Mkuu nakubali kwamba miundombini ya barabara nk.sio mizuri nchi nzima.Lakini kumbuka kwamba maendeleo ni hatua.Najua pia kwamba kuna kazi kubwa ya kufanya kwenye Kilimo.
Naomba nikutonye kwamba Kilimo kilianza kuharibiwa kwenye awamu ya kwanza.Nadhani unakumbuka utaifishwaji wa mashamba kwenye awamu ya kwanza.Ule ulikuwa mkakati wa kuharibu Kilimo.Kwa ujumla upo mkakati mkubwa wa kuharibu Kilimo,sio Tanzania tu,bali ni mkakati wa dunia nzima.Katika mkakati huu zinatumika mbinu nyingi,tena zingine za siri sana,ambazo Tanzania peke yake haiwezi kuzimudu.
Yapo kwa mfano mabadiliko ya hali ya hewa.Leo mkulima hajui lini apande mahindi,kwa sababu ya mabadiliko haya ya hali ya hewa. Maeneo mengi ambayo vuli kwa kawaida haikuwepo,msimu huu wa mazao vuli imerudi!!Huu ni mkakati wa kumchanganya mkulima kwa makusudi,ili asijue la kufanya,kwa hiyo asifanikiwe katika Kilimo.Kwa mtizamo finyu watu wanaweza kusema mabadiliko haya ni heri,lakini yana nia mbaya sana kwa wakulima.
Wapo wadudu wanaozalishwa kitaalamu ili wawe waharibifu zaidi au wasiweze kuuliwa na dawa kirahisi.Upo uzalishaji wa mazao ambayo yanaharibiwa na wadudu kirahisi.Utakumbuka kwamba mahindi ya zamani yalikuwa yanastahimili wadudu,kwa maana kwamba mbegu zake zilikuwa ngumu na kwa hiyo si rahisi kuharibiwa na wadudu.
Upo mkakati mkubwa wa kuhakikisha kwamba mbegu zetu za asili zinapotea,na tunaingiziwa mbegu za hovyo ambazo kama nilivyosema, zinashambuliwa na wadudu kirahisi.Upo mkakati wa mashirika makubwa kama IMF na World Bank kutupa ushauri mbovu,wakitushari tu-adopt miradi ambayo wao wanajua fika kwamba haina tija kwenye kuboresha Kilimo chetu, lakini sisi kwa ujinga wetu tunaikubali.Ndio maana pamoja na miaka mingi ya kuwa na miradi hiyo ya IMF na World Bank,kilimo chetu kinazidi kurudi nyuma.Jambo hili lilifanyika sana kwenye awamu za tatu na nne.
Mikakati ni mingi mkuu.Inawezekana wataalamu wetu hawajui mikakati hii au wanajua lakini wanashirikiana na wabaya wetu.Kwa hiyo usidhani mambo ni rahisi kama unavyodhani,mambo ni magumu sana.
Nimalizie kwa kusema,kwa kuwa mikakati ya kuharibu Kilimo ni ya kidunia, tunahitaji mikakati ya kidunia ili kuweza kukabiliana nayo.Niseme pia kwamba kwa sababu nilizotangulia kusema, tatizo sio Nyerere,Mzee Ruksa,Mkapa, Kikwete au Magufuli per se.,tatizo ni mchanganyiko wa mambo mengi,ukiwepo mfumo muovu wa kidunia imposed on us.