Wengi tunaumizwa na serikali hii ya awamu ya tano. Tunakatishwa tamaa na serikali hii ya awamu ya tano. Tunapuuzwa. Tunaonewa. Tunadhalilishwa. Tunadhihakiwa. Ndugu zetu wanapotea. Ndugu zetu wanaumizwa. Ndugu zetu wananyanyaswa. Ndugu zetu wanatishwa. Hakuna wa kuwatetea. Hakuna anayejali.
Tupeanae faraja. Tujengane kisaikolojia. Tuungane kwa maumivu yetu. Tutafute majibu kwa pamoja. Tutafute adhabu inayostahili kwa serikali ya awamu ya tano.
Wafanyabiashara. Mama ntilie. Wafanyakaz/watumishi. Wakulima. Wafugaji. Wavuvi. Madereva. Wakandarasi. Vijana. Akina mama. Wazee. Wasomi. Wanaolala njaa. Tuungane, tuiadhibu CCM na serikali yake.
Hatuwezi kukombolewa na vyama vya upinzani. Hatuwezi kukombolewa na wazungu. Hatuwezi kukombolewa na Mbowe ,Maalim ,Lipumba wala Zitto. Hatuwezi kukombolewa na CHADEMA, CCM, CUF. Hatuwezi kukombolewa na Rais Magufuli.
Njia pekee ya kujikomboa ni kuungana. Ni kupambana na kila fikra hasi bila kujali imetolewa na nani. Njia pekee ni kuamua leo ni namna gani tuendeshwe sio wao watuamulie namna gani watuendeshe. Muda ni sasa. Tuchukue hatua. Tujikomboe.
Kila kundi tuna wajibu wa kujikomboa kwa kuweka tofauti zetu pembeni na kuungana.
Mungu ibariki Tanzania. Mungu ibariki Africa.