Karibuni sana great thinkers wote tujadili na kutafakari mapungufu ya kimfumo na uendeshaji wa serikali ya Tanzania kuanzia awamu ya kwanza wakati tunapata uhuru mpaka utawala huu wa John Pombe Magufuli .
Tujadili bila ushabiki wa kisiasa juu ya mapungufu hayo na tutoe mapendekezo yanayoweza kusababisha mapinduzi makubwa ya kimandeleo kwa wananchi na uchumi wa Taifa letu kwa ujumla
Sisi wote ni mashuhuda wazuri wa lindi kubwa la ufukara na muelekeo mbovu wa uchumi wa Taifa letu kwa sasa .
Ninaamini tunaweza kubuni mfumo
Mzuri na ambao unafaa katika Taifa letu ili kujikwamua na kutupeleka katika hatua nyingine kubwa sana .
Wakati tunapata uhuru katika taifa letu kuna nchi kama Korea , Taiwan , Vietnam nk ambazo tulikuwa nazo au tulikuwa tunatofautiana kidogo sana katika level ya kimaendeleo ya kiuchumi . Leo hii sisi ndo wakuomba misaada kwao ,
Je ni wapi tumejikwaa na ni jinsi gani tunaweza kujikwamua kutoka katika giza hili ?
Kuna msemo maarufu unasema "Welevu hujifunza kutoka katika makosa ila wapumbavu huendelea kufanya makosa bila kujifunza chochote toka kwayo " .
ONYO :
Matusi na kejeli hayaruhusiwi , tujadili na kupambana kwa hoja na si matusi
Karibuni wakuu .
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using
Jamii Forums mobile app