Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Ukijua tulikotoka utajua tunakoelekea mimi Nina furaha saaanaaa Leo hii naingia ofisi za umma naulizwa umehudumiwa? Jambo ambalo halikuwepo, makusanyo ya kodi yametia fora tulichezewa mno jamani tunakoelekea ni lami tuuuu


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mzalendo wa kweli kwa Tanzania yetu hii (bila kujali msimamo wake kisiasa au kidini) ni lazima atatetea haki, atapinga uonevu na kukataa ubadhilifu, rushwa na ufisadi.
Magufuli anafanya yote yaliyo kinyume na sifa zinazotakiwa kwa mzalendo.

1. Ni mtu asiefuata sheria (unless sheria hiyo inaelekeza anachokipenda muda huo); mtu anaefuata sheria hawezi kamwe kumuambia mtu "akikupa ten percent ichukue....".

2. Sio mkweli na ni kigeugeu. Mtu aniambie kitu chochote ambacho Magufuli amekifanya consistently kwa pande anaoupenda halafu aka-apply the same thing kwa asiempenda.

3. Ni mbadhilifu; angekuwa anapinga ubadhilifu angependa transparency (bungeni na kwenye vyombo vya habari). Lakini alishasema hadharani kuwa anatamani "malaika ashuke na azime mitandao yote".

Niambie uzalendo wa Magufuli nami nikuonyeshe kuku mwenye miguu mitatu.
 
Nimetoka kumaliza kusoma kitabu cha rais mstaafu Benjamin William Mkapa, kinaitwa "My Life, My Purpose: A Tanzanian President Remembers".

Ndani huko kapiga madongo sana uongozi wa nchi wa siku hizi, na katika madongo hayo, mengi sana yanamgusa Magufuli, ingawa hakumtaja kwa jina.

Nitatafuta muda niandike full review.
 
hakuna jungu dhidi ya Magufuli litakalowafanya wananchi wageuze msimamo
Hilo linawezekana kuwa ni kutokana na ujinga wa wananchi, si uzalendo wa Magufuli.

Tunajua asilimia kubwa ya Watanzania wana elimu ndogo na si wafuatiliaji wa hoja.

Kukubalika sana na wajinga si lazima maana yake iwe una uzalendo sana, inawezekana umejua kuwashikia akili vizuri tu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom