Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Nothing special in Tz ,poor roads ,heath care , mtu akioongea English sio mzalendo ni ushamba tu bora Africa kusini its a free county with great opportunities

Siitetei Tanzania, ila hiyo Afrika Kusini unayoisifia kuwa na uhuru si huko ndiko wageni waafrika weusi huchezea mapanga, bora niishi kwenye shithole yangu kuliko kuishi nchi ya mazombi kama hao wa Afrika Kusini.
Huko hata ufanye lipi, ipo siku mtafurushwa.
 
Nothing special in Tz ,poor roads ,heath care , mtu akioongea English sio mzalendo ni ushamba tu bora Africa kusini its a free county with great opportunities
Wewe po po ma sasa si uende ukaishi hiyo nchi,
Cha ajabu unaita poor roads wakati ndio unazikatiza daily,
Nyie ndo mnafanya bangi isihalalishwe.
 
Nothing special in Tz ,poor roads ,heath care , mtu akioongea English sio mzalendo ni ushamba tu bora Africa kusini its a free county with great opportunities
Utakuwa umepagawa na mapepo wewe.
 
Miaka mitano umekanyaga haki za watumishi wa Umma, unakiuka waziwazi sheria za Utumishi wa Umma Halaf unatamba kununua ndege kila kukicha, huku unatutukana na kuwatukana Nyerere Hadi Kikwete Kwamba hawakununua Ndege as if Ndege is someone's manhood...

Hata huwazi Kuwa wenzako Hizo hela unazozitumia wewe kwa kificho Bila Bunge wala CAG Kujua wenzako walizitumia kulipa nyongeza ya mishahara kwa watumishi waliopo na kuajiri wengine wapya...

Wewe umedhulumu Haki za watu Kisa unapenda ndege...sawa Mzee wa Midege, See You in the ballot booth next year...UNA DHARAU SANA YAN!
 
Inaoneka una uchungu sana mkuu sio hilo tu la watumishi huyu jamaa baya zaidi ni hili la uminyaji wa democrasia hali iliyofanya vyombo vya habari kutoripoti habari zozote za wapinzani ambao walikuwa wanazungumza vitu vilivyokuwa vinawafungua wajinga ila sasa wajinga wamebaki kushangilia ndege tu bado ndege saba kutimia ndege 14 ni mtaji mzuri kisiasa ila si kimaendeleo
 
Kiukweli anajitahidi kwq mengi tatizo kiburi cha madaraka na kujimwambafai. Abariki mchakato katiba bora bila kushawishi tutamkumbuka na kusamehe yote.
 
Huyu jamaa na wapambe wake, hawajui kuwa pesa ni za watanzania sio za Magufuri kwa hiyo anapozitumia anapaswa kutatua matatizo makubwa ya jamii siyo kutumika kwa utashi wa mtu huku jamii ikiendelea kuteseka miaka nenda rudi kwa vitu ambavyo vina uwezo wa kutatuliwa na Wananchi wakaishi maisha yaliyo bora kabisa. Yaani pesa zitumike zi - reflect matatizo makubwa ya jamii siyo utashi wa Jiwe.
 
Mbona unatokwa povu na ndege tu mengine huyaoni ambayo mnafaidi pia nyie kundi dogo la wafanyakazi miongoni mwa watanzania woote karibu 60mil. Mshahara unatoka kwa wakati kati ya tarehe 21 hadi 25 tofauti na enzi za JK hadi tarehe 5 ndani ya mwezi mwinginea Elimu bure, vituo vya afya na zahanati na hosipitali zimeboreshwa na kujengwa mpya, umeme wauhakika hakuna mgao, barabara, upanuzi wa bandari na meli mpya zinatengenezwa ziwa Victoria, Nyasa na Tanganyika, madaraja, masoko ya kisasa, flyover, barabara za juu bahari ya Hindi, kuthibiti mfumuko wa bei ya vyakula, umeme, mawasiliano n.k, n.k. Hayo yooote hamyaoni? Au mnajiondoa ufahamu ili mpinge? Kalaghabhao
 
Reactions: Ole
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…