Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Naomba kujuzwa,ni nani mwenye sauti ya Kumkemea Mkuu wetu wa Nchi endapo ataendelea Kutoa Matamko yenye utata kama lile tamko la Huko Pemba.Na kikatiba richa ya Upinzani ni nini kinaweza chukuliwa kama hatua za awali au ni mwendo wa Kuumizana mpaka miaka Mitano Ipite?
 
Hanna hats hati ya mashitaka,mashahidi,hukumu? Atahukumu yeye hapohapo au?

Baba wa Taifa hayati JK. Nyerere - Mungu amrehemu, aliwahi kutuonya kuwa katiba yetu ilikuwa inauwezo wa kumfanya awe dikteta. Sasa kama tuna katiba inayotoa fursa kwa mtawala kuwa dikteta hilo litashindikanaje?
 
Binafsi nadhani ana nia nzuri.

Lakini sidhani anajua anakoelekea.....

Yupo yupo tu.
Mie zamani nilijua mtu akiwa amekwenda kuishi majuu ni kichwa kweli kweli.yaani wewe nyani hadi leo hujui mkuu ana nia gani .wewe ulitaka uambiwe vipi kwa mfano
,maana mie kila akihutubia namsikia akisema nia yake na matendo yanaonekana wewe huelewi nini?acha hizo we kama umekimbia nchi tuachie wenyewe tuje mdogo mdogo!!
 
Mh.rais wetu hatoweza kufanya anyoyaona kuwa yana mapungufu kwa wakati mmoja,akumbuke kuwa mshika mawili moja huponyoka sasa yeye KASHIKA ZAIDI YA HATA HAYO MAWILI ndio maana tunaona vimbwanga kila kukicha ebu tazama mambo haya yanaweza kufanyika SAMBAMBA kwa rasilimali zetu?
1.Elimu bure na Kupunguza hadha ya kupanda kwa bei ya sukari(lipi limefanikiwa na kuleta tija kwa taifa?)
2.Kuhamia dodoma na Tanzania ya Viwanda (lipi lenye mwelekeo wa kufanikiwa?)
3.Watumishi hewa na vyeti feki na Wapigaji wa pesa za umma(lipi limefanikiwa?)
4.Kutengeneza ajira mpya kwa vijana na kusitisha ajira(lipi limefanikiwa?)
5.Kutoa matamko ya kukera na kuuzi na kuwakamata watu kwa kesi za uchozezi lipi limefanikiwa?
Watanzania sasa wanamkosoa sana rais wao kuliko kumpatia sifa na pongezi mf.humu JF.
 
nimesikiliza kauli kadhaa alizotoa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mheshimiwa john pombe magufuli, moja wapo ya kauli iliyonitisha na kunifanya niogope huko tuendako ni kumshauri mheshimiwa shein kutosain stahiki za maalim seif zilizopo kisheria kwa sababu tu hakupewa mkono msibani. kama baba mlezi ndo kwanza ameongeza mvutano badala kuupunguza mvutano. sidhani kama tutakuwa sahihi kuamini kuwa vyombo vya ulinzi vinatosha kuleta amani na utulivu endapo wananchi watagawanyika. pia binafsi naamini jambo lolote ambalo idadi ya watu wanaolipinga ni sawa au ina karibiana na ile idadi ya watu wanaolikubali basi jambo hilo litatuliwe kwa uangalifu mkubwa sana na ndo maana huwa linatumika neno kutafuta maridhiano kama lina husisha kikundi cha watu wachache basi huwez sikia neno maridhiano. kama mtazamo wangu sio sahihi karibuni kwa hoja. ila pia naomba ieleweke wazi kuwa sio kwamba naunga mkono kitendo cha maalimu seif kutosalimiana na shein
 
Tumepata Mfalme jjuha
 
Alipoingia madarakani alijitambulisha kama ni mcha Mungu. Alikwenda katika madhehebu mbali mbali kusali na kote huko akiomba aombewe ili aongoze kwa haki kwani alisema "kazi hii ni ngumu" Mara nyingi amesikika akisema "msema kweli ni mpenzi wa Mungu"

Kutokana na wito huo watu wa Mungu tuliingia katika maombi ili kumuombea awe na hekima kama alivyoomba mfalme Suleimani ili atawale na kuongoza kwa hekima kubwa na kwa haki. Katika madhehebu mbali mbali ikiwa ni pamoja na hili ninalosali mimi huwa kuna kipengele cha kuiombea serikali na hasa rais katika kila ibada zetu za Jumapili. Sasa cha ajabu, kadiri tunavyoomba ndiyo mambo yanakwenda sivyo ndivyo. Sasa kila akifungua mdomo badala ya kuhubiri amani, upendo, umoja, uvumilivu, upatanisho yeye anahubiri ubabe, utengano, visasi, kukomoana na kwenda kinyume kabisa na katiba na sheria za vyama vya siasa nchini. Sasa mimi sielewi Mungu anakataa maombi yetu au hatuombi vizuri kiasi kwamba inakuwa kinyume chake? Nafikiri wakati umefika sasa wa yeye kujiombea yeye mwenyewe na kutuombea sisi labda tutaona tofauti. Matamshi yake kwenye ziara hii ya visiwani yametutisha, kutushangaza wengi na kutuacha midomo wazi. Jamani tumekosea wapi ili tujirekebishe? Maana huko tuendako naona kama itakuwa ni zaidi ya kupatwa kwa jua. Mungu tusaidie!

Raha na furaha katika familia ni pale baba anapoonekana na kuongea anawaacha katika amani, matumaini na furaha lakini sio kujawa hofu na mashaka kwamba sijui leo itakuwaje? Je akiongea na kuondoka tutabaki na furaha, amani na matumaini au tutabaki na vilio, manung'uniko, mshangao na hofu?

Kuwa baba ni zaidi ya kuwa mwanaume!
 
Nimekuelewa, kumbe dola ikiwa juu export inaweza kuongezeka sababu dola kidogo kwa pesa ya ndani nyingi ambapo wafanya biashara wengi watakimbilia kufanya biashara

sasa kwanini wanauchumi wao wanapima uchumi kwa kupanda kwa thamani ya pesa wakilinganisha na dola? Na mimi ndo niliwakariri wao, ukiona tu uchumi umeyumba wanawahi kusema dola imepanda.
Uvivu wa kufikiri tu.

Dola moja ikiwa thumni, halafu huna production, uchumi utapanda vipi?
 
HII TAREHE NDOO IMESABABISHA WATANZANIA WENGI KULIA MAISHA MAGUMU .

HAKUNA AJIRA

HAKUNA DEMOKRASIA

SOKO BAYA LA MAZAO

KUSHUKA KWA UCHUMI

MAISHA YA WATZ KUWA MAGUMU

WANAFUNZI ELIMU YA JUU KUTAABIKA NA MIKOPO.

WATUMISHI WA UMMA KUNYANYASWA

HII TAREHE KILA MTU HATAISAHAU
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom