Salam wote,
Hoja yangu ya leo ni juu ya huyu dereva wetu...kwanza niseme wazi kabisa jamaa ni msanii, lakini pia ana Roho mbaya nafikiri tukitafuta duniani, anashika namba zenye digit Moja.
HAWA MAWAZIRI anao wateua, ni kama MBWA anayepewa NYAMA yenye SUMU! matokeo yake semeni wenyewe.
Mambo yote yanayoharibika hapa NCHINI kuanzia ukusanyaji MBOVU wa pesa, KUHARIBIKA kwa KOROSHO, kushuka kwa MAPATO, kufungwa kwa BIASHARA, watu kupotea kwenda KUSIKO JULIKANA, SIASA CHAFU na harakati chafu za kina MUSIBA......................
Yoote hayo, ni MATOKEO ya maamuzi mabovu ya MAGUFULI na sio MAWAZIRI anaojifanya KUWATUMBUA!!!!Kwanini?? Kwasbabu..
1. Ni nani aliyevuruga utaratibu wa wafanya biashara wa maika yote kununua KOROSHO na akatuma jeshi???
2. Ni nani aliyesema POLICE akiua asishitakiwe bali apandishwe cheo???
3. Ni nani aliyesema HAPANGIWI NA MTU YOYOTE CHA KUFANYA NA UKIMPANGIA NDO UMEHARIBU???
4. Ni nani aliyesema TRA watumie nguvu yoyote kukusanya mapato??
5. Ni nani aliyesema ole wake mkurugenzi atakaye mtangaza mpinzani kuwa mshindi????
Sikilizeni watanzania, POINT ya tatu ni msingi wa matokeo yote na mambo yote yanayoendelea hapa nchini... JIULIZE SWALI? WEWE NI BABA MWENYE NYUMBA NA USHASEMA NDANI YA NYUMBA YAKO HAKUNA WA KUKUPANGIA CHA KUFANYA..UNADHANI SIKU UKIVAA MKANDA UKAVUSHA TUNDU MOJA KUNA MTU ATAKUAMBIA?….Je utakapoenda ukaaibika huko nje unarudi KUWATANDIKA WATOTO kwa kutokukuambia umefunga mkanda VIBAYA??...HUO NI UONEVU..NA kwa level ya NCHI huo ni U-DICTATOR.
MZEE MAGU, MAMBO UMEYAHARIBU MWENYEWE, DANGANYA NYUMBU MIMI NIMEKATAA..TOKA HADHARANI UTUAMBIE una mkakati gani wa kututoa kwenye hili shimo? Wale wanufaikaji, mnakaribishwa pia, ila hapa ni mahali huru pa kujadili mustakabali wa MAMA TANZANIA.