Dr Matola PhD
Platinum Member
- Oct 18, 2010
- 62,453
- 111,795
Kwahiyo sasa wale wabunge wa ccm wanaishi Dar ambao huwa hawaendi majimboni kwao sasa wamepata kisingizio cha kutoitisha mikutano ya wananchi kuwapa milejesho!!Mustakabali wa kinachoendelea kwa sasa utatoka ndani ya ccm yenyewe! Chama kimesurrender kwa mtu mmoja wote wanamsikiliza yeye tu! Anasema hadi 2020 serekali itakuwa imehamia dodoma kesho yake unasikia mawaziri kila mmoja anatamka tarehe ya karibu kuhamia dodoma kumshinda mwenzake, anasema sukari bei elekezi ni 1800 viongozi wote hadi Waziri mkuu nae anacheza wimbo huo bila hata kuhoji, anasema kuna watu walikuwa wanaimba tuna Imani na mtu fulani ningekuwa mimi mwenyekiti ningewapoteza watu wazima wanacheka kama mazuzu hata hawahoji ungewapotezaje? Anasema hapa kazi tu kila mtu anacheza hapa kazi tu wakati hamna kazi, anasema mikutano ya siasa hadi 2020 watu bila kuhoji wanacheza nyimbo yake hadi Waziri mkuu, hamna mwenye courage ya kumwambia umekosea, wakitoka njee ndio unasikia wanaulizana umemwelea muheshimiwa? Wengine ndio unasikia huyu jamaa haeleweki nakwambia hii nchi itamshinda. CCM ya sasa inaendeshwa na mtu mmoja wenye weledi wamebaki kushangilia ili wapate chakula cha kuishi!
Kikwete alikuwa mpole,matokeo yake kuitwa dhaifu na mnyika, na magufuli pia awe mpole basi umekuwa utoto. Alenselema alejaa, kanyaga twende,magufuli anatupeleka kwenye neema.alitakiwa kuwa mpole
no....nchi inaongozwa kwa katiba na sheria tulizojitungia...sio matakwa ya mtu binafsi.Kikwete alikuwa mpole,matokeo yake kuitwa dhaifu na mnyika, na magufuli pia awe mpole basi umekuwa utoto. Alenselema alejaa, kanyaga twende,magufuli anatupeleka kwenye neema.
Ni zaidi ya 80%. Watu wameshamkinainikifuatilia comment za RAIA zaidi ya 60% wamesha mchoka tofauti na alipp kua ananza
RubbishHawa authority ya kulilia demokrasia wakati internally wanaogaragaza.
Huu msala ni wa Mbowe na Chadema (excluding chadema asilia? Ambao demokrasia yao iliminywa ndani ya chama chao). Wapinzani wengine kujiunga kwenye huu msala ni kujipendekeza wasipopendwa. Kama hawaamini wanatumika wajiulize ukawa imeishia wapi na nini utakua mwisho wa ukuta.
Rubbish
Huwa sibishani na watu wa aina yako! Utanigandisha ubongoMagu kawashika pabaya wenye mnaanzisha mambo ya ukuta.
kusema ukweli hao watu unaotaka wakamponye magufuli nawachukia kutoka moyoni.Nikimsikiliza Rais Magufuli napata picha ya mfanyabiashara mdogo wa duka la kaya aliyepewa mtaji na nduguze ili ajikimu yeye na familia yake lkn kabla hata hajaanza kufanya mauzo, anaamua kuanza kutafuna biskuti na kulamba sukari kiasi cha kufikia kula mtaji wote na hatimaye duka sasa kalifunga - Magufuli hakika ameamua kujihujumu na kuufanya Utawala wake kuwa mgumu pasi na sababu.
Basi natamani wapatikane wazee wenye busara (Maaskofu na Masheikh ) wakazungumze naye kwa upole wamkanye tu kwamba speed aliyo nayo ya kuelekea kupotea njia ni kubwa mno - ataivuruga nchi na atajivuruga mwenyewe, halafu wale wazee wa CCM akina Kikwete na akina Mkapa wataanza kumcheka.
Hakika kuna shida kubwa nafsini mwa Rais Magufuli - akikutana na Maaskofu na Masheikh naamini watamfanyia na maombi pia ili apone - Rais huyu anahitaji UPONYAJI.
Hizo si ndio Sera zenu CDM?Hili la JPM sio la kulichekelea kwa wapenda Demokrasia.
Nonsense.Magu kawashika pabaya wenye mnaanzisha mambo ya ukuta.
Mbowe kuandamana jimbo la hai usiku na mchana ili kudumisha democrasia ni kinyume cha katiba ??Inasikitisha na inahuzunisha sana kwa Tanzania kuwa na Rsis wa aina ya Magufuli!
Tangu ameingia madarakani mheshimiwa JPM amekuwa ni mtu wa kutoa matamko yasiyo zingatia Katiba na Sheria na hii ni hatari sana! Rais anayeongoza Taifa lenye takribani watu milioni 50 kwa kuongozwa na hisia au mihemko ni janga kwa Taifa!
Kila kitu au mtu kuna sehemu ya uzuri na ubaya na huo uzuri au ubaya unapimwa kwa kuangalia upande upi unaoelemea mwingine!
Pamoja na sifa ya JPM kupambana na Ufisadi na kusaidia vijana wetu kielimu katika machache mazuri mizani inaelemea kwenye Wingi wa ubaya. Kitendo cha kuendesha nchi bila kufuata Katiba au Sheria ndiyo inabeba ubaya wa JPM kwa asilimia kubwa kama ni kwa aslimia basi ni 60-80%!
Kwa kiwango hichi cha ubaya wa JPM anajitengenezea kaburi lake na la chama chake cha CCM! Laiti JPM angelikaa siku moja na kutafakari kura alizopata mwaka jana 58%(8m votes) zidi ya UKAWA/Lowassa aliyepata 40%(6m votes) kati ya Watz milioni 40 alitakiwa kuwa mpole na kuwaheshimu wale 6m na wengine zaidi ya 25-30m ambao hawakupiga kura kabisa!
Kwanza Rais anapotamba na kuanza kuzuia mikutano ya siasa kwa kisingizio cha Hapa Kazi Tu siyo sawa! Rais anapozuia Bunge la JMT kuonyeshwa LIVE siyo sawa! Rais anapotumbua/fukuza/simamisha kazi watu bila kufuata taratibu na sheria za kazi hiyo si sawa!
Rais anapotisha wanachama tena wa Chama chake watakaompinga kuwapoteza hiyo si sawa!
Rais anapowatisha Wapinzani kuwa yeye Hajaribiwi na atakayejaribu ataona siyo sawa hata kidogo! Hawa Wapinzani wana haki na wana nguvu ya Kikatiba kufanya hivo na si kumjaribu JPM! Wana haki kuwatembelea na kufanya mikutano na wapiga kura wao zaidi ya 6m!Sasa unapozuia wasikutane eti tu kwa sababu hawakupata kura za kuingia Ikulu si sawa! Kwa maana hii JPM hatakiwi kufanya mikutano kwenye Majiji,miji na Majimbo yanayoobgozwa na wapinzani maana hawakumchagua! Je, hiyo ni sawa????
Nimalize kwa kusema kuwa OGOPA SANA MTU ANAYETANGULIZA UMIMI/UBINAFSI kwenye maswala ya kitaifa kana kwamba Tanzania ni nyumbani kwake,mkewe na watoto!
Sina hakika kama JPM amebahatika kusikiliza hotuba za wagombea Urais wa Marekani wa Demokratiki na Republican hasa mama Hillary Clinton ambsye Hotuba yake imesheheni "WE BELIEVE IN....." yaani Tuna amini na tutafanya 123,tuta...tuta....n.k! Na siyo NITA...... na majigambo kibao kama ya"Tanzania ya Magufuli,Serikali ya Magufuli n.k,n.k. Huo ni uzuzu wa kisiasa kutaka kuonyesha kuwa wewe peke yako unaweza na cyo Katiba ya nchi!
Kwa sheria na Katiba hizi anazotunga Rais majukwaani na kuungwa mkonon na Majeshi ya Ulinzi na Usalama ni hatari sana kwa mstakabari wa nchi!
Watu waombe na kusali sana ili Mungu aondoe moyo wa kiburi na jeuri ndani ya Rais wetu vinginevo.........!!!!!????