Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ukiangalia hapa jukwaani wewe ni mmoja wa waanzisha post nyingi ikiwemo na kuchangia post. Ila kwa sehemu kubwa ya michango yako unachangia kipuuzi, kishabiki na kejeli. Sioni shida kwani ndio demokrasia, tatizo langu ni kwamba wewe umewekwa na chama chako kukitetea hapa mitandaoni. Nilitaraji kwenye sehemu kama hizi ndio ungekuwa unamwaga nondo na kutolea ufafanuzi mambo mengi ikiwemo na upotoshaji wowote. Unaposhauri watu wakasome ilani na ahadi kuna tofauti gani na kile unachoponda kila mara kwamba EL aliwaambia wananchi wakasome ilani ya ukawa kwenye mitandao!!?
Ni kwanini unakimbilia kwenye kejeli na upuuzi, kirahisi ni kwamba mengi ya hayo yaliyoahidiwa yameahidiwa tu kwa mazoea kwani huwezi kuingia kwenye kampeni bila ahadi wala ilani. Nchi hii haijawahi kuwa na tatizo kwenye upande wa maandishi wala mipango, ila tatizo la nchi liko kwenye utekelezaji, hivyo hapa ndio ulipaswa kuchanganua kwamba tunafikaje huko kwani katika budget inayoendelea kusomwa haiakisi hilo. Sasa watu wanataka ufafanuzi isije ikawa ni kauli mbiu kama nyingine zilizowahi kutolewa na mpaka leo hata wale waliozitoa wanashangaa watu wameendeleaje kuwa wavumilivu kwa kile kilichotokea.
We mbona hujadili mwelekeo wa chadema? Mna Sera ipi kwa sasa, je ya sukari, au kupambana na ufisadi au ipi hasa??Siasa za vyama tumeacha 2015 Wewe mpu..mbavu. hapa tunajadili mwelekeo wa taifa letu. Hayo mawazo yako ya mgando peleka chumbani kwako
CCM wanapenda sana watu wanaofikiri kama wewe HongeraBinafsi uchumi naona unakuwa kwa asilimia 7.1 na tuna wazidi hata wa kenya hivyo basi tukianza kufanya export kwa wingi na import kwa uchache itapelekea hata thamani ya hela kupanda, japo hata sasa ivi hela imepanda, inflation imepungua mpaka asilimia 5.3 mm naona tunaelekea kuzuri, .. kwa sera ya hapa kazi tu.
Hatuamki asubuhi tukasema tunaenda kwenye viwanda, lazima tujiulize vilivyokuwepo kwa nini vilikufa. Tuna mioundombinu ya uhakika? tuna umeme? tuna malighafi? Leo tunalizwa na sukari, tumejiuliza kwa nini hatuwezi kuzalisha sukari ya kutosheleza mahitaji?
hakuna wanaoamini viongozi wa ccm kama ukawa hasa chadema kwani kwa mabaya yote waliyokuwa wakizungumzia ccm sikutegemea kama wanaweza kuwapokea waliowahi kuwa viongozi wa ccm tena walioshika nyazifa za juu kama lowassa na sumaye ambao siku zote walituaminisha sio wasafi
juzi waziri mkuu wake kasema kuna makampuni 52 yanakuja kuwekeza kwrnye Umeme, jpm anasema serikali haitaki tena makampuni yatuuzie Umeme, hawajipanda hawaHatujui kwamba ataanza kuboresha kwanza umeme ndo afwate viwanda..
Au aanze viwanda kwanza ndo afwate umeme...
[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] hii ndo Bongoland
Ni aibu sana mtu kutoa swali kama hili la msingi na likajibiwa na baadhi ya watu kimzaha au kutoa vijibu vya kipuuz au visivyo na mashiko,hoja hujibiwa kwa hoja,kama huna hoja kaa pemben,swali lako ni la muhimu kwa mtu anayeitakia nchi hii mema,na siyo kupelekwa pelekwa kama Kondoo.Hoja yako haina tofauti na hoja niliyomuambia rafiki yangu mmoja kuwa "NCHI YETU INA TAKRIBANI MIAKA 55 HAINA DIRA YA MAENDELEO ILIYOTEKELEZEKA",akabisha akasema Dira ipo,nikamuambia Dira ipo kwenye MAKABRASHA TU.Mwl Nyerere aliwahi kusema "hatuwezi kuwa na rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.
Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya rais au waziri mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida. Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.
Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu
Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je? anajua jinsi ya kututoa? Anajua anakotupeleka? Nimejitahidi kuangalia bunge ili nione labda mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi. Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!
Wanasafiri vyombo tofautijuzi waziri mkuu wake kasema kuna makampuni 52 yanakuja kuwekeza kwrnye Umeme, jpm anasema serikali haitaki tena makampuni yatuuzie Umeme, hawajipanda hawa
Mkuu mi naamin hoja hujibiwa kwa hoja,inashangaza mtu anapojibu kama yupo FB,hii ni hatari sanaHivi ni sehemu gani, jf, au mitandao mingine naweza pata hoja na mada zinazojibiwa Wa hoja. Maana inaonekana kama huwa kuna watu wanatumwa kujaribu kila mjadala sijuini kwa faida ya nani.
Nitarudi bdae
Mkuu umenenaTafsiri ya hiyo ndugu Tindo ni moja tu, mada hii imewaudhi wana CCM kwa kuhoji utendaji na uelekeo wa serikali hii ya CCM!!
Afadhali hata Jakaya Kikwete alipoingia mwanzoni mwa utawala wake, ingalau alikuwa na utaratibu wa kuwa anazungumza na taifa kila mwisho wa mwezi kuelezea uelekeo wa sera zake za kiuchumi pamoja na kutoa ufafanuzi wa some burning issues za wakati husika. Kwa mfano ikitokea watu watu wanajiuliza swali km hili la mleta mada kwamba hivi tunaelekea wapi, alijitokeza na kutoa msimamo na kuwaweka watu ktk mstari hata kama ni kwa kuzuga tu!!
However, utamaduni huu nao ulijifia automatic, kwani pamoja na hayo ukosoaji kwa kila alichokuja nacho ulimfuata nyuma yake!
Huyu yeye hata hayuko huko bali ni purely anaenda enda tu, yupo yupo tu kwa ku create matukio yatakayompa publicity. Ukiona kakaa kimya kwa muda flani watu wanaanza kutojua uwepo wake, basi ujue atatafutiwa tukio na mahali ambapo ataibukia huku akiwa ameambatana na camera za TV ili watu waseme,
".....lol....aisee lima - Magufuli bwana, leo kidogo awatumbue ........".
Yes, hivi ndivyo tunavyopelekwa na tunavyokwenda kama taifa
Mimi na wengine nadhani tunatarajia Rais pamoja na kurejesha nidhamu ktk utumishi wa umma, kusimamia makusanyo ya kodi nk tulitarajia sasa aje na mikakati mahususi ya kuijengea misingi imara kwa kuhakikisha kunakuwa na sheria madhubuti zitakazosimamia na kuyaimarisha haya anayoyaanzisha.
Lakini binafsi sioni chochote kwani anapita mule mule walikopita watangulizi wake, na maana yake iliyo dhahiri ni moja tu, ni kuwa hata yeye atachoka na atashindwa tu na atatahamaki 2020 imebisha hodi mlangoni kwake!!
Well and good. Tunaambiwa kuna ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2015 - 2020 na kwa hiyo tuisome hiyo na ndiyo uelekeo wa Magufuli. Swali kwa hawa wanaosema haya.
Kwani kuna awamu CCM haijawahi kuwa na ilani? Zilileta tofauti gani eti? Mbona ndizo hizo hizo ilani tofauti tofauti za CCM zimekuwa msingi wa malalamiko na majipu haya haya yanayotumbuliwa leo?....This is purely confusion!!
Mkuu kauliza nani anayejua Magufuli anatupeleka wapi,kwa hiyo tegemea majibu kama hayo kwa sababu kuna watu wanajua anakotupeleka na wengine hawajui.Mkuu mi naamin hoja hujibiwa kwa hoja,inashangaza mtu anapojibu kama yupo FB,hii ni hatari sana