Habarini Wadau,
Nimeamua kushare na ninyi maajabu ninayotafakari na maswali ninayojiuliza mara kwa mara na nashindwa kujua hatma ya Baba yangu na ya nyumbani kwetu kama familia.
- Baba mkali, Dikteta na Fashisti ila hawezi kukubali hilo kirahisi ila wanawe tunaona kila dalili za sifa hizo.
-Mtu mzima lakini Hashauriki asilani.
Geniouses na Watu maarufu wenye uzoefu wa kutunza familia na uelewa mkubwa ulimwenguni wanashaurika namshangaa huyu mzee hapa home.
- Anapenda sifa huyo...ukitaka atoe matamko mpaka ikifika usiku aote anatoa matamko basi msifie tu.
-Hajui kiingereza...teh teh teh, hapa ndipo baba anaponishangazaga sana...yaani yeye ananisisitiza kujua kuzungumza kiingerezea fasaha ili niweze kuwasiliana na walimwengu na kupata uelewa mpana, kujifunza kwa wengine na kukaribisha maendeleo nyumbani kwangu Lakini YEYE HAJUI na napata aibu awasilianapo na wageni...aibu nakuwa naipata mimi.
Hivi si ni maajabu haya?
Walllah, Natamani ningeweza kumbadilisha huyu baba nipate mwingine.
Nimshaurije huyu baba na namheshimu sana isiwe namchochea tu kwenu.