Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Ndugu paul alex pole sana mkuu

Nasikitika kukupa taarifa kwamba Magufuri ni hadi 2025.
 

Kiongozi bora anatakakiwa kupunguza Stress...sio kulala na mafaili.
 
KOLA LILILYO (shika / kalia hilo hilo)
 
Mtu anayetembea bila kujua anakoelekea lazima awe ni kichaa
 
Nilijikalia kimya sana kama mnakumbuka nyuzi zangu za nyuma nyuma nilikua namchambua sana na kumkosoa magufuli kuhusu demokrasia na uchumi...mwaka huu nikajipa miezi tisa nikawa nimepumzika tu natafakari na kumwacha nione kama atabadilika au mambo ya kiuchumi kuwa shwari nikawa napost zangu za telaviv na tehran tu wadau wa international forum wananijua nimerudi kuangalia hali ndo imezidi kuwa mbaya na hajabadilika chochote huyu mtu
Ameingia na kafanya mambo ya ajabu sana
.
Ameua uchumi wa kila mtu biashara zote kaharibu

Amewanyima vijana wanyonge ajira


Ameua kilimo ambacho kilikua kimeanza kuleta matumaini toka sera ya kilimo kwanza ianze


Ameua demokrasia


Hapendi kukosolewa


Anafurahia mateso ya wapinzani


Ametumia pesa za wananchi vibaya



Hajali maendeleo ya watu anajali vitu tu mandege na madaraja ni chakula??


Amesababisha sarafu ya tanzania kuporomoka


Ameua biashara zaidi ya laki 7 za maduka hapa nchi kwa mwaka mmoja tu yamefungiwa

Ameharibu chama cha mapinduzi kila kitu na kuwaweka watu wake tu


Pesa za wanyonge za ajira,madawa, maji amechukua badala yake akanunulia mandege


Ameiondoa serikali yake kutoka kujiendesha "kiuwazi" (open government) na kujiendesha kwa siri oneni trilioni 1.5 iko wapi?

Amejenga mazingira ya kuona wakosoaji wake kama maadui

Ameharibu diplomasia ya tanzania na nchi nyinginezo

Anakopa pesa sana nje halafu miradi yenyewe haitarudisha hizo pesa na kinachoumiza zaidi anakopa kwa siri mara nyingi na riba kubwa.....mfano mkopo wa dola milioni 300 ambao riba yake ni dollar milioni 800

Amesababisha mfumuko wa bei na bidhaa nyingi kupana



Nb; Huenda akawa rais wa pekee ambaye utawala wake una mapungufu hiv[emoji1312][emoji1312][emoji1312][emoji1312][emoji1312][emoji1312]kila serikali na kiongozi mara nyingi zinakuepo kasoro na dosari chache il a huyu wetu anazo zote kwa 99% alichokifanya cha maana labda ni hiyo steglers tu maana inaweza kuwa na faida kwa watz vingine vyote kama mandege, madaraja hayana faida kwetu kwa mwendo wa dunia ulivyo angeacha tu kuhusu ndege sasa hivi mashirika mengi yanajiendesha kwa hasara sasa yeye hajifunzi tu?bado ananunua tu ndege???kwenye viwanda ashafeli mapema mno nambieni ni kiwanda kipi cha maana mmekiona?tuambiane mjue 2025 hii nchi alisema itakua ya viwanda nilitarajia nione hata viwanda 100 vikubwa tu mpaka sasa kama mwanzo wa matumaini ila hamna kitu 2020 tuseme ndo ishafika na hamna kiwanda na bado miaka 5 iwe 2025 ya ndoto ya nchi ya viwanda viko wapi??????kwanini tunafanywa watoto?

Ifike mahali tu ukweli usemwe
Magufuli sitokaa nimpigie kura na wala simpendi maana utawala wake hauna faida kwa wanyonge
 
Taratibu mkuu punguza jazba, ishakua ata ufanyeje atabaki kuwa Rais. Mbaya zaidi kura yako haiwezi badilisha chochote maana yule bwn hajawekwa pale kwa kura.
 
Hapo kwenye viwanda umemuonea, kwenye ile symposium iliyoitishwa na sycophantic professors, alisema tayari viwanda 3660 vimeshajengwa. Sasa usije ukaniuliza vimejengwa wapi na vinazalisha nini, mimi sijui, nilisikia tu amesema hivyo.
 
Sema wewe n irrelevant maana ulipoondoka miezi 9 hamna mtu aliyenotice
 
Aisee! si kwenye biashara tu, kila sehemu hali ni mbaya. Pesa hakuna kabisa.
Waajiriwa tangu 2015 mshahara ni uleule, ilhali gharama za maisha zinapanda kila siku.
 
Uzi wa mwaka juzi unaishi mpk sasa, naamin ata wale wapiga vigele gele yamewafika hapaaaaaaaa
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…