Akili zako na hao watu wako wa vijiweni ninakili za vijiweni .Kama haya ni ya kweli ambayo wanafanyiwa kabila hili basi nchi yetu tayari imegeuka. Ingawa tunaweza kusema ni ya kweli au siyo ya kweli, vipo vihashiria vinavyosema ni ya kweli.
Wapo watu fulani wakubwa tu wenye makampuni yao ambao walikuwa wamekaa kama kamati fulani kujadili namna ya kukabiliana na kile walichokiita changamoto wanazokabiliana nazo katika biashara. Watu hawa ni wa kabila moja maarufu sana Tanzania linalotoka kanda ya kaskazini. Kiukweli ni maneno ambayo nimeyasikia wakiyaongea tena wanayapa mkazo kwelikweli na mbinu ili kujikwamua.
Jamaa mmoja akasema yeye ni mtu anayeomba tenda mbalimbali za kusambaza vifaa kwenye taasisi za serikali ila amekuwa akipata changamoto ya kunyimwa tenda lakini akakiri wazi kuwa kabla ya utawala wa awamu ya tano mambo hayakuwa hivi! Huyo akadiriki kusema kuwa aliamua kuanza mchakato wa kubadili jina lake la ukoo kwenye documents anazoombea tenda ili tu asikatwe kwa kigezo hicho. Anakiri wazi kuwa walau hilo limeanza kumpa uhai. Naomba ninukuu baadhi ya maneno aliyosema "Siwezi kutumia tena jina la TARIMO kwenye kuomba zabuni. Limekuwa likiwa kikwazo kwangu! Hata wanangu wote nimewaambia wabadili jina lao la ukoo kwenye mambo yao ya shule! Wasitumie kabisaa jina hilo" Mzee huyo kweli akawa anasisitiza hivyo.
Katika maongezi yao kumbe kuna mama mmoja mfanya biashara ambaye alishauriwa asiweke jina lake la asili kwenye makabrasha yake ya kuomba tenda ya mabilioni ya fedha kwenye moja ya mashirika ya serikali. Nadhani aliyemshauri ni mmoja kati ya wazee waliokuwa wakijadiliana katika mjadala huu. Mara lile jina lake likaanza kujadiliwa. Nadhani hili jina linaweza kuwa linatokea Maeneo ya Wilaya ya Moshi. Lakini katika mjadala wao wakagundua kuwa jina hili halifahamiki sana kama jina la kikabila. Mara nikaona mzee mmoja akinyanyua simu na kumpigia yule mama na katika maongezi yake akamuambia "Kwenye documents usiweke jina la ukoo la mume wako! Hilo linajulikana, tumia jina la upande wa baba yako ambalo linaonekana siyo maarufu kulitambua" Kwakweli nimeacha mjadala ukiwa hot sana na inaonekana hili kabila limeanza kukutana na adha kubwakubwa za hapa na pale katika miangaiko yao ya kutafuta riziki.
Pamoja na hayo nalisifu kwa kung'amua hilo na kuanza kutafuta mbinu za kukabiliana na hili jambo.
Hayo ndiyo niliyokutana nayo kijiweni moja ya maficho maalum ya wazee maalum ambapo nilibahatika kuingia hapo baada ya kuwa nimempeleka boss fulani kumkutanisha na mtu ila huu mjadala umechukua muda mrefu nawanajadili kwa umakini na wanaweka uthibitisho! Wengine wanasema kuwa wanapigiwa simu kutoka huko juu na watu wanaowapenda na wamekuwa wakiwapa huo ushauri wa kuondoa kabisa majina ya koo zao au kuyaandika kwa herufi moja tu pale wanapotaka kuomba zabuni mbalimbali.
Hapa ni kazi kwa kazi.Tafuta mbinu ya kupata kazi!
Acha akilinza vijiweni ,lete akili za darasani