Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Hili ni ombi kwa mheshimiwa raisi kiukweli si ombi la kupuuzwa nchi inaelekea sehem ambayo si salama kabisa kuna mambo mengi yanatokea mabaya zaidi tunayoyajua na tusiyoyajua huu ni wakati mgumu sana zaidi ya ufikiriavyo kwa taifa letu inabidi tumweke Mungu asimame kutuongoza kuvuta salama katika kipindi hiki hivyo naomba mheshimiwa raisi tangaza japo siku moja tu watanzania wote tufunge Na kuliombea taifa tena kwa kulithamini hilo wewe kama kiongozi ndo uwe wa mfano
Kweli ndugu zangu haya mambo yanayotokea hapa kuna kitu ambacho kinaendelea kisichoonekana kimwili lakini tukiungana kumwomba Mungu naamini atatuepusha Na mengi yanayokuja
Muhimu sana

Mungu yupi
 
wewe kichaa nini yaani na njaa hii unataka kuongeza njaa.Bwana yule tayar kawaomba malaika waje na wewe utatoka

swissme
 
Ni kweli kabisa mambo mengi yanakwenda ovyo. Sura nyingi za wenyenchi hazina siha.. Wakati mwingine nahisi CCM hawakushinda uchaguzi kihalali. Na ndo maana zanzibar wamewakea SERIKALI ya ku force. Ni majanga . Kweli lowasa angepita watu tungekuwa na furaha tu hata kama maisha yangekuwa magumu hivi.. Nirudi kwenye Maada iko haja ya kujitoa kuombea nchi.. Mkuu tuanze mimi na wewe tujitoe Kwa maslahi. Hata dua ZETU zinaweza zikawa na NGUVU
 
Leo umevuta ya wapi? Arusha au ya nyanda za juu kusini?
Au hii imetoka Columbia??
Kwani umeambiwa jamaa ana Mungu?
 
Ni kweli kabisa mambo mengi yanakwenda ovyo. Sura nyingi za wenyenchi hazina siha.. Wakati mwingine nahisi CCM hawakushinda uchaguzi kihalali. Na ndo maana zanzibar wamewakea SERIKALI ya ku force. Ni majanga . Kweli lowasa angepita watu tungekuwa na furaha tu hata kama maisha yangekuwa magumu hivi.. Nirudi kwenye Maada iko haja ya kujitoa kuombea nchi.. Mkuu tuanze mimi na wewe tujitoe Kwa maslahi. Hata dua ZETU zinaweza zikawa na NGUVU
Tujitolee lakini pia wapo humu ambao watapenda kuwa pamoja katika kuliombea taifa tuungane tuliombee taifa letu wanaopinga sijui ni raia wa wapi
 
sioni kama kuna haja ya maombi zaidi ya watu kufanya kazi kwa bidii.....pesa ndo inaleta maendeleo...maana kuna sehemu za ibada hali sio nzuri kwa kuwa hawana pesa lkn maombi wanaomba kama kawa.....anyway ungeweka namba naamin watakupigia ili wakuelezee vizur tunakoenda
 
wewe kichaa nini yaani na njaa hii unataka kuongeza njaa.Bwana yule tayar kawaomba malaika waje na wewe utatoka

swissme
Mkuu ni bora njaa ya siku moja kuliko majanga yanakuja kutokea eti kisa kuogopa njaa
 
sioni kama kuna haja ya maombi zaidi ya watu kufanya kazi kwa bidii.....pesa ndo inaleta maendeleo...maana kuna sehemu za ibada hali sio nzuri kwa kuwa hawana pesa lkn maombi wanaomba kama kawa.....anyway ungeweka namba naamin watakupigia ili wakuelezee vizur tunakoenda
Ishu sio wafanyakazi kufanya kazi kwa bidii hapa ishu ni kuwapoteza hao wafanyakazi sasa hayo maendeleo yatakujaje
 
Ishu sio wafanyakazi kufanya kazi kwa bidii hapa ishu ni kuwapoteza hao wafanyakazi sasa hayo maendeleo yatakujaje
simaanishi wafanyakazi tu...namaanisha wananchi wote kwa ujumla wenye nguvu na uwezo wa kufanya kazi...uwe mkulima...uwe kada yeyote ile
 
Jina "Mungu "limezoeleka Sana ktk vinywa vyetu, kila mara huwa tunalitumia hata kujiapiza hata Kwa mambo ya uongo ,Huwa tunafanya hivyo Kwa lengo moja tu ili Tuaminike kuwa tunachoapa ni kweli tupu...
Huwezi kumsikia mtu akiapa Kwa jina la Shetani maana Shetani anafahamika Kwa uovu wake.
Mh Rais, uliapa kuwa utailinda katiba ,na uliapa mbele ya Mungu ukiwakilishwa na Biblia uliyokuwa umeishika mkononi mwako.
Na hata kabla hujawa rais, ulizunguka nchi nzima kwenye kampeni ukiapa Kwa kutumia jina la Mungu kuwa "Hautatuangusha watanzania ".
Leo hii mh rais umekuwa wa kwanza kutuangusha,katiba uliyoapa kuilinda ndo hiyo umeisigina.
Ni kweli kabisa huu si wakati wa kufanya kampeni maana kampeni ziliisha na wewe ndo rais,lakini mikutano ya kisiasa ipo kikatiba ambayo wewe uliapa kuilinda mbele za Mungu.
Mh rais, wewe ni rais wa watanzania wote bila kujali itikadi za kisiasa walizonazo,lakini kuna mambo yanafanyika mbele za macho ya watu wote na kuashiria wazi kabisa kuwa wasio upande wa chama tawala wana nafasi ndogo Sana kwenye
 
Kuna vitu vingi mhimu vinavochangia mageuzi ya viwanda nchi yoyote moja wapo nI
1.ELIMU
2.ELIMU
3.ELIMU
hii mada ntazungumzia elimu mengine yanafahamika, kama slogan ya RAIS aliyotumia na kutuaminisha kuwa tanzania ya viwanda inakuja ndipo nilipoamua kuhama kozi kwani nimemaliza diploma ya computer science na ikabidi niapply mechanical engineering ili twende sambamba na mkuu wa nchi ila tatizo sasa nimejuta leo hii mkopo wanafunzi wa diploma hatujapa bila sababu yoyote ile .
Mwaka jana wanafunzi waliopata mkopo ni 48,634 na diploma pia walipewa mkopo mpaka kozi ambazo sio kipaumbele et mwaka huu mkopo wanafunzi 25,000 nusu ya mwaka jana. Naumia sana mm kama diploma holder niliyekosa mkopo tena kozi ya kipaumbele kabisa inayoendana na tanzania ya viwanda kama slogan ya RAIS MAGUFURI yaan mechanical engineering. Kwa mwendo huu nimeanza kuona kabisa hakuna tanzania ya viwanda ila huu wizi na uongo tu unaenezwa na serikali ya mheshimiwa.
 
viwanda vitatoka wapi ilihali kila kukicha tunaambiwa eti ni "maelekezo kutoka juu" sasa na viwanda vinatoka juu?
 
Mnaodai hamzungushi mikono tuambieni tunaelekea wapi kiuchumi? Binafsi najaribu kumsoma sielewi hata taifa la viwanda hakuna hatua zozote za tofauti za kumjulisha mtu kwamba tunaelekea kwenye viwanda,tupotupo tu
Utaelewa tu ana mwaka mmoja tu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom