Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Msema kweli ni mpenzi wa Mungu, ni lazima tumwambie ukweli Rais wetu hata kama hataki kuusikia.
Haiwezekani tuwe watu wa kusifia tu kila jambo hata kama halina mantiki.
Rais wetu tangu aingie madarakani maisha yamekuwa magumu kupindukia,na bado kila kukicha yanakuwa magumu halafu eti tumsifie kwa lipi?
Sera yake ilikuwa kuua upinzani na siyo kujenga uchumi,hata sisi wauza nyanya tunaitwa wapiga dili,yaani kila anayeteseka na maisha akilalamika ni mpiga dili.
2020 Tumkatae kwenye sanduku la kura.
Hatupo tayari kuendelea na mateso haya.
 
💃🕺...acha waisome nambaaa eee...

....CCM ni ILEILE....

Ulidhani upinzani ndo wanaisoma peke yao?

Sasa hivi CCM wenyewe WANAIANDIKA kabisa achilia mbali kuisoma.

WASTAAFU na wanaoelekea huko woooote ni CCM damdam.
 
Huyu sanduku wala halijali anajua hakubaliki sema uchaguzi haupo2020
Labda kwa nguvu za USA na EU watuchomoleee
 
Mtapata Tabu Sana.. Baba magufuli kaza mwendo usisikilize porojo za wasiolitakia mema taifa
 
Weee kipofu usilete ujanja shikilia fimbo ya anayekuongoza. Uko kwenye right track. Acha kusema umepotea wakati hauoni
 
Upinzani ni kioo cha serikali jinsi inavyofanya kazi zake.
Lakini Magufuli amewaona wapinzani kama maadui wa serikali. Ameanzisha misheni ya kuteketeza upinzani , hususani CHADEMA chama chenye nguvu kubwa, hili liko wazi. Lakini asilolijua Magufuli ni kwamba hatafanikiwa kuuwa upinzani, anajipa tu moyo na kujidanganya ktk misheni yake chafu ya ukandamizaji kwa upinzani. Aangalie mfano wa Ethiopia ambako waziri mkuu wa zamani Haile Mariam alifanya kama yeye lakini leo yuko wapi; alishindwa na sasa waziri mkuu mpya ameanza kurudisha demokrasia iliyoumizwa na dikteta Mariam.

Chadema imejipanga kupambana hadi tone la mwisho la damu, auwe, afunge magerezani kama alivyodai , vyovyote vile mapambano ya kutetea haki, demokrasia, na utawala wa sheria yataendekea.

Kwa MAKAMANDA: "Never give up, when you want to give up ask yourself why you started", waache hao wachumia tumbo waende kujiunga na watesi wetu, ccm, mwisho wa siku watapata malipo yake.
 
Nafikiri njia sahihi ya kuua upinzani ni kuwaletea maendeleo wananchi na kuinua uchumi, hapo wataona upinzani hauna mashiko. Lakini ubabe, ukatili, uuaji, hujuma zinazalisha usugu. Anachokifanya ni kama mtu mwenye tabu nyingi anakunywa pombe ili apate usingizi, akizinduka matatizo yanakuwa mara mbili yake.
 
Njia rahisi ya kuua upinzani, chapa kazi, waletee maendeleo wananchi, wapende raia wako wote, usiwabague, waache wapinzani waongee kama hawaletii uvunjivu wa amani, acha kusikiliza kelele zao, wafutie kesi zao zote zilizo mahakamani za kisiasa, usiwaseme vibaya hata kama wanakusema, jitike kutatua kero za wananchi wako. Ukifanya hivi baada ya miaka miwili wapinzani wote watakuwa wamekwisha na kurudi wenyewe bila hata kusema wananunuliwa na watakaobaki huko watakuheshimu sana. Kuwa na huyu moyo unahitaji msaada kutoka wa Mungu. Biblia inasema "Upendo huvumilia, hufadhili, hauhusudu, haujivuni, haukosi kuwa na adabu, hautafuti mambo yake, hauoni uchungu, hauhesabu mabaya, haufurahii udhalimu, hufurahi pamoja na kweli, huvumilia yote, hustahimili yote (1Wakoritho 13:4-8)"
 
Anaangamiza wafanyakazi kwa kuwapora kiinua mgongo huku akiua soko la bidhaa za kilimo na kufilisi wafanyabiashara
 
Watumishi fanyeni hujuma indirect dhidi ya serikali hii onevu ni miaka 3 hakuna ongezeko la mishahara na maslahi yenu inazidi kandamizwa.
 
Mwambie huyu ndo habari ya mujini
Adobe_Post_20181202_225653.jpeg
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom