Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Tatizo humu Jamiiforums imefikia kipindi tunadharauliana sana. Yaani tunaonana wote tumekuwa wapuuzi wa kiasi hiki.
Kabisa Mkuu umeongea neno.

Pia watu hawajui kusoma nyakati, yaani wengine ilimradi tu maneno yamtoke tu aonekane ka-comment.
 
Mlizoea kufanya kazi kwa mazoea mkajua maisha yataendelea hivyo hivyo kumbe lo! Asante rais wangu magu.
 
Kweli tupu, ila alishachelewa akibana huku tunatokea kulee.

Aliyetangulia katangulia tu
 
Uchochezi huu.
Aliyeleta hii thread ndio mchochezi. Anataka kutuaminsha kuwa Serikali inabagua Kabila Lao. Anadhani Watu wote hawa jui tabia na mambo ya Kilimanjaro ktk kuimarisha ukabila, upendeleo, wizi, ukwepaji kodi n.k. Nawasifu maana wakikaa kupanga mambo yao hawabahatishi na hawaogopi. Ndio maana sasa wameanza kukana Kabila Lao na koo zao. Mbona mnashindwa Biashara na Wakinga kariakoo kama nyie mna akili nyingi za Biashara Nchi hii. Wajinga wanatoka mkoa wa Njombe zamani Iringa hawatoki lake zone. Nyie hamuwezi competition katika mazingira halali ya kila kitu. Kwenye rushwa, wizi, upendeleo mlishinda sana sasa havipo hivyo mnalalamika wenzenu wamezoea haki sasa inapatikana wanashinda tender. Endelea kubadili majina. Hadi 2025 mtajua kushinda kwa haki maana hamtaweza kushindana na penye haki
 
Watuminye tu lakini mkoa wake hauwezi kuwa na foleni kama za kilimanjaro mwezi december, najua roho inamuuma akionaga ile misururu.
Sisi lake zone hatutapanga foleni kwa kuharibu mazingira. Mnajifurahisha na mifoleni huku mnasahau kuwa mnaharibu mazingira. Sisi tunasubiri train ya mwendo kasi SGR yatosha. Riziwani aliwaonya kazikazini hamkuamini
 
Kijana tema mate chini usubiri mshahara wako mwisho wa mwezi si rahisi kuelewa au kuamini haya kama haujawahi kuwa karibu au kufanya haya mambo.
 
Huyo anashiriki biashara nyingine siyo ya government tendering, vigezo vya tenda ya umma zaidi ya specs na vigezo. THE LOWEST BIDDER WINS na zaidi ya hapo, anayeshindwa anatumiwa notification ya ni nani kashinda ili ikilazimu atoe pingamizi. Huyo alikuwa anafanya biashara za deal siyo tendering, hizo zimekuwa biashara kichaa aachane nazo kwa awamu hii.
 
Tukisema Tanganyika kuna ukabila kuna watu wanapinga.....nchi inaelekea ukingoni....
 
True
 
 

Leo ndio nimekubali kuwa kuna waongo waliopitiliza.
Unapoanzisha thread humu jiridhishe pasipo shaka kuwa kuwa unauhakika wa kile uzungumzacho.

Nibahati nzuri pia baadhi ya wanaojibu thread hii ni watu wanao deal na tender procedures.
Nikuhakikishie kuwa awamu hii hao unaowasema ni kina akina Tarimo ni either wamekosa sifa ya kupata zabuni au walizoea kuhonga ili kupata zabuni.

Awamu hii tafadhari elewa kuwa hakuna anaye hatarisha kazi yake kwa ajili ya kumfurahisha mtu fulani hata awe nani.

Professional wa manunuzi naamini wamebadiluka tofauti na huko nyuma ilivyokuwa.

Kwa sasa elewa kuwa anayekosa zabuni ni dhahiri amekosa sifa za zabuni husika.

Hayo mambo ya ukanda katika professional za watu hayapo kabisa mkuu.

Kesho watu wajinga waanza sema ukienda hospital na jina la Nkya huwezi tibiwa kisa ni kabila toka kaskazini.

Shem of you uliyoanzisha hii thread
 
Ivi unapiandika hayo yote hukuwauliza taratibu za mtu kushinda zabuni?
Kwamba aliyeomba zabuni ni kampuni au mtu binafsi,?
Kama ni kammpuni nani anatokea kama muombaji?????
Me naona unaukosefu wa uwelewa katika manunuzi.
Nenda pale PSPTB kachukue hata foundation course utaelewa nini huwa kinafanyika katika kuaward tender
 
Hao watu wakati wenzao wanalalamika kunyimwa fursa,walikuja juu sana kwamba wamesoma,acha wachomolewe,walikua wanapeana tenda kwa kuamgalia majina,sie akina Mwalwisi tulisubiri sana na hatukulia lia
Ukisha zoea kula nyama za watu hutaacha! Kwa ujinga wenu mnadhani mkiwabagua hao ndio mtaacha ujinga wa kuwa na ngombe 10000 lakini bado mnalalia ngozi? acheni siasa za kijinga .
 
Ukisha zoea kula nyama za watu hutaacha! Kwa ujinga wenu mnadhani mkiwabagua hao ndio mtaacha ujinga wa kuwa na ngombe 10000 lakini bado mnalalia ngozi? acheni siasa za kijinga .
Unawaongelea wamasai?
 
Story za vijiweni kama ulivyosema si za kuchukulia seriously sana, ni changamsha genge muda uende.
 
Wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere,kuna wakati ulifika wazee wengi sana wa kichaga walibadili majina ya ukoo kwenye majina ya watoto wao.Kama ambavyo mtoa mada alivyosikia kwenye hayo mazungumzo.UKWELI NI KWAMBA HATA MIMI PAMOJA NA NDUGU ZANGU WOTE KWENYE FAMILIA YETU. HAKUNA HATA MMOJA ANAELITUMIA JINA LA UKOO ALILOKUWA ANALITUMIA BABA YETU,AMBAE ALIKUWA MTUMISHI WA SERIKALI.WATU WENGINE WANAPENDA KUBISHANA TU.MSISAHAU KUWA "LISEMWALO LIPO,NA KAMA HALIPO BALI LAJA".
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…