Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Are you sure hakuna option nyingine mkuu
Sisi abiria tuko poa na tunajua tunakoelekea na kasi ya dereva wetu sio mbaya.hataki maswali maswali kwanza mpaka akamilishe hizo kilomita 2020.
 
Kwa yanayoendelea nchini Tanzania,je kuna sehemu tunakwenda kama nchi?

Tuendelee na safari ama ni muda sasa wa kushuka chomboni?

Wale wa vyama pendwa...mkitaka kuparuana...uwanja huu hapa
 
Sisi abiria tuko poa na tunajua tunakoelekea na kasi ya dereva wetu sio mbaya.hataki maswali maswali kwanza mpaka akamilishe hizo kilomita 2020.
Huko jikoni mnufaika wa mfumo utoshindwa vipi kusifu na kuabudu,ila kanifurahisha ni ishu ya viroba nampa OK,jinsi watu wasomavo no vingeuwa wengi sana kama kimbilio.
 
Huko jikoni mnufaika wa mfumo utoshindwa vipi kusifu na kuabudu,ila kanifurahisha ni ishu ya viroba nampa OK,jinsi watu wasomavo no vingeuwa wengi sana kama kimbilio.
Sijui ndio nini sasa!.
 
Sisi abiria tuko poa na tunajua tunakoelekea na kasi ya dereva wetu sio mbaya.hataki maswali maswali kwanza mpaka akamilishe hizo kilomita 2020.

Nyie mchekeeni tu huyo dereva wenu. Gari linaenda kwenye Korongo bado mnakenua meno tu. Kwa speed hiyo mtaishia Mochwari au Muhimbili.
 
Nyie mchekeeni tu huyo dereva wenu. Gari linaenda kwenye Korongo bado mnakenua meno tu. Kwa speed hiyo mtaishia Mochwari au Muhimbili.
Tunaimani nae kama nynyi mlivyokuwa na Lowasa sasa kipi cha ajabu.
 
Aliyeanzisha huu uzi alionekana humu mara ya mwisho 11th march 2018! I hope yupo okay kwakweli maana nasikia tunawindana kama digidigi. Aliona mbali.
 
Kwani tawala zilizopita hazikuyaona yote unayoyasema wewe, je ni nini kilifanya mambo yawe shaghalabaghala mpaka tukafikia tulipofikia?
Je waliweka utaratibu gani wa kutimiza na kutekeleza ilani zao, kwanini hapakuwa na matokeo mazuri sana?
Kwa sisi tuliokula chumvi nyingi na kushuhudia tawala zote tangia uhuru, tunamuona Magufuli kama mtawala bora kabisa anayeweza kutuvusha kwa dhati toka sehemu tuliyokuwa tumenasa kama taifa.
Huu umangimeza wa kifisadi wa kufanya mambo kiuoga, ulianza kuota mizizi tangu awamu ya kwanza, ikiwa ni mbinu za kula kombe bila mwanaharamu kuona. Tawala zilizofuata zilipalilia na kulea sana mafisadi. Kulikuwa na kamsemo kao "chama hakimtaji mtu", huu msemo ndiyo ulio wapa kichwa mafisadi na kufanya waliyoyafanya bila hatua zozote za maana kuchukuliwa dhidi yao.
Tunafurahishwa sana na namna ambavyo awamu hii inavyoenda na mambo yote na kufanikiwa kuyakamilisha kwa wakati.
Miaka miwili na nusu tu ya utawala wao imekuwa kama wametawala miaka 10!
Kwa nini tuendelee kuhoji na kubeza mbinu zao walizoamua kuzitumia namna ya kulisikuma gurudumu?
 
ndani ya chama chetu kumejaa wafia chama.....huna haja na mtu aliyethibitiwa ..hivyo ni vema wakateuliwa toka upande uleeee.
 
Ukitaka kujua CCM waliingia makubaliano na wabunge wa CHADEMA waliohama hivi karibuni kutoka majimbo ya UKONGA na MONDULI watazuia kura za maoni kwenye majimbo hayo ila kwa jimbo la KOROGWE ambako Mbunge Stephen Ngonyani(PROFESA MAJI MAREFU) alifariki wataitisha kura za maoni.

Wananchi mkiambiwa kuna agenda ya siri kwa CCM katika mkakati wa kuwarubuni na ama kuwahonga wabunge na madiwani wasiojitambua na kujiamini msishangae! Hapo ndipo CCM MPYA ya Yohana ilipofika.

Kibaya si kuhama kwao, tatizo ni wamehamaje na kwa nini wamerudishwa kugombea ubunge huo huo walio ukataa?
Haya ni matumizi mabaya ya kodi za wavuja jasho kwa koti la Demokrasia ina gharama"
Mark my words, time will tell!!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…