Assalaam Alleikhum....
Niseme tu kila nabii na kitabu chake,kila zama zina mambo yake,awamu ya tano/awamu ya jiwe inaongozwa zaidi kimkakati na propaganda,falsafa nyingi sana zimezaliwa,wananchi wamekaririshwa kuamini serikali haikosei,na atakayeona serikali inakosea na akapaza sauti huitwa 'si mzalendo',kwenye uzi huu nitaangazia dhana/kauli mbalimbali ambazo hutumika/zimetumika kama kichaka cha kunyima stahili za mwananchi bila mwananchi mnyonge kugundua kirahisi
1.Uchochezi_kuminya haki ya kutoa maoni/mawazo
2.Watu wasiojulikana_kukwepa jukumu la kuwajibika haswa kwa vyombo vya ulinzi
3.Uhakiki ni Endelevu_kuminya stahili za mtumishi
4.Sio Mzalendo_hii imetumika kuwajengea chuki kwa raia viongozi wanaoikosoa serikali
5.Hapa kazi tu_ni kauli ya muendelezo wa kuminya maslahi ya mtumishi,kuminya haki ya mikusanyiko n.k
6.Uchunguzi/Upelelezi haujakamilika/kesi itaskikizwa mwezi flani_hii ipo kimkakati kukomesha mtu fulani aendelee kusota rumande
7.Serikali ina pesa_ni muendelezo wa kuhadaa umma kwamba mambo yanaenda vizuri hata kama sio kweli.
Unaweza kuongeza dhana au kauli zingine zilizozaliwa/kuasisiwa katika awamu ya Jiwe ambazo yamkini unaziona zipo kipropaganda au kimkakati zaidi...
Sent using
Jamii Forums mobile app