Hili la kutumia nguvu kwa kila kitu sijui limekaaje, kudharau taaluma ya Mtu sijui ni nini kitatokea, sijui, naona mbele kuna hatari kubwa inakuja.
Moja: Sijui kama kazi hizi za kulazimishana bila kuangalia changamoto za kazi yenyewe zitafanyika kwa Moyo thabiti,
Mwalimu unamnyanyasa na kumpa maneno ya Dharau,
Dactari hivyohovyo,
Mwanasheria,
Majaji,
Wabunge,
Wenyeviti wa Serikali za Mitaa,
Madiwani,
Wote hawa katika awamu hii ya Tano kazi zao ni kudharaulika tu, hawana umuhimu kwa Jamii ya Watanzania,
Awamu hii Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa wilaya ndio Viongozi wa kuongea na kufanya chochote,
Sasa kwa kifupi nikiangalia Picha ya mbele endapo hawa wanaodharaulika wakaamua au wakashindwa kufanya kazi zile za Taaruma zao ipasavyo kitatokea nini, naona kuna matokeo mabaya sana.
Mungu atusaidie, CCM tunaomba hii Miaka 5 ni mingi sana, inatosha kuangamiza, kutesa, Kudumaza kila kitu ambacho kimetengenezwa kwa Miaka 50 ilyo pita, kwanza Umoja unakufa, Ubinadamu unakufa, Chuki.
Upinzani wameliona hilo ndio maana wanajaribu kutumia Mahakama kutetea Wananchi , ingawaje mahakama zilionekana kutumika kukandamiza Haki sasahivi mapambano yameongezeka sana. Walitaka kutumia njia za Maandamano na Mikutano lakini waligundua huyu mtu hana huruma na kumwaga damu za Watanzania, Hicho ndicho kilichopo, Sasa kama kiongozi wa nchi anakuwa hana huruma na kumwaga damu na Mpinzania kuwa na huruma sijui tunawezaje kuwa salama, CCM sitaki kuwaambia mfanye nini, mnajua usalama wa Chama chenu ni upi, Chama kazi yake kutetea haki ya Mwananchi? au kukandamiza Haki ya Mwananchi.
Kwa pamoja tujenge Nchi yetu, CCM, Chadema, Cuf, NCCR na wenyineo,
Asanteni