Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Pongezi za dhati kwa JPM na MAHIGA democracy sio msosi UMEME wa uhakika kwangu ni muhimu zaidi aise

Sent using my iPhone using jamiiforum app
 
Katika utafiti wangu nimegundua wafanyakazi wengi wanatamani hats uchaguzi uwe kesho Jiwe aondoke mana katika kipindi chake kimekuwa na mateso makubwa mfano hakuna nyongeza ya mshahara.Hela za likizo watu hawalipwi pia upandishwaji was madaraja umekuwa was kusuasua.
Maoni yangu Serikali iwaangalie watu hawa wanateseka sana pia serikali ijue hawa ndo wapiga kura isifikiri uchaguz ukikaribia watawadanganya kwa kuwapa nyongeza watu wengi wanajitambua kwa sasa.
Note:Mimi sio mfanyakazi in mfanyabiashara nmewasema wafanyakazi sababu wengi nawajua na na najua masahibu yao
 
Hao wafanyakazi wenyewe waongo kwasababu kipindi cha kupiga kura hua hawaendi kupiga kura, nasema hivo kwasababu nimeishi na wafanyakazi wengi na niliziona tabia zao! vile vile mke wangu ni mfanyakazi ukimwambia mambo ya kupiga kura mnakosana kabisa.
 
Karibuni sana great thinkers wote tujadili na kutafakari mapungufu ya kimfumo na uendeshaji wa serikali ya Tanzania kuanzia awamu ya kwanza wakati tunapata uhuru mpaka utawala huu wa John Pombe Magufuli .

Tujadili bila ushabiki wa kisiasa juu ya mapungufu hayo na tutoe mapendekezo yanayoweza kusababisha mapinduzi makubwa ya kimandeleo kwa wananchi na uchumi wa Taifa letu kwa ujumla

Sisi wote ni mashuhuda wazuri wa lindi kubwa la ufukara na muelekeo mbovu wa uchumi wa Taifa letu kwa sasa .

Ninaamini tunaweza kubuni mfumo
Mzuri na ambao unafaa katika Taifa letu ili kujikwamua na kutupeleka katika hatua nyingine kubwa sana .

Wakati tunapata uhuru katika taifa letu kuna nchi kama Korea , Taiwan , Vietnam nk ambazo tulikuwa nazo au tulikuwa tunatofautiana kidogo sana katika level ya kimaendeleo ya kiuchumi . Leo hii sisi ndo wakuomba misaada kwao ,

Je ni wapi tumejikwaa na ni jinsi gani tunaweza kujikwamua kutoka katika giza hili ?

Kuna msemo maarufu unasema "Welevu hujifunza kutoka katika makosa ila wapumbavu huendelea kufanya makosa bila kujifunza chochote toka kwayo " .

ONYO :
Matusi na kejeli hayaruhusiwi , tujadili na kupambana kwa hoja na si matusi

Karibuni wakuu .

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna sababu ya kuzungumzia uchumi wa maraisi waliopita enzi zile hapa tudeal na huyu huyu Mh Mpz wa Mungu/rais wa wanyonge in short raisi wetu tunamuomba aache mentality ya kuamini kila kilio ni matokeo ya wapiga deal,pili namuomba raisi aache kuwatumia TISS kwenye kusaka wakosoaji na badala yake TISS washughurike na infors zitazomsaidia raisi kuinasua nchi iliponasa la sivyo kuna siku chache mbeleni nchi yetu inaweza colapse tukaanza kutafutana ubaya.
NITARUDI

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu ni uzi muhimu, ila jina halijakaa vizuri, kwa sababu wenyewe wenye serikali yao, hawapendi kuambiwa wana mapungufu, hivyo badili title uiite " Kuijadili Changamoto za Awamu ya Tano".
P

Hujasoma kaandika (1-5) au hukumuelewa?

Jana kuna post yako umemuhukumu marehemu kama vile wewe ni Mungu.. ulinishangaza nikawa napiga picha sura yako kama vile nakuona unayatamka.. ulivyoingia kwenye upaparazi kweli umeonyesha upande wako wa ukweli ulivyo.. duh!!!
 
Pia wateule wa raisi waache tabia ya kumuogopa mpaka kupelekea kutoa data za uongo zenye kumfurahisha mhe raisi kisa tu wanaamini raisi wetu hapendi kusikia -ve side ya utawala wake hii itamsaidia kujua ukweli wa kinachoendelea kwenye kila kiunga cha nchi kihalisia zaidi,Kinyume na hapo kuna siku tutaamka mambo hayaendi kwa sababu data za uongo haziwezi kutumika kutoa solution zà ukweli na matokeo yake nchi itapotea mazima,pia mhe rais namuomba aache kuwa mkali kupitiliza kwa wateule na watendaji wake kwa sababu hii tabia inamfanya aogopeke kupitiliza mpaka kufikia point watendaji wake wanakosa maamuzi kwenye mambo madogo madogo na hatimae kupelekea kudanganywa kupitia report ili kumfurahisha yeye.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jambo lengine namuomba mhe Rais wetu wa JMT aweke desturi ya kuwaamini na kuwatumia watalamu wetu kupitia sectors na wizara mbali mbali kwa kufanya hivyo itamsaidia yeye kama mkuu wetu kuja na majibu yanayostahili kwenye tatizo husika na pia apunguze kuamini yeye ni mjuzi wa kila jambo hii itapungu failure ya mipango yetu kama nchi la sivyo tunaona kwenye ndege,korosho,diplomasia na mahusiano ya nchi yetu na nchi wahisani kuyumba na kupelekea nchi yetu kutengwa.


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Hizo nchi ulizozitaja, Korea, Taiwan, Vietnam hawakupiga hatua kimaendeleo kwa kuongea, watu walijituma, wakawa wabunifu na kuwajibika, Tanzania kila kukicha ni kuongea. Hivi kwanini hatujuilizi Wahindi wanaoshi nchi hii wana hali nzuri kiuchumi, lakini sisi waswahili tunalalama? Tunataka kupewa asali na maziwa?
 
Wewe binti mbona uwa unapenda kuchangia visvyoeleweka?? Soma uzi ndo uchangie... Acha kukurupuka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umezungumzia hapo Korea . Nimejifunza kwanini Seul (South Korea) wanafanya vizuri zaidi kiuchumi kuliko Pyongyang (North Korea).

South Korea wamefungua milango na ni ma democrat kwa uhalisia. Hawa act ni uhalisia. Kubwa zaidi viongozi wao hawako juu ya sheria. Wanawajibika kwa matendo yao wakiwa madarakani au baada ya madaraka. Na kwa kweli wako juu. Na mfano mmeona viongozi wao wastaafu wakifishwa mahakamani.

Lakini kwa North Korea (Pyongyang) hawa wamefuata mambo kama ya waTz . Ni uongozi wa mtu moja mungumutu asiyekosolewa. Ni ma Dictator the same na Tz . Ambao chama kimoja kina dictate uelekeo wa nchi , hata kama wameshafail leadership. Wamewekeza kwenye vyombo vya dola (usalama) na si kwenye uchumi wa nchi na wananchi.
Na kweli economically wako chini ukilinganisha na wale wa kusini.

Napendekeza kuwa siasa za ki communist hazitufai, zimetuletea katiba isiyo ya wananchi, bali ya viongozi mamiunguwatu, wasiowajibika kwa matendo yao mema au mabaya wawapo madarakani au wakishastaafu eg. Mikataba mibovu ya madini mafuta na Gas au kuamua bila kushirikisha Bunge .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…