Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Mkuu kabla hajachukua form alitakiwa kabisa awe na maono/vision kwamba nikipata nafasi hii nataka kuipeleka nchi hii pale,yaani sasa hivi angekuwa anatushawi/anatuelimisha watanzania il tukubaliane na vision yake badala yake mambo yamekuwa tofauti.Watu m naomba apewe muda sasa sijui huo muda uko wapi wa kumpa.Any way this is Tz ya ccm
Napita tu ila tusiwe na tabia kama mashabiki Wa mpira , timu ikisajili mchezaji mpya wanataka aanze kufunga magoli asipofanya hivyo bac utasikia mchezaji gani huyu hafai, ni vyema kwa apewe muda kabla ya kumuona hafai, nilichotaka kusema mapinduzi ya kweli huwa hayaji kiurahisi na huwa hayatoi matokeo on sport.
 
Hapo uchumi nikimaanisha macro na sio micro , micro tusubiri viwanda.. labda tutaajiriwa au kupata fursa na sisi kuanzisha viwanda vidogo vidogo, kupitia hivyo labda tutaona maisha yakibadilika na kuwa mazuri,. Ila kuona mabadiliko ya magufuli bado sana , ndio uchumi hauwezi kubadilika hivyo, saiv tumbue minyororo ya ufisadi labda tukishakuwa wasafi ndio ataanza kufanya implemention za kukuza uchumi binafsi.
 
Mwl Nyerere aliwahi kusema "hatuwezi kuwa na rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya rais au waziri mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida. Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.
Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je? anajua jinsi ya kututoa? Anajua anakotupeleka? Nimejitahidi kuangalia bunge ili nione labda mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi. Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!
Endelea kutumika kwa kujiehua!
 
Kwani we unajua Mbowe anakokupeleka?
 
Kwa mzungusha mikono kama wewe huwezi jua muelekeo wa nchi...subiri 2020 uwazungushie tena mikono
Jingalao, think critically, JF ni home of GT, ni bora mchango wako ukawa constructive ukifafanua kila mtoa mada alichogusia. Inashangaza mtu unajibu mistari miwili lakini ni pumba tupu. Hii nchi ni yetu sote, kuwa na dira inayoeleweka ni tija kwa ustawi wa nchi. Nchi ikiwa na ustawi ni faida kwa wote, bila kujali mambo ya vyama ambapo mr Jingalao umejipbu kwa muktadha wa ushabiki wa kivyama. Lakini waweza kukuta, muanzisha uzi ni mtu Neutral, lakini anaependa kuona Taifa likivuka,kama ambavyo mimi ni mmoja wa neutral man, Taifa kwanza Itikadi BAADAE
 
Mnaodai hamzungushi mikono tuambieni tunaelekea wapi kiuchumi? Binafsi najaribu kumsoma sielewi hata taifa la viwanda hakuna hatua zozote za tofauti za kumjulisha mtu kwamba tunaelekea kwenye viwanda,tupotupo tu
Chadema taabani bin Hoi. Chezea noti ya lowassa weye
 
Akupeleke kwani wewe umekuwa zombie? Raisi Magufuli hayuko hapa kukupeleka wewe popote pale, bali wewe ndiyo unatakiwa ujipeleke mahali kwingine, wewe ndiyo unatakiwa ujitoe hapo ulipo na kwenda sehemu nyingine, wewe ndiyo unatakiwa ujifungue minyonyoro uliyofungwa na fisadi Lowasa, Mbowe & Co. na kuwa mtu huru Raisi Magufuli hawezi kulifanya hilo na wala siyo kazi yake!
Siasa za vyama tumeacha 2015 Wewe mpu..mbavu. hapa tunajadili mwelekeo wa taifa letu. Hayo mawazo yako ya mgando peleka chumbani kwako
 
Lowassa angeingia madarakani matumaini ya kuishi yangeongezeka..
kwanza ni furaha,kuongozwa na mtu umpendae..
utumbuaji wa majipu ni tamaa tu za hela..
nilidhani wachaga ndio wanapenda sana hela kumbe kuna wengine ukimnyima buku tu koo litakauka kwenye vipaza sauti.
 
Umepotea peke yako kwan rais wetu n baba na kipenz cha wanyonge acha fikira hzo jomba JPM n mzalendo w nchi hii
 
Hadi gharama hospitali ya muhimbili zinatozwa dawa na chakula
 
Jinga lao wakati fulani acha akili yako ifanye kazi kams Mungu Alivokujalia unajua kinachoendelea serikalini! Na unajua hali itakavyojuwa mwakani,acha ushabiki kamanda!
 
Matamko tu kibao utendaji SIFURI
  • Najuta kuchukua form ya kugombea Urais
  • Urais sikupewa na mtu bali nimepewa na Mungu (sijui ni Mungu yupi maana hakuna Mungu wa mafisadi)
  • Nitaweka hadharani salary slip yangu (Siku zinayoyoma tu)
  • Nimejitoa kafara (sijui kajitoa kafara kwa nani maana bado anawakingia kifua akina Lugumi na mafisadi wenzie)
  • Nitarudi kijijini nikachunge ng'ombe
  • Nimepiga marufuku uagizaji wa sukari toka nje (matokeo yake wote tunayajua)
  • Bunge live gharama za shilingi bilioni nne kwa mwaka ni kubwa sana (Mbio za mwenge gharama ni 120 billion)
  • Nchi imeharibiwa na Wazee (Yeye alikuwemo ndani ya serikali kwa zaidi ya miaka 2o huku kapiga kimya "akifanya yake")
Ali mradi ni mtu ambaye haeleweki na nchi inayumba kutokana na kushindwa kwa kiwango cha juu kabisa, mara kawaita Mkapa na Kikwete Ikulu mara kenda kumuona Mkapa nyumbani kwake na yote yanayojiri ni siri yao huku nchi ikiendelea kuyumba.
 
Ukimaliza kushangaa uliza.cdm toka wamesajiiwa na kushiriki chaguzi zote wanaajenda ngapi? Na IPO wameisimamia?
 
Huu utawala hautapga hatua katika maendeleo maana JPM ana dhamira nzuri ila watendaji wake hawatak kubadilika.... ataishia panga pangua na siku znaenda.... hakuna priorities, kipi kianze kipi kimalizwe... bajeti za wizara hazi reflect hali halisi.... uhaba wa maisha utazid
 
Watanzania tuna akili fupi sana ndo maana hatusonge mbele kama taifa na mtu mmoja mmoja, maada ni nzuri inawweza kutusaidia kuibua njia mpya za kumsaidia rais kama ushauri, mtoa mada hana nia mbaya na rais bali anajaribu kutushirikisha tuangalie mwelekeo wa sisi kama taifa, kwa hiyo tuache kumkebehi tuchangie mada kwa mtazamo chanya kwa kutoa michango na ushauri wa kujenga taifa.

Sijui kwa kweli tunafikiri nn juu ya hatima ya tz yetu na watoto wetu, yaan watu wamajaa uchadema na uccm tu, hata ukileta jambo jema utapingwa kwa siasa tu. jibu ni moja tu kumaliza hili. Ni kuchanganya viongozi toka ktk vyama mbalimbali. Natambua katiba inavyosema
 
Mkuu inaonekana unawaamini sana viongozi wako wa ccm?siku ukipata ufahamu jiulize hivi,kama kweli ccm wanaipenda nchi hii hayo majipu tunayoambiwa yanatumbuliwa na magufuli yalitokana na nini? Kwa nini hawataki bunge live,je gharama za kuonesha bunge live ni kubwa kuliko kununua v8 na kulihudumia for one year? Je gharama ya kuonesha bunge live ni kubwa kuliko kufuta kinga ya kutokushitakiwa ya marais wasitaafu?
hakuna wanaoamini viongozi wa ccm kama ukawa hasa chadema kwani kwa mabaya yote waliyokuwa wakizungumzia ccm sikutegemea kama wanaweza kuwapokea waliowahi kuwa viongozi wa ccm tena walioshika nyazifa za juu kama lowassa na sumaye ambao siku zote walituaminisha sio wasafi
 
Back
Top Bottom