Namchukia sana Rais John Pombe Magufuli. Sijajua watanzania tulimkosea nini muumba tukapewa adhabu hii nzito kwa miaka hii kumi(kama hataamua kung'ang'ania madarakani)
Binafsi, namchukia mno Rais Magufuli(naamini kumpenda au kumchukia mtu sio kosa, hivyo sitegemei moderators kufuta Uzi wangu huu)
Marry, binadamu ndivyo tulivyo, huwezi kupendwa na wote, hata mimi nilipokuwa mtangazaji wa kipindi cha Kiti Moto, kuna watu walikuwa wanawahi nyumbani kukiangalia ili wasikimisi, na kuna watu, nikitokea tuu, wanazima TV au kuhamisha stesheni!. Ni kama ganda la mua la jana, wewe umelitupa, mwenzako ni neema. Kuna waziri fulani wa Mkapa, mtu wa Musoma, nikamsikia mdada mmoja akisema, hivi mtu unawezaje kumpenda jitu kama lile?!, amimi usiamini, nilipokea taarifa jinsi waziri huyo anavyogombewa na warembo!, hivyo usichokitaka wewe, wenzako wakitafuta!.
Kumchukia mtu sio kosa, ila ni dhambi kwa Mungu!. Amri Kuu ni upendo, hata adui mpende!. Chuki ikizidi, inageuka ugonjwa, hivyo angalia usiugue!.
Kuna wengine wanachukia kwa chuki tuu for no apparent reasons na hakuna kosa lolote!, na wengine ni just chemistry tuu haziendi, hivyo hakuna kosa kumchukia yoyote, ila kosa ni kumjengea chuki ili achukiwe na wengine, huu ni uchochezi.
Vivyo hivyo wewe unavyomchukia, vivyo hivyo ndivyo wengine wanavyompenda hadi kuomba atawale milele!.
Wakati wa JK, alibezwa sana, na kuna watu walifunga na kuomba Mungu atuletee rais dikiteta ili ainyooshe nchi, na kweli Mungu kasikia sala yetu, akatupatia Magufuli.
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba!
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?
P.