapa kiki wapinzani
 
Tatizo mnaye mshauri sidhani kama atawaelewa maana ni mmoja wa walevi wa madaraka tangu awali kila mmoja humu ulitambua hilo...
 
Tumbua, tengua, teua !!
Tumbua, tengua, teua !!
Tunahamia Dodoma, tunahamia Dodoma !!

Viwanda, viwanda, viwanda !!
Nasema nahitaji Tanzania ya viwanda !!
Tutawafunga mafisadi, tutawafunga mafisadi !!
Tumbua, tengua, teua, rudisha !!

Wafanyakazi hewa, wafanyakazi hewa !!
Tutamwaga ajira tutamwaga ajira !!
Tumbua, tengua, teua, rudisha..


Daah, sijapenda kuandika hivi na sio kwa ubaya wowote, lakinii tujiulizeni maswali na tujenge hoja.
1. Tangu mwaka jana na tunaingia huu mwaka habari kubwa ni kutumbua na kuteua na sasa pia kurudisha waliotumbuliwa.
2. Mwaka jana 2016 vijana hawajapata ajira zozote ambazo zinatolewaga na serikali, japo tulisikia zingetoka nyingi.
3. Now maeneo mengi kumekuwa na ukame na sasa tunasikia usalama wa chakula ni mdogo.
4. Tangu huu mwaka uanze bei ya dola imepanda maradufu na hii inatishia hata mfumuko wa bei na ni hatari pia maana kama hili baa la njaa likiwa kubwa gharama pia za kununua chakula nje itakuwa kubwa maana dola inaenda juu.
5. Ukandamizaji wa aina mbalimbali pia tumeushuhudia na wa waziwazi.

Kama nakosea naomba mnisamehe, lakini binafsi nimekata tamaa kabisa kabisa, na sioni tumaini lolote huko tunakoelekea. Kwa kipindi cha mwaka mmoja tu, tumeshapoteza vitu ambavyo ilituchukua mda kuvipata.
. Mahusiano ya kidiplomasia na nchi za nje
. Umoja wa kitaifa unapotea sasa, ukabila unatamalaki tena wazi wazi.
. Tunashughudia viongozi wengi wenye viburi nao wanatamalaki.
. Mgawanyiko mkubwa ndani ya jamii

Kwa ufupi nahisi na naona tupo kwenye consolidation ya kupoteza dira siku hadi siku.

Ikibidi tusali sana watanzania wenzangu ili na hawa viongozi waone yanayotokea sio sawa na tunahitaji about turn ya haraka sana. Hatuendi vizuri kabisa.

#Busara_za_Naantombe_2017
 
Tofautisha uwongo na ukweli.. Kuna ambacho nimeandika hapa ni uwongo? Je, si kweli kwamba habari kubwa zimekuwa za kutumbua, tengua, na teua? .. Kama ukweli kwako ndo wauita uchochozi, basi nenda kanisemehe
Corrections
Uchochozi>Uchochezi

Mada
Unadhani wote waliotuhumiwa kwa uchochezi walikuwa wanasema Uongo?
Nani anauhakika kama Lema alitudanganya ndoto yake?
Sio kila uchochezi ulikuwa ni Uongo, ila wapo wanaojutia Ukweli wao.
Hata hivyo sijakuzuia kuusikiliza wimbo wako wa kila siku, hata mimi hapa nimeupenda na ninausikiliza, ila siuimbi.
 
Jamani naomba waungwana mnisaidie maana ninachokiona huyu bwana pombe amekuja kulipa kisasi kwa wapinzani, ana hasira ambayo sio ya kawaida. Kumbe walivyokua wakiikosoa serikali yeye alikua anauma meno akisema moyoni labda Siku moja nisiwe raisi, maana ikitokea nikawa raisi watakoma. Sasa kawa raisi! niambie mtanzania usiye mnafiki, unaona nini juu ya Magufuli na upinzani? Na je adhma yake itatimia?
 
Wakubwa msifute huu Uzi tunataka tujadili adhma ya huyu bwana, na hatima ya Tanzania yetu. Kuna shimo refu sana liko mbele sasa sijui linammeza nani.
 
Jamani naomba waungwana mnisaidie maana ninachokiona huyu bwana pombe amekuja kulipa kisasi kwa wapinzani, ana hasira ambayo sio ya kawaida. Kumbe walivyokua wakiikosoa serikali yeye alikua anauma meno akisema moyoni labda Siku moja nisiwe raisi, maana ikitokea nikawa raisi watakoma. Sasa kawa raisi! niambie mtanzania usiye mnafiki, unaona nini juu ya Magufuli na upinzani? Na je adhma yake itatimia?
Mkuuuu huu uzi ni wenyewe [emoji16]
 
Ni lazima tujue kuna "leader" mfano jk na "managers" mfano yule jamaa mwenye jina la kinywaji chenye kilevi!! Hata siku moja leader hawezi fanya anayofanya huyu mtu!!
 
Na akisha kamata viongozi wote Wa upinzani na kuwafunga na kuwanyang'anya maliza zao, anadhani RAIA waliowachagua watamtafsiri kama mwanadamu Wa aina gani?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom