Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
M50 kila kijiji vp wananchi tunasubili huku atazitoa lini raisi wangu mpendwa????
 
Kwan huyu rais tulie nae anashaurika? Ni one man show,na hz nyuz huwa si zan kama anasoma zaid ya kutafuta wachochez ili awashughulikie!
 
Mods hii post ina views zaidi ya laki 2, inatakiwa kuwa sticky post... Hebu fanyeni wajibu wenu
 
Maisha hayajirudii Mara mbili tunahitaji kupiga hatua, tunataka maamuzi yenye tija kwa nchi sio maamuzi yenye hasara kila kukicha.

Magufuli wewe ni mkuu wa nchi, tumekupa kila kitu ili uwe dereva wa nchi yetu.

Sasa kwanini unakosea kila maamuzi unayofanya? Ni kweli watanzania tulikosea kukuchagua?

Magufuli kuwa fisadi sio kuiba Mali ya umma tu hata kulitia Taifa hasara kutokana na maamuzi ya hasira na yasiyofuata sheria ni ufisadi.


Tulikuamini, tukasema Tanzania imepata Nyerere mpya lakini imekuwa tofauti.

Tupo njia panda mkuu Magu hatujui jahazi laenda kus au kas.

Tuliza kichwa Fanya maamuzi sahihi usituharibie nchi.

We live once, miaka mitano au kumi inatosha kabisa kuharibu maisha ya watu kutokana na Sera zako.

This is a wake up call

02 : 35
Sep.05.2017

Usiku mwema

mchana toch ,usiku magogo tufanyaje?
 
Hii ni sawa tu na watoto kumlalamikia baba au mama yao kuwa ni mnoko anawapa wakati mgumu. Sawa, kwa uelewa wao mdogo wanakuwa sahihi, lakini kwa aliyepevuka kiakili atagundua kuwa wakifanyacho wazazi kwa watoto ni sahihi. Mwisho wa siku hao hao watoto, wakishafikia umri wa utu uzima, watajirudi na kuanza kuwasifia wazazi wao kwa kuwapa malezi safi kabisa yaliyowajenga kimaadili.
Hakuna mzazi mwenye nia mbaya na makuzi ya mwanae. Vilevile mzazi akifuata maelekezo au malalamiko ya watoto kuhusu malezi kwa hakika ataharibu tu mfumo mzima wa malezi bora.
 
Raisi au kiongozi wa nchi akifuata hayo maneno ya mtaani ya we only live once,sijui maisha ni mafupi,tumia ela ikuzoee,ponda mali kufa kwaja..... etc,nchi itageuka kichaka cha walanguzi.Huo waweza kuwa ukweli lakini usiotakiwa kutiiliwa maanani hata dakika moja na kiongozi yoyote.
 
You people are hopelesses of the kind! Hivi mtu akiwa kiongozi anapaswa kufanya maisha ya watu yawe mazuri au aharibu? Kwani hakuna njia bora zaidi ya kuwatesa watu? Kwa mawazo yenu ni kwamba ili aonekane yu sahihi ni lazima watu wawe fukara? Hizo akili makinikia huwa mnagawiwa wapi wakati wengine wanazo zenye fikra yakinifu? Kwendeni zenu huko!!
 
Ufukara hauletwi na Raisi wa nchi yoyote,wala hakuna Raisi anayegawa pesa,tafuta alternative pale ulipo kwa namna yako,swala la kulalamikia serikali lipo miaka yote na nchi nyingi za Africa,hatupendi kufanya kazi,tunataka shortcut,tunaishi nje ya uwezo wetu,tunapenda kubahatisha,huna uwezo wa kuweka mafuta kwenye gari unanunua gari la CC 2500 au 3000,umetoka chuo juzi juzi unatangaza ndoa fasta na budget mil 25,mshahara laki 8 unamlipia mtoto milioni 2 kwa mwaka school bus laki na 60 kwa mwezi tena nursery.Kumbe ni michongo ya ofisini,uongozi ukibadilika akaingia mwingine mambo yakabadilika unalalamikia serikali,ikusaidieje?,.,.Kwa waliozoea kula kwa jasho na kuishi ndani ya uwezo tunaona ni poa tu.Kila mtu apambane na hali yake hakuna namna.
 
.
Mkuu, tafadhali ainisha hapa hayo maisha mabaya wanayoishi watu. Pia tuwekee hapa ni kwa namna gani kiongozi anawatesa watu.

Pia kumbuka hakuna mtu aliyekatazwa kuwa tajiri. Ufukara wa watu ni kutokana na lifestyle yao mkuu, hakuna kiongozi atakuja awe anagawa pesa kwa watu ili kuwakwamua kiuchumi. Kama mnategemea hicho sahauni, hata mitume wakishuka hawataweza kuwaridhisha.

Mara nyingine watu kama nyie ndio mnapalilia umaskini hapa nchini kwa kuamini na kuhubiri kuwa umaskini unasababishwa na serikali. Tumieni raslimali na nguvu zenu kujikwamua, msingoje serikali iwawekee mabomba ya maziwa na asali.
 
.
Wengi wanaamini maisha bora yanakuja pasi kufanya kazi. Unakuta vijana wanashinda kijiwani halafu ndio wanaongoza kwa kuilalamikia serikali. Wangine wanataka kuishi maisha ya ghali kuliko vipato vyao, na ndio hao walalamikaji wa kila kukicha. badala ya kufikiri kuongeza kipato chao fikira zao zimelenga kukosoa tu kila kifanywacho na mamlaka.
 
Unajieleza mambo meengi utadhani wakili wa serikali au msemaji wa ikulu. Jus 'bear it into your rug-head, ukiwa kiongozi unapaswa kuzijua hali za wananchi na kuzifanya kuwa bora.
Halafu, hakuna mtu anayesema anataka kugawiwa fedha na serikali. Kauli za baada ya uchaguzi ni kama hizo zako. Hivi alivyokuwa anapiga tu-pushapu twa JKT alikuwa anataka nini? Aliahidi nini? Kwa mawazo yako mtu akimsomesha mtoto wake shule ya gharama ni lazima awe amepiga dili? Acheni kuongozwa kwa hisia hasi mtahasiwa!!!
 
Hivi weye unaishi nchi gani hadi nikupe mifano? Acha kuwa mpiga zumari mwenye mapengo. Kila mtu analalamika kuwa maisha yameenda kombo. Haya, weye unaeona yapo sawa, hongera!
 
Mnufaika wa uongozi wa kifashsti lazima utie neno
 

 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…