Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Ni mwaka mmoja sasa umetimia tangu rais Magufuli aingie Ikulu, katika kipindi hiki yapo mazuri kadhaa amefanya na vijana wanaunga mkono lakini kila kukicha vijana wamepoteza imani na rais Magufuli kwani tangu aingie madarakani hali kwa vijana imezidi kuwa mbaya kwani ndani ya mwaka huu mmoja wa kukaa kwake Ikulu amesimamisha ajira mpya jambo linalo wagusa vijana wengi, na mpaka sasa vijana wengi hawajui kesho yake ikoje.
Mimi ni kijana,na nina IMANI na rais wangu.najua siku za usoni kama si mimi basi watoto wangu watafaidi matunda yake hapa nchini,so labda vijana wa wapi sijui unaowasema!
 
Mkuu mleta mada ameongea hoja moja nzito na ya kuzingatia. AJIRA ni muhimu hii ikipuuziwa itakuja kuisumbua serikali ya awamu ya tano. Nashauri serikali watafute namna ya kuhakiki wakati huohuo waendelee kutoa ajira vinginevyo hali itakuwa mbaya sana miezi michache ijayo. Akitokea kichaa jasiri akahamsisha maandamano ya kupinga ukosefu wa ajira anaweza kupata waunga mkono ambao ni vijana wengi mno kwa sasa. Tatizo ni kuwa wengi hawana familia(mke/mume na watoto) hivyo hawana cha kupoteza watajitoa muhanga. Mimi natumaini Seriali yetu sikivu watalifanyia kazi hili swala maana hili ni bomu linalosubiri kulipuka.
Kwanza tambua kwamba Serikali haina uwezo wa kuajiri kila mtu aliyeko mtaani ambaye ana sifa za kuajiriwa,pili Serikali imeshaajiri lkn hao waajiriwa wako pending kupisha uhakiki unaoendelea ambao bila shaka umekaribia mwisho,tatu hata kama yatatokea maandamano kama unavyobashiri bado haitakua suluhisho.Fahamu pia kua Serikali haiwezi ikafanya kila kitu ambacho kila mmoja wetu anataka overnight.
 
Poleni mliowahi hata kuweka imani zenu!! Nchi hii bila kuingiza mpinzani Ikulu maendeleo tutabaki kuyasikia ughaibuni!!
 
Figisu figisu za mikopo ya elimu ya juu ilikuwa sababu tosha ya kumpa somo mtu.

Lakini ndio basi tena.
 
Sijawahi kuwa na imani na huyu mtu kabisa, narudia kusema tena, kijana yeyote anaeishabikia fisiemu na kuona kuwa inatenda mema basi huyo kijana atakuwa ni mwendawazimu na akizeeka asipokuwa mchawi,basi atakuwa mganga wa kienyeji!
 
Kwanza tambua kwamba Serikali haina uwezo wa kuajiri kila mtu aliyeko mtaani ambaye ana sifa za kuajiriwa,pili Serikali imeshaajiri lkn hao waajiriwa wako pending kupisha uhakiki unaoendelea ambao bila shaka umekaribia mwisho,tatu hata kama yatatokea maandamano kama unavyobashiri bado haitakua suluhisho.Fahamu pia kua Serikali haiwezi ikafanya kila kitu ambacho kila mmoja wetu anataka overnight.
Mkuu kuna hao unaosema wameshaajiriwa lakini wapo pending wanahali mbaya sana kiuchumi, mdogo wa jirani yangu ni muhanga wa hii kitu. Usiombe ikutokee ni afadhari usikie kwa mwenzio, yaani unaenda kazini lakini haulipwi mshahara kwa miezi zaidi ya miwili na ajira yako haijathibitishwa rasmi... Toa maoni ukiwa umevaa viatu vya hawa wadogo zetu. Jambo la pili suala la ajira sio kusema ni jambo la serikali haiwezi kumsikiliza mtu mmoja mmoja. Unajua vijana wangapi wamehitimu elimu ya juu yaani degree, pamoja na diploma na certificates mwaka 2015 na 2016 ambao hawajapata ajira?Tatizo la ajira ni la watu wengi na limeangusha serikali kadhaa mfano Tunisia ile ARAB UPRISING. Hivyo toa maoni kwa uzito wake sio kisiasa au kishabiki. Suala la ajira ndio ajenda kuu ktk medani za siasa kama unataka upate ushindi wa kurudi ikulu, na hii ndio sababu ya wehu wengi walikuwa wanazungushwa mikono juani Jangwani na kudeki barabara kampeni za uchaguzi wa 2015. Mimi nilichangia kama kumsaidia Rais wangu niliyempigia kura na nina mtetea sana hapa JF katika mabandiko mengi anayoshambuliwa lakini mimi sio mnafiki na mnazi anaeona serikali imepotoka na ukweli anaouna lakini hajaribu kuwaeleza ukweli anajaribu kutetea tu. Mimi sio shabiki wa siasa za CCM au CHADENA/UKAWA.
 
Tatizo hapa ni kwateua wasimamizi wasioelewa majukumu yao,ameteua wanasiasa ambao kwa kiasi kikubwa wanawaza kutafuta sifa kwa wananchi ili 2020 wagombee Ubunge. Hawana uzalendo kabisa na wala hawajamwelewa Rais anataka nini.

Kuna uwezekano mkubwa kabisa kufikia 2020 serikali ikashindwa hata kutimiza ahadi zake hata 60%. Sijajua wananchi waliokua wamejiandaa kupokea mabadiliko makubwa kabisa wataambiwa nini?
 
Ni mwaka mmoja sasa umetimia tangu rais Magufuli aingie Ikulu, katika kipindi hiki yapo mazuri kadhaa amefanya na vijana wanaunga mkono lakini kila kukicha vijana wamepoteza imani na rais Magufuli kwani tangu aingie madarakani hali kwa vijana imezidi kuwa mbaya kwani ndani ya mwaka huu mmoja wa kukaa kwake Ikulu amesimamisha ajira mpya jambo linalo wagusa vijana wengi, na mpaka sasa vijana wengi hawajui kesho yake ikoje.
Ana mwaka m'moja kiaje boss......kwani mwaka una siku ngapi au miezi mingapi........maana uchaguzi tu ulikuwa ni october 25 mwaka jana.......na yeye kupewa ofisi ilikuwa ni miezi mingine kadhaa .......sasa sijui huo mwaka ametimiza lini?!
 
Kwanza tambua kwamba Serikali haina uwezo wa kuajiri kila mtu aliyeko mtaani ambaye ana sifa za kuajiriwa,pili Serikali imeshaajiri lkn hao waajiriwa wako pending kupisha uhakiki unaoendelea ambao bila shaka umekaribia mwisho,tatu hata kama yatatokea maandamano kama unavyobashiri bado haitakua suluhisho.Fahamu pia kua Serikali haiwezi ikafanya kila kitu ambacho kila mmoja wetu anataka overnight.
Kwa nchi kama Tanzania ambayo haina uchumi wa viwanda wala haijawekeza sawa sawa katika kilimo serikali ndio hutoa ajira kwa zaidi ya 50% hasa kwa mfumo wetu huu wa elimu ambao haumjengi mtu ktk mtazamo wa kujiajiri.
 
Tatizo hapa ni kwateua wasimamizi wasioelewa majukumu yao,ameteua wanasiasa ambao kwa kiasi kikubwa wanawaza kutafuta sifa kwa wananchi ili 2020 wagombee Ubunge. Hawana uzalendo kabisa na wala hawajamwelewa Rais anataka nini.

Kuna uwezekano mkubwa kabisa kufikia 2020 serikali ikashindwa hata kutimiza ahadi zake hata 60%. Sijajua wananchi waliokua wamejiandaa kupokea mabadiliko makubwa kabisa wataambiwa nini?
wengi wao hawana upeo wanatafuta kiki kwa mzee wa kaya kigezo cha promotion ni kutengeneza tukio.
 
Mkulu kaandaa makada mapema wa kumsaidia ktk uchaguz 2020 anawekeza zaid katika kutawala hadi muda huu bado hali za watanzania ni mbaya sana na miaka inakimbia sana wakija kupata akili tayar 2020.
 
Hii awamu ya tano na haka kamsemo ka serikali ya wanyonge, raisi wa wanyonge, sisi tunajali wanyonge etc! naona kama hakiendani na wanayo-potray, nikawa nachelea kutaka kujua hivi hili neno "wanyonge" hapa linatumika kama kisifa cha jina (adjective) au verb (kitendo)!

Kila mtanzania maskini na tajiri wanaumia na hawaridhishwi na hali iliyopo lakini si wao tu, nadhani hata hiyo serikali haina kitu tangible ambacho wanaweza kusema kuwa hiki ndicho tulichowaaandalia maskini wa nchi hii.

Kama mpo humu please waserikali hebu mnijuze matumizi ya hilo neon!
 
Tangu wagundue namna ya kuiba chaguzi kupitia Tume ya wizi wa kura na chaguzi na mtutu wa bunduki hawana hofu tena ya chaguzi wanajua watashinda tu hata kama watavurunda kwa kiasi gani.

Back
Top Bottom