Kwa jinsi raisi wetu JPM alivyo mwoga kukosolewa, inazidi kumshushia credit.
Ukiwa mwoga maana yake watu wanakuona weak. Alafu mtu mwoga kila siku lazima apige mikwara ili kutisha watu kumbe mwoga.
Kuna tv series moja iitwayo Game of Thrones, kuna mfalme mmoja mwoga aliyekua akiamuru sana na kutoa kauli za kutisha.
Siku moja mfalme huyo, mbele ya babu yake akawa anawatisha watu huku akijipiga piga kifua. Watu walipombishia, aliwatisha na kusema, 'I can kill you all, I AM THE KING.' Babu yake alimcheka na kumwambia, 'ANY KING WHO threats his people by saying I AM THE KING, he is no true king.' Na yule mfalme mwishowe alikuja kuuliwa kirahisi sana akiwa hata hajatawala kwa muda mrefu.
Vivyo hivyo hapa kwetu, Rais anapotoa kauli mbali mbali za kujinadi mfano,' MIMI NI RAIS NINAYEJIAMINI.. 'Hii ni sign ya woga. Wewe fanya kazi alafu wananchi waseme wenyewe kuwa Rasi wetu anajiamini. Hii inafanya watu watambue kuwa he is weak.
Kikwete hakuwa mwoga kukosolewa na bado aliwapiga chini wapinzani kwa kishindo awamu zote mbili. Na sasa anaheshimika ulimwenguni kote.
Rais timiza majukumu yako, kuwa na policies zako, ruhusu demokrasia, wape watu uhuru wao.. Usiwe mwoga kukosolewa
Woga huu ndiyo utakaomfanya ashindwe uchaguzi 2020.