Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Tatizo tu nazungumzia viwanda wakati tunategemea Mchina ndiyo aje na hivyo viwanda!!
 
Hapa kasi tu. Makampuni ya simu yanatamba jinsi yalivyoongeza kasi ya kutuibia hela.
 
Tatizo umeshachelewa vichwa vyacwatu vimejaa kauli za magufuli
 
Tupotee mara ngapi...sioni Tanzania ya viwanda..naona Tanzania ya zimbabwe
 
Tatizo tu nazungumzia viwanda wakati tunategemea Mchina ndiyo aje na hivyo viwanda!!
Mkuu ccm imeua elimu yetu na pia akili za watanzania walio wengi. Watanzania tumebakia kushabikia wasemayo wanasiasa,walioko madarakani na wasio madaraka,hatuwezi kufikiria tena, kiukweli inauma sana.Mtu anakaririshwa Tanzania ya Magufuli itakuwa ya viwanda ,then watu wasomi kwa wasio soma kama Mimi tukajitoa ufahamu kushabikia bila hata kujiuliza hivyo viwanda atajenga nani na vile tulivyokuwa navyo vilienda wapi, watu hatuwezi fikiri tena,na hata tukifikiri uwezo wetu unaishia Leo,we can't think about tomorrow na ccm kwa uroho wa madaraka wanaendelea kutudanganya misukule yao, elimu yetu wameua sasa sijui kwa akili zao nani atajenga kiwanda kama si mtanzania? Nani atazalisha malighafi za hicho kiwanda kama si mtanzania, Nani atafanyakazi kwenye hicho kiwanda kama si mtanzania? Je huyu mtanzania anaelimu ya kufanya hayo? Sasa masikini wadanganyika hasa wanaccm wakabaki kukaririshwa tu.I hate ccm
 
Tatizo tu nazungumzia viwanda wakati tunategemea Mchina ndiyo aje na hivyo viwanda!!
Kipaumbele cha Elimu,Elimu,Elimu nilikuwa sahihi sana maana elimu ndiyo huzaa viwanda,malighafi,umeme na mambo mengine ila wadanganyika waliozoea kudanganywa,wadanganyika hawa wasiofikiria kesho yao wala ya watoto wao wakaishia kuimba hapa kazi tu huku wakiwa hawana kazi,Tanzania ya viwanda huku wakiwa hawana elimu hata ya kuwawezesha kupata kazi ya ukarani,Tanzania ya viwanda huku wakiendelea kuvuna kilo 100 hadi 200 kwa ekali moja ya pamba,mahindi nk.Wakati mwingine unaweza ukaona aibu kujitambulisha kuwa ni mtanzania
 
Binafsi nadhani ana nia nzuri.

Lakini sidhani anajua anakoelekea.....

Yupo yupo.

Kudhani ni kudhani tu hakuna mantiki kisayansi kwa sababu unaweza kuwa unasukumwa na kutojua au itakadi mgando au hisia tu, kuache kudhani kubaki kudhani tu. Mwenye kazi yake anajua anakoelekea. Go go JPM. tulia tuli!
 
Napita tu ila tusiwe na tabia kama mashabiki Wa mpira , timu ikisajili mchezaji mpya wanataka aanze kufunga magoli asipofanya hivyo bac utasikia mchezaji gani huyu hafai, ni vyema kwa apewe muda kabla ya kumuona hafai, nilichotaka kusema mapinduzi ya kweli huwa hayaji kiurahisi na huwa hayatoi matokeo on sport.
 
wewendio hujui unaelekea wapi hii nchi iligeuka kichaka cha wezi na mafisadi ndio maana watu watu walifikiri wanaweza kununua nchi kwa pesa zao za ufisadi jiulize hao watu wangechukua nchi wangetupeleka wapi
Mkuu inaonekana unawaamini sana viongozi wako wa ccm?siku ukipata ufahamu jiulize hivi,kama kweli ccm wanaipenda nchi hii hayo majipu tunayoambiwa yanatumbuliwa na magufuli yalitokana na nini? Kwa nini hawataki bunge live,je gharama za kuonesha bunge live ni kubwa kuliko kununua v8 na kulihudumia for one year? Je gharama ya kuonesha bunge live ni kubwa kuliko kufuta kinga ya kutokushitakiwa ya marais wasitaafu?
 
Hatukusema tunataka matokeo on the spot ila mwelekeo. Ili tuyafikie hayo matokeo tunahitaji kuona njia ya kutufikisha huko, ndo maana tunasema tumepotea
 
Kudhani ni kudhani tu hakuna mantiki kisayansi kwa sababu unaweza kuwa unasukumwa na kutojua au itakadi mgando au hisia tu, kuache kudhani kubaki kudhani tu. Mwenye kazi yake anajua anakoelekea. Go go JPM. tulia tuli!

Kudhani ni haki yangu na nitaendelea kudhani na hakuna yeyote awezaye kufanya lolote juu ya hilo.
 
Mbona swali la mleta mada liko linaeleweka ila wachangiaji wengi wamekuja wanatokwa na mapovu wakati ukweli ni kuwa jitihada zote zinazofanywa na mheshimiwa rais lakini hatuoni maboresho yoyote katika hali ya uchumi wa wa Tanzania walio wengi wa hali ya kawaida.
Tuache ushabiki tuongee ukweli.
 
Ukiwaambia namna hii wanakasilika sana wanaishia kutaja Majina ya watu....unafanya jambo lile miaka yote then unategemea Jipya kama sio upumbavu nini
 
Kama haina umuhimu basi hata makamu wa Rais asingepewa nafasi ya kwenda huko angebaki kwa shughuli zingine za kitaifa


Kudhani ni haki yangu na nitaendelea kudhani na hakuna yeyote awezaye kufanya lolote juu ya hilo.

Wacha mihemuko dogo! Endelea kudhani (Njozi!) wakati wenzio wanatafakari na kuchukua hatua, go go JPM
 
Binafsi uchumi naona unakuwa kwa asilimia 7.1 na tuna wazidi hata wa kenya hivyo basi tukianza kufanya export kwa wingi na import kwa uchache itapelekea hata thamani ya hela kupanda, japo hata sasa ivi hela imepanda, inflation imepungua mpaka asilimia 5.3 mm naona tunaelekea kuzuri, .. kwa sera ya hapa kazi tu.
 
Uchumi kuanza kukua kwa kasi ni wimbo aliyoanza kuimba Mkapa, JK hadi sasa, nini kimebadilika? Maisha ya watanzania yamebadilikaje kuenda na kukua kwa uchumi?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…