Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Ninamkumbuka mzee kingunge alisema huyu alistahili kuwa mnyampala wa Barabara na si vinginevyo sasa yametimia
 
Hahaha...umetisha kamanda!

Mkuu kupimwa UTI lazima uwe na ELIMU ya TL vinginevyo utapata majibu ya Masogange na mkemia hajui rangi ya mkojo wake.

Acha kabisa Tanzania ya V-wonder 2015-2020
 
Napatwa na kwikwi, akitajwa huyu nduli,
Naishia kusema kwi, kwa huyu baladhuli,
Bora tuseme hasimikwi, kwa ijayo serikali.
Watanzania tutajuta, ng'ombe kuikabidhi sukani.

Wewe naona unamtafuta mkulu maana kule kwingine umemwita ng'ombe na huku nduli. Mkuu una hasira mbaya sana na huyu mtu.
 
"Memori fullu!"
Ukigeuka hivi, huyu kacharazwa na Dc, ukitaka kujikuna, huyu kanyimwa dhamana, ukisema uanze kusali, huyu kasepa na rambirambi! Ukitaka kwenda kuoga, huyu anazuia sabuni hadi ulipe deni la ugoro... Ukitaka kuketi kula, huyu ashaagiza uhame mji bila ndala!

Ukitaka kujipumzisha baada ya stress za mchana, buldoza linachungulia dirishani! Ukisema ushike mswaki upunguze wadudu mdomoni, mkemia anataka mkojo apime wadudu wa mdomoni...

Ukitaka kula makande, huyu ashazuia mahindi anasema yasagwe! Ukiinama ufunge kamba za viatu, noah ishafunga breki miguuni... Ukisema ufanye kazi kwa bidii, huyu anataka ukrem jina lake... Ukitaka kulia kwa ghadhabu, unawekwa korokoroni kwa kupigia watu kelele isiyowahusu....

Ukitaka kuandika shairi lako, washakudaka na sheria ya mitandao... Ukitaka kupanda bajaji, washakulazimisha upande pangaboi... Ukimdai bosi mshahara wako, ashakutupia jembe ukalime... Ukikodisha shamba ukalima, jua lishaizidi mvua na hakuna msaada....

Ukitaka kumpeleka mwanao chuo, washakuitia mkopo kwenye ofisi za chama... Ukitaka kwenda Zimbabwe, usharudishwa na ushuzi wa babalao.... Ukitaka kuwa karibu na mema ya nchi, ushaulizwa kama wewe ni "sibling".'.. Ukitaka haki yako, washakulazimisha usimamishe msafara wake....

Ukitaka "kupupu," ushadakwa uoneshe risiti ulikula wapi.... Ukitaka jshshsjsosks, jshdjejsie????(peni imegoma ngoja nijaribishe tena...) nsnsjshdeueuhdisisksks! (Naenda dukani kusaka nyingine)

Ila nikirudi, Hasira zote nazimaliza kwa marafiki wanaopost picha kuanzia januari hadi disemba...... No, sio hao... Ngoja.... Nimekumbuka... Wale wanaohamisha posti za wenzao hawataki kushea, wanazikopi na kuzifanya zao.... Nawablokuuuuuuuuuuuuu hadi vidole viume....

Memorifufjfjdirirrirkkkmmldjdjdieiss!'&#&#$&÷&#
mkuu, popote ulipo...heshima kwako kamanda
 
Wewe naona unamtafuta mkulu maana kule kwingine umemwita ng'ombe na huku nduli. Mkuu una hasira mbaya sana na huyu mtu.
Wewe hujabomolewa nyumba yako iliyopo mita 120 toka hifadhi ya barabara, ndiyo maana unasema hivyo.
 
Wewe hujabomolewa nyumba yako iliyopo mita 120 toka hifadhi ya barabara, ndiyo maana unasema hivyo.

Usijali mkuu tupo pamoja ila nilishangazwa tu na jinsi unavyombatiza mshikaji majina lukuki. Naelewa kama taifa tupo kwenye kipindi kigumu sana.
 
Usimwige Kagame, mwenzio aliingia Kijeshi, na sii Kijeshi tu, Kabila lake ni kubwa na kalibia Jeshi zima ni kabila lake,

Maana hii iko wazi tu, ili uweze kumkandamiza mtu lazima uwe na Vyanzo na Nyenzo.

Tanzania hapa Baba CCM Mtoto Chadema, Mtoto CCM Baba Chadema na hakuna mazingira ya kumzuia kuingia Chama fulani maana Tanzania vyama vyetu sii vya kikabila wala udini.

Sasa nikwambieni Serikali ya tano,
Baba akiwa CCM, Mtoto Chadema, Mtoto mwingine Mwanajeshi, mwingine Polisi, Je ikitokea Vita unategemea huyu Mwanajeshi au Polisi kwenye hii familia atamshambulia Baba alioko CCM au Kaka yake au Mdogo wake alioko Chadema? Huo ndio Ugumu wa kufanya ukandamizaji kwenye Nchi ambayo ilishajengwa huru, Kaa ukujua ukifanikiwa uivuruga nchi kama hii ni vigumu kuiunganisha maana utakuwa tayari umegombanisha ndugu kwa ndugu.

Kuweni makini awamu ya tano.
 
Just imagine,kwa hii performance ya JPM ingekuwaje kama Lowassa na wanasiasa wengine wangekuwa huru kueleza umma? JPM angeweza kutembelea sehemu gani nchi na watu wakawa na hamu ya kumsikia?
Nampongeza mh. JPM kuwazuia wanasiasa wenye mvuto na weledi wa kuelewesha wananchi juu ya utendaji wa mashaka wa serikali kuna mfanya aendelee kupata heshima kwa baadhi ya wananchi. Ni vizuri JPM akaachiwa utulivu wa kutumikia nafasi yake kwa kiwango chake kwa muda huu mfupi. Lowassa na wenzake warekodi na watatueleza muda mwafaka.
 
Kwahiyo unamanisha Lowasa angemfunika JPM kama angeruhusiwa kufanya mikutano yake ya kisiasa...!?
 
WAKATI MWINGINE NI HERI MUWE MNAPUMZISHA AKILI KULIKO KUJA NA PUMBA HIZI. LOWASSA ATUELEZE NINI KAMA AMESHINDWA KUTUAMBIA PESA ZA RICHMOND NANI KALA? BE CAREFUL UNAPOLETA MAADA HAPA LA SIVYO NENDA HUKO FB
 
Akupeleke kwani wewe umekuwa zombie? Raisi Magufuli hayuko hapa kukupeleka wewe popote pale, bali wewe ndiyo unatakiwa ujipeleke mahali kwingine, wewe ndiyo unatakiwa ujitoe hapo ulipo na kwenda sehemu nyingine, wewe ndiyo unatakiwa ujifungue minyonyoro uliyofungwa na fisadi Lowasa, Mbowe & Co. na kuwa mtu huru Raisi Magufuli hawezi kulifanya hilo na wala siyo kazi yake!
hakikaa
 
Kama ulikuwa hujui>>Kuna trick moja inaitwa "Divert/distract people's attention" ambayo inatumiwa sana na wanasiasa na watu maarufu duniani kwa manufaa yao. Kuna nchi nyingine unakuta vyama vina kitengo maalum ambacho kazi yake ni ku divert attention ya watu pale inapobidi. Na wakati mwingine kama mwanasiasa huyu amechemka mahali na attention ya watu ikawa kwenye hilo, huwa linatengenezwa tukio lingine zuri ambalo litawafanya watu wasahau alipochemka. Au kama mpinzani wake amefanya jambo zuri la kuwafanya watu wampende zaidi, yeye anatengeneza tukio either la kuchafua alichokifanya mwenzake au tukio bora zaidi la ku divert attention ya watu kutoka kwa mpinzani wake na kuileta kwake.

Na pia wanasiasa wengi hutumia sana hii trick katika kufukia makosa yao pale wanapokosea, yaani badala ya kukubali walipokosea na kuwajibika, wao hutengeneza matukio mapya mazuri ya kufukia ubaya wao. Na hii inakuwa rahisi kwao hasa pale wanapokuwa wanaongoza watu ambao wanaongozwa kwa matukio badala ya matokeo. Uongozi wa matukio ni adui wa maendeleo! by me

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanzania inaingia wap hapo na vi-wonder vp ndugu ulitaka kutujuza kuhusu TZ.

Philips X2560
 
Wapenda demkrasia hawajapasuka ,lkn wanakaribia kupasuka
Manyanyaso wanayofanyiwa wapenda demkrasia nchi vyama vya upinzani,na watetezi wa haki za binaadamu, serekali isipokuwa makini itavuna aibu,kuna tabia zimejitokeza hivi karibuni,tabia ambazo sio utamaduni wetu wa kisiasa,ni tabia za kikaburu kaburu Tabia za kikaburu kaburu zimeanza kuota mizizi,tabia za makuburu zimeanza kushamiri nchi, tabia hii ya kikaburu inashamiri kwa kasi ya ajabu sana nchini
Sherea nyingi zinazotugwa sasa hivi,ni sheria za kikaburu kaburu,anzia sheria za mitandao,sheria za kupata habari,sheria za vyama vya siasa,hizi ni sheria ambazo ni sheria za kikaburu kaburu
Ushauri wangu kwa serekali,ijitahidi kujenga demkrasia,uhuru,na utawala Bora,serekali ikijenga demkrasia,uhuru wa wananchi kupata habari,kusambaza habari,uhuru wa kukusanyika haya yakizingatiwa ,nchi yetu itapata maendeleo makubwa kiasi ambacho mataifa mengine yataishangaa tanzania kwa hatua kubwa za maendeleo na nchi nyingine zitakuja kujifunza hapa kwetu,lkn kama serekali itaendelea na tabia yake ya kukandamiza demkrasia nchini wapenda demokrasia watapasuka,w wapenda demkrasia wakipaauka nchi itapata hasara kubwa sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
b757f530d63f6ef962c475955845c52e.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Muda mwingine unaweza kuonyesha uwerevu lakini kupitia uwerevu wako ujinga wako pia ukaonekana, hivi Dkt Magufuli tangu aingie madarakani alikua anaenda na bajeti aliyoiandaa au aloandaa Kikwete? Tabia za namna hii haitusaidii sisi kama watanzania, hata kama aumpendi jitahidi kupima kwa haki, nafikiri unafuatilia bunge la bajeti na kilichomo unakiona hapo ndo tuanzie, nchi haiendeshwi wewe unavyotaka bali Rais anavyoona inafaa muda wa kupima anafanikiwa au la bado aujafika kupitia bajeti hii tutaweza kupima ni kwa kiasi gani Rais anafanikiwa lakini hii tabia ya kumkatisha tamaa Rais haifai ni tabia za watu wenye husuda na zaidi wamejaliwa wanawake kuwa nazo nchi ikiyumba sio yeye Rais atakayeteseka bali ni sisi wananchi, ni jukumu letu kukosoa pale palikosewa na kuonyesha njia sahihi ya kupita lakini kukosoa tu bila kuonyesha nini kilitakiwa kifanyike hiyo ni tabia ya kike
Taifa la kidemokrasia kama Tanzania haliendeshwi kama rais anavyoona, bali linaendeshwa kwa kufuata katiba, sheria na miongozo mbalimbali. Na sina shaka hata chembe rais wetu anafata hivyo.
Kuna marais walijaribu kuendesha nchi wanavyofikiria wao na ilileta dhahama. Mfano ni Idd Amin alidhani akiwafukuza wahindi Uganda ingekuwa tajiri zaidi matokeo yake ikafilisika kabisa. Alipoambiwa benk kuu haina fedha kabisa akaamrisha fedha zichapishwe kwa mamilioni hiyo nayo ikaleta kiama kingine cha umasikini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wana jamvi, nimejaribu kutafakari sana juu ya dhamira ya mkuu wa kaya, kwa miaka miwili aliyo kaa, mpaka sasa sijajua dira yake, dhamira yake ni kuipeleka nchi wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom