Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Kikwete alitudekeza tulimuona mshikaji na alipenda ushirikishaji wa wengine mpaka kukawa na polisi Jamii leo hii tunaambiwa Raia wanaofanya kazi kwenye taasisi za Kipolisi watoke...? Mwanzoni ulivutia wengi sasa hivi tunamkumbuka Kikwete wetu.....
 
Huu uzi modes unatakiwa ufutwe kumuokoa mtoa hoja
 
Na bado mtamkumbuka sana mkwere wetu, si mlisema dhaifu na wengine kutumia nafasi vibaya kwa wizi wa malı za umma. Hiyo ngoma ichezeni kimya kimya msipige kelele tafadhalini
 
Tunajua wakati unapita kutuambia tukuchague ulisema mengi sana, kiukweli maskioni yalikuwa mazuri sana sasa tunajiuliza baada ya kupewa dhamana je unakumbuka ahadi zako? au huzijali tena? au madhali wewe ndio rais wetu u never care any more.

1)mh mpango wa kuanzisha viwanda ukowapi?
viwanda vingapi viko kwenye process kuanza mpk 2020?
2) wapi ulituahidi kua serikali itahama immeadetely mbn kwenye bajeti halikuzungumzwa? hizo hela za kuhama nani kaidhinisha?
3) uliahidi kulinda amani na mshikamano, je kukamata wapinzani, kukamatwa watu wa upinzani kweli kunajenga ya upendo au uadui? mh najua unatambua hakuna amani pasipo haki
4) HIV bomoa bomoa imeishia wapi? Kinondoni,jangwani xilibomolewa vp lile gorofa la. mchungaji lwakatare limeishia wapi?
5) HV elimu bure ndio imeishia elimu michango hasa vijijini

naomba hembu jaribu pitia mtaani kidogo km kipindi kile cha kampeni utapata MREJESHO halisi wa maisha yetu kwa sasa.

kwenye
 
Hayo ni maneno ya mzee KIKWETE leo ndo nimeweza kumkumbuka kweli kwa yale aliyofanya enzi za utawala wake ambapo leo mambo mengi hayafanyiki kama vile 1. UHURU WA HABARI 2. DEMOKRASIA 3. MIKUTANO YA HADHARA 4.STARTIMES HAIONYESHI TENA BURE LOCAL CHANNEL mengine jazieni ila mzee KIKWETE utakumbukwa daima
 
"Mzee umeniachia kila kitu hewa hewa tu" Magufuli akimwambia Kikwete.
 
Hii chenga ya mwili nadhani hata ccm wanaona maruweruwe tuu sasa kazi ipoo
 
President is simple coddiwompling economically and politically! He just started purposefully but with a vague destination !he know he must move the country and he is doing that but had no idea to which direction he should push!
 
Mwl Nyerere aliwahi kusema "hatuwezi kuwa na rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya rais au waziri mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.

Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.

Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je? anajua jinsi ya kututoa?

Anajua anakotupeleka? Nimejitahidi kuangalia bunge ili nione labda mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.

Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!
katika jukwaa hili nakiri kusema hii comment ni best kuisoma kwa mwezi huu
 
Huu ni Mkoa wa tatu sasa katika pitapita zangu wafanyabiashara wadogo wadogo wanalia kweli kweli, mbaya zaidi wamefika mbali na kudai ati angalau "RUSHWA ilifanya pesa ipatikane kwa urahisi". Ukweli ni kwamba tafsiri halisi ya mapambano ya dhidi ya rushwa yanaanza kupoteza uelekeo hasa pale wananchi wasipotoa ushikiano na pekee ikibaki na vita hiyo bila ya kuungwa mkono. Madhara ya kubana matumizi hadi kupitilizi bila ya tathimini ya kina bali kutafuta kusifiwa tayari tunayaona madhara yake.
 
Ndugu zangu watanzania nimekuja mbele zenu ili niwaombe kwa dhati kabisa kwamba Rais wetu anahitaji maombi tena ya kila siku kwa muumba wetu.

Rais wetu na Serikali yake wametoka kabisa kwenye njia kuu ya uongozi tuliokusudia badala yake anafanya mambo yasiyostahili kabisa.

Moja, Rais anaendesha nchi kama ni kampuni yake binafsi, haitaji ushauri kutoka kwa mtu yeyote utadhani anamiliki share za nchi hii asilimia 100.

Pili, Rais anafukuza watumishi ovyo ovyo bila busara wa hekima yoyote hata bila kusikiliza upande wa pili. Mfano ni wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anna Kilango Malecela alifukuzwa bila kujua upande wa pili kulikuwa na tatizo gan. Juzi juzi hapa DED wa Bagamoyo naye katimuliwa kwa kosa la kutoa ushahidi uliokipa ushindi chama cha demokrasia na maendeleo katika majimbo ya Kilombero. Yaani kutoa ushahidi ndo kutoridhika na utendaji wa huyu mama Mbilinyi wakati CCM wenyewe waligawanyika. Ama kweli miaka hii mitano tutaona mengi sana kwa utawala huu.

Tatu, Rais amefanya kosa kubwa katika uteuzi wa MaDED ambao ni wanachama wa CCM na wengi wao walikuwa si watumishi wa Serikali kitu ambacho ni kwenda kinyume na kanuni za utumishi wa Umma. Katika sifa mojawapo ya kuwa DED (District Executive Officer) ni kwanza uwe mtumishi wa Serikali na uwe na uzoefu wa zaidi ya miaka kumi (10) katika utumishi Serikalini, lakini kuna MADED ambao hiyo ndio ajira yao ya kwanza Serikali. Swali je ni lini wataqualify nafasi walizopewa na Mhe. Rais kwa mujibu wa sheria na kanuni za utumishi wa umma?

Nne, Rais kila siku anaanzisha mambo mapya hata kabla ya mambo yaliyotangulia kukamilika. Hili linaweza kumfanya hadi kufikia mwaka 2020 asiwe na kipimo halisi cha maendeleo atakayoyafanya katika kipindi cha miaka mitano ya kwanza na hivyo kuvipa nguvu sana vyama vya upinzani kupata cha kusema. Alianza na timua timua, baadaye watumishi hewa, baadaye wafanyabiasha kulipa kwa EFD, amefunga akaunti za serikali kwenye mabenki ya biashara, ameazisha kodi za ongezeko la thamani (VAT) kwenye biashara mbali mbali na kubwa kuliko ni kuhamia DODOMA.

Tano, Rais ameamuru watumishi wote raia wanaofanya kazi majeshini waondolewe. Hapa ndo matamu. Rais Magufuli hajataka hata kujua kwanini kuna watumishi raia majeshini. Hajataka kujiuliza kwanini Mwalimu Nyerere alianzisha utumishi raia kwenye haya majeshi. Hataki wala hana mpango wa kujua kwenye maasi ya mwaka 1964 pale kambi ya Lugalo aliyetoa taarifa kwamba kuna wanajeshi wameasi ni raia au ni askari. Hataki kutumia hata akili ndogo kwamba watumishi rais ndo walinzi wake kwenye haya majeshi la sivyo itakuwa ni hatari kwa utawala wake.
Rais Magufuli hataki kuamini kuwa kuna umuhimu mkubwa sana kuwepo watumishi raia majeshini ili kutowapa mwanya wa makamanda hawa kukaa pekee yao na kupanga mambo yao bila kuingiliwa na mtu yeyote. Hajui na wala hataki kujua kuwa watumishi raia ni kwa ajili ya usalama wa nchi na wake binafsi. Hataki kujua kuwa bila watumishi raia kuchanganywa jeshini utawala wake utakuwa mashakani muda si mrefu.

Sita, Rais katangaza kuhamisha makao makuu ya nchi kwenda Dodoma kama Ilani ya Chama Cha Mapinduzi inavyotaka, lakini amesahau kuwa kuhamia Dodoma kunahitaji sana hekima na busara. Bila hekima na busara tunaweza kama nchi tukasimama kwa zaidi ya miaka mitano, tushindwe kufanya kitu chochote cha maendeleo kwa muda wote huo tukihangaikia kuhamia Dodoma. Hili jambo linahitaji mpango wa angalau miaka kumi (10), angesema ndani ya miaka kumi atahamia Dodoma angalau ingekuwa sawa ili tunapojipanga kuhamia huko basi watoto nao waendelee kula. Utakuwa baba wa ajabu ambaye unapoamua kujenga nyumba unawataka watoto walale njaa hadi utakapomaliza ujenzi wa nyumba. Baba mwenye mipango mizuri ni yule anayepanga mipango ya maendeleo huku shughuli zingine akiziacha zikiendelea.

Kuhamia Dodoma kunahitaji gharama kubwa sana hasa kuihamisha IKULU sambamba na NGOME ya Kijeshi iliyopo Upanga. Rais Magufuli atambue kuwa Ikulu ni ofisi ya Kijeshi na itahamishwa na wanajeshi wenyewe na ili waihamishe kokote watakakoipeleka wataiunda kwa mtindo wa kijeshi. Nimfahamishe tu kwamba katika nchi yetu ya Tanzania kuna IKULU moja tu ya Magogoni nyingine zote ni ''rest house'' kwahiyo Dodoma hakuna Ikulu kama ambavyo amekuwa akisema.

Mhe. Rais palipo na Ikulu pana Ngome ya Kijeshi ambayo ndiyo inayoratibu mipango na shughuli zote za Ikulu. Ikulu ya Magogoni imeundwa kwa mpangilio ufuatao, Mashariki ya Magogoni kuna Kikosi cha Majini na Kikosi cha Mbagala, Upande wa Kusini kuna vikosi vya Gongolamboto na cha Rada pale External, Upande wa Magharibi kuna kikosi cha Kibaha na Kikosi cha Makongo Juu na Upande wa Kasikazini Kuna Kikosi cha Lugalo na vikosi vingine vidogo vidogo vyote hivi vikiizungunguka Ikulu chini ya uangalizi wa Kikosi Kikuu Jeshi cha NGOME pale Upanga ambacho pia kipo katikati ya vikosi hivi kama ilivyo IKULU. Hivi vikosi havijakaa hivyo kwa bahati mbaya vimepangwa kitaalamu kabisa. Hivyo hivyo ili uhamie Dodoma hawa jamaa watataka Ofisi yao yaani IKULU ya Dodoma ipangwe kama ilivyopangwa Magogoni period. Hivyo jaribu kufikiria gharama za kuunda hivyo vikosi nilivyokutajia Ikulu ya Dodoma ukiondoa Kikosi cha Majini itakuwa ni Tshs. ngapi na itatuchukuwa miaka mingapi sisi kama Taifa kufanya kazi hiyo kwa usalama wako na nchi yetu?

Mwisho, Rais umewakatisha tamaa watumishi wa Umma kwa vitisho vyako vya kila siku, watumishi wa umma kila siku wanatishwa hawana amani kabisa na kazi zao. Usije ukafikiria ni kwanini mapato yanashuka kila mwezi, sababu ni kwamba watumishi wamekuacha wewe na wateule wako mfanye kazi wenyewe kwasababu mnajiona ninyi ni malaika hamkosei. Kila mwezi mapato yatapungua tu kwasababu watumishi wamekosa muelekeo wa maisha yao na familia zao kwa kuwapuuza wao na kuwaamini wagombea uongozi kwamba ndio watumishi waaminifu kuliko wao ambao wameitumikia serikali hii kwa miaka mingi lakini hawaaminiki kabisa.

TAFAKARI SANA NA MUNGU AKUPE HEKIMA NA BUSARA!!!!!!!!

WATANZANIA TUMUOMBEE RAIS WETU HAYUKO SAWA!!!!!!!!
 
ANAANDIKA jenerali ulimwengu



''Tunachagua kama vipofu,kisha tunalalama kama Vichaa. Sasa tuamue; ama tuchague Viongozi wetu kwa umakini au tukae kimya wakati wakitunyanyasa''.........
 
Ukikuwa wapi kwenye utawala uliopita? Wanaoitakia wanaitakia hii nchi mambo mema sisi tunaona yuko kwenye the right track.majipu ndio roho juu.i wish wangekujua uchunguzwe na wewe nina wasiwasi sana na wewe.kumuombea tunamuombea usiku na mchana,mungu azidi kumpa afya njema,na akaze buti.
 
Hao unaosema waliitumikia hii nchi na uzoefu ndio walioifikisha hii nchi mahali pabaya tulipo.wewe ni jipu linahitaji opperation kabisa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom