Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
MAjasusi wa CPJ wamenyooshwa na Tanzania itaendelea kuwanyoosha majasusi wa namna hiyo bila kujali kelele za vibaraka wao wa ndani na nje ya nchi.
.Wazri wa mambo ya nje ya Afrca kusini wanakotoka aliwachoma vizuri tu mbona.Huko waliko watakuwa hawana hamu na Tanzania
 
Hebu ngoja kwanza... Amewapa Taifa Stars 50M na wamemwangusha.... afanyaje sasa?

Kampa Ruge 50M ya matibabu bado hamjaridhika?

Hebu tuwe na subira anaweza kumrushia Tundu Lissu visenti vya matibabu...

Ngoja tununue Korosho kwanza wakati jeshi letu likiwadhibiti wanaotorosha fedha za kigeni huko Arusha.
 
Mkuu, asante sana kwa kuonesha uzalendo

"KUDANGANYA KUNAPUNGUZA HESHIMA NA INASHUSHA THAMANI YA ELIMU YAKO. Huyu Governor wa Bank Kuu anasema tuna akiba kubwa ya fedha kuliko nchi yoyote Africa Mashariki....anachekesha!!! Bank of Tanzania ina akiba ya fedha za kigeni kiasi cha US$ 5.6 Billion inatosha kununua huduma na bidhaa (Import) kwa muda wa miezi mitano (5 months), Central Bank of Kenya (CBK) inayo akiba ya US$ 8.3 Billion ambayo inatosha ku-service import kwa miezi 6 na nusu (6.5 months) hizo figures ni za jana ......"

Nasubiri waimba mapambio waje hapa
 
Mkuu, asante sana kwa kuonesha uzalendo

"KUDANGANYA KUNAPUNGUZA HESHIMA NA INASHUSHA THAMANI YA ELIMU YAKO. Huyu Governor wa Bank Kuu anasema tuna akiba kubwa ya fedha kuliko nchi yoyote Africa Mashariki....anachekesha!!! Bank of Tanzania ina akiba ya fedha za kigeni kiasi cha US$ 5.6 Billion inatosha kununua huduma na bidhaa (Import) kwa muda wa miezi mitano (5 months), Central Bank of Kenya (CBK) inayo akiba ya US$ 8.3 Billion ambayo inatosha ku-service import kwa miezi 6 na nusu (6.5 months) hizo figures ni za jana ......"

Nasubiri waimba mapambio waje hapa
Wewe ni Gavana wa benki kuu ya kenya hadi tukuamini unachoongea? Takwimu alitoa Gavana wa benki kuu ya Tanzania tunasubiri kauli ya gavana wa benki kuu ya kenya ndio tuamini sio wewe
 
Wewe ni Gavana wa benki kuu ya kenya hadi tukuamini unachoongea? Takwimu alitoa Gavana wa benki kuu ya Tanzania tunasubiri kauli ya gavana wa benki kuu ya kenya ndio tuamini sio wewe
Mtapata tabu sana kutetea uongo.
Kinyesi cha kobe/paka hata ukifunike vipi kitanuka tu
 
Tatizo linalokera bongo ni kutekana tekana na kupigana marisasi kipuuzi! Hili Raid inapasa alikemee na kulirekebisha kwanguvu stahili. Hayo mengine nimadogo saaana ukifananisha na mazuri mengi yanayofanyika. Cpj kupigwa vibao sio ajabu maana hatujui walikuwa na agenda gani,huwezi kuingia kwa watu na kuleta sarakasi za kijinga ukaachwa hivihivi!! Yapo mazuri menhi yanafanyika muhimu watanzania tujivunie kila hatua tunayopiga badala ya kulalamika kila kukicha utadhani tukovitani! Nchi yetu ni shwari ukijishughulisha unapata riziki vizuri,ukitaka kusoma shule ni tele na nibure nabaadae unakopeshwa,ukiumwa tuna bima unatibiwa fresh,usafiri nirahisi Barbara zikopoa,ndege nk. Biashara ndogondogo ruksaaa,ardhi IPO njenje,umeme umeboreka,ukitaka Marsha utalii hapa ndopake!! sasa tusilielie tupige kazi
 
....Mafisadi wamenyooshwa na mtetezi wao keshajichokea na anakimbiwa hovyo na wanachama.
ESCROW: 324 BIL
EPA: 133 BIL
RADA: 70 BIL
RICHMOND: 260 BIL
TOTAL: 784 BIL
AWAMU YA 5: 1,500 BIL
UNUNUZI WANASIASA: ??
 
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, "Hatuwezi kuwa na Rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli, hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya Rais au Waziri Mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.

Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.

Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu.

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je, anajua jinsi ya kututoa?! Anajua anakotupeleka?

Nimejitahidi kuangalia Bunge ili nione labda Mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.

Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!
Huwezi kupotea kama hujui uendako
 
Kuua umoja wa kitaifa

Kuua demokrasia

Kuua amani ya Watz

Kuongeza uadui kati ya raia na jeshi la polisi

Kuongeza chuki kati ya wana CCM na upinzani Na mengine lukuki.

Kuleta hofu kwa wananchi kuichukia nchi yao kama wapo uhamishoni

Kufilisi Mifuko ya Pensheni ya wastafu

Watu wanaojulikana wanafichwa kwenye giza la wasiojulikana

Watu kuokotwa kwenye viroba

Wananchi kuwa masikini wakutupwa

Kununua wapinzani, na mtoto wa Dada kuwa mlipaji mkuu wa Hazina
 
Haya,tumekusikia mafanikio naona yapo kuwa watu wawili tu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom