Je msomi anayewatukana watu wake at the same time ni kiongozi?Msomi hawezi toa matusi kama hayo in short wewe sio msomi
Nyie huko ndo mlipiga KURA ZA KIKOLOMIJEHuku kanda ya ziwa tumesubiria meli mbili mpaka basi. Sasa hivi usafiri Wa maji na bandari zimekufa.rais yupo kimya
Mipaka kieleweke , tumbua na huyu alizoea vya kunyonga.John kaza baba hapa tunaanza kuwaona wa Tz halisi.
Hakuna jiwe litakalo salia juu ya jiwe lingine
Me nionacho ni kampeni anafanya kukinusuru chama chaoHuyu siyo kiongozi ni mtawala, hajui anacho kifanya mpaka sasa miaka miwili inaisha.
Hostel za UDSM zitaitwa jina sawa na Chattle AirportNawaza tu. Siku Airport ya Chattle ikiisha ikapata jina kwa heshima kubwa kabisa.
Pombe International Airport.
Dah, hivi waarabu watatua hapo? Teh teh teh
Unazungumzia huduma zipi?Kulala chini hosptal,kushindwa kulipa mishahara,kwa na miundominu mibovu ya elimu?Kushindwa kuwakamata wezi wa almasi ya thamani a USD MIL 200?Akili ya wewe mleta uzi, raisi wako(wetu) na wana upinzani kwa ujumla wake akili zipo group moja utofauti ni mdogo sana hakuna mtu mwenye akili ya tofauti ambaye anaweza kutuletea hayo uliyo yaona kwenye video kwa sasa au kabla ya 2025 tuko mbali sana, tanzania hii ya yasasa kinacho angaliwa nikupata tu huduma za msingi za mwanadamu hizo tafiti za wanaanga bado sana. Sina hakika sana kama upinzani ungeshika dola wangeweza kuuzidi utawala wa JPM.
Leo hii tunaambiwa kama unaishi maisha ya RAHA ZA AJABU utaish kishetani,so tunarud zama zilezile za awam ya 1Ungejua kwanza nini maana ya maendeleo tungeenda pamoja.
Jiulize nchi hii inamiaka zaidi ya hamsini ikiwa huru na ikiwa na siasa ndani yake
Je? Hivi ilivyo ndio matunda ya siasa??
Bahati nzuri mimi nimebahatika kuishi katika vipindi vyoote vya uongozi wa nchi hii toka kupata uhuru mpaka leo, nimeyaona madhara ya vijana wengi kugeuza elimu zao kuwa deni la taifa kuwapa ajira mkuu.
Waliojitambua walijua wajibu wa elimu zao na leo hii wako mbalii vya kutosha.
Kazi zangu zilianzia mbali nje kabisa ya siasa, japo kuna miaka tulifilisiwa lakini hicho kipindi hakitukatisha tamaa
Hatukuthubuti katu wale tuliokutwa na janga hili kukaa chini nakusubiri nini wanasiasa watatufanyia.
Nje na siasa na kutegemea wanasisa wewe unajishughurisha na nini?? Hilo ndio muhimili pekee wa maendeleo yako mwisho yanakuwa ya taifa.
Sasa chama kinachojali maslahi hayo maana ya nchi ni kipi?! Hawa walioimilikisha raslimali za nchi kwa hao wanaoitwa wawekezaji kwa mrabaha wa 3% ?! Bora kufanya majaribio!!Kutoelewa hoja nako ni magonjwa kama magonjwa mengine.
Wewe unataka mimi nikishabikie chama kwa kukionea huruma??
Kisa eti nikicuanga, nikikabidhi nchi kwa majaribio??
Nengependa ukatambua kabisa nchi sio maabara pa kufanyia majaribio ya vyama, tunataka chama kitakachosimamia maslahi ya taifa
Wapo walioishi raha za ajabu kwa njia zisizo harali hao lazima warudi nyuma wajipange, waliutumia unyonge wetu wakajinufaisha lakini mianya hiyo imezibwa hivyo kuishi kama mashetani hao haiepukiki mkuuLeo hii tunaambiwa kama unaishi maisha ya RAHA ZA AJABU utaish kishetani,so tunarud zama zilezile za awam ya 1
Mwl nyerere alishatujengea msingi wetu,mambo ya kichina sijui ya kimarekani ya nn,tanzania mwl alishatujengea mfumo wetu wa kufuataNikupe mifano miwili hai:
MFANO wa 1.
Marekani na nchi za magharibi waliwadharau sana Urusi walipoanzisha kituo chao cha utafiti angani kilichoitwa MIR. Warusi walitumia teknologia rahisi sana ya kupeleka/kurejesha watu na vifaa kwenye MIR yao. Walijifunza mengi kuhusu athari za binadamu kukaa angani kwa muda mrefu.
Wakati wote huu Marekani ilitimbwirika kupeleka mtu mwezini na kumrudisha hai, waliunda space shuttle kupeleka vyombo angani. Mwisho wa siku Wamarekani wakakubali kuwa mission na system za Kirusi ni bora kuliko zao na ndipo wakaomba waungane kujenga hiyo ISS na kutumia system rahisi kama ya Kirusi ya kupeleka na kurudisha wanaanga kwenye ISS.
Mrusi walimdharau mwanzoni lakini mwisho wa siku wakakubali kuwa system za Kirusi ni bora na bei ya chini kuliko zao.
MFANO wa 2.
Kwa kipindi kirefu sana Marekani na Ulaya waliona kuwa mfumo wao wa kibepari (capitalist system) ni bora zaidi na kuwadharau China kuwa mfumo wao wa kijamaa ni duni. Wachina waligangamala na mfumo wao, wengi wakiuita ni wa kidikteta (reminds you of anyone?). Leo hii China imeikaribia marekani kiuchumi na ndio wanaowakopesha Marekani. Marekani inadaiwa mpaka kwenye kope na Wachina.
Imekuaje nchi ya mfumo wa kikomunisti iwapite wenye mfumo wa kibepari? Swali zuri sana.
HITIMISHO:
Usizidharau juhudi za Magufuli katika kuleta maendeleo TZ. Hii nchi ilikuwa haiendelei kwa sababu kila mtu alikuwa anachota toka serikalini tani yake. Sio viongozi wa juu, makampuni ya nje, mpaka mtumishi wa chini kabisa (mesenja) alikuwa amategemea kuchota kutoka hii serikali. Hatua ya kwanza ya kuleta maendeleo ni kuhakikisha hii mianya ya uchotaji rasilmali zetu inazibwa. Magufuli amejaribu kwa kiasi kikubwa kuiziba na ndio maana wale waliokuwa wanategea ule mfumo wa zamani wanapiga kelele kuwa maisha magumu.
Kama Marekani ilivyowakejeli Urusi na Uchina hapo nyuma na sasa wanafuata nyayo zao, vile vile hata watu wanaomkebehi Magufuli kwa sasa watakuja msifia na kufuata nyayo zake hapo baadae.
Hakuna chama mkuu tunachoweza kusema kwa sasa kipo kwa maslahi mapana ya nchi, hivyo kuwategemea wanasiasa ni kutaka kufa masikini wewe na familia au vizazi vyako mkuuSasa chama kinachojali maslahi hayo maana ya nchi ni kipi?! Hawa walioimilikisha raslimali za nchi kwa hao wanaoitwa wawekezaji kwa mrabaha wa 3% ?! Bora kufanya majaribio!!
Kukinusuru na nini?Me nionacho ni kampeni anafanya kukinusuru chama chao
Maendeleo ambayo Magufuli ameyaleta kwa miaka miwili lowassa angeweza au mngekua mnatafuna tu nchi saivi, nyie ikulu sahauni tena ngoja 2020 tuwapunguze kwanza Bungeni.Yeye mwenyewe hana mawazo ya Maendeleo ataletaje maendeleo
Maendeleo gani hayo.kayaleta? Ana yamemgusaje mtu mmoja mmoja hasa mwanachi masikiniMaendeleo ambayo Magufuli ameyaleta kwa miaka miwili lowassa angeweza au mngekua mnatafuna tu nchi saivi, nyie ikulu sahauni tena ngoja 2020 tuwapunguze kwanza Bungeni.
Sijui kama watamruhusu aweke mambo hadharani na kuna uwezekano mkubwa wa kubensananiwa au kutundulisiwa!
Sasa kama hakuna chama tufanyeje?! Turidhike na kinachoendelea?! Kuna haja WaTz wakajitafakari upyaHakuna chama mkuu tunachoweza kusema kwa sasa kipo kwa maslahi mapana ya nchi, hivyo kuwategemea wanasiasa ni kutaka kufa masikini wewe na familia au vizazi vyako mkuu