Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Kama manenoyako ni kweli tusubiri 2020 panapo majaaliwa.kwa Mimi nionavyo JPM hana mpinzani, ila kwenye mitandao blabla haziishi.
magu nimbabe atapita kibabe, ila bila kuwa wanafki magufuli hana upepo mzuri sanaaa maana ukipita katika kikund cha watu 10 basi 2 wanamfaglia 8 wanalalmika either uchumi mgumu au utawala wakimabavu. ....2020 haitomaanisha chochte ila ukweli walio wengi wanahaha sana na huu utawala
 
Tulisema hapa mwaka 2015 kuwa na vijana wengi wasio na ajira ni bomu linalosubiri kulipuka. CCM walipojipa ushindi magu akaanza kupunguza ajira badala ya kuongeza. CCM mpambane na hali mliyoitengeneza, vijana sasa wanataka mabadiliko kwa gharama yoyote bila woga.
Naona mnachukua vtu vdogo tu ilu kutoa hitimsho pa uongoz mbaya,sjui yale mazur mnayaona ama hamuyaon???? Kila kitu mathalan maswala ya uongoz kuna uimara wake na udhaifu wake katka shabaha ya maendeleo.Msiendeshwe na itikad zenu wakuu
 
96fce0bf3cbb176ca77a9274dccc4dd4.jpg
 
Naona mnachukua vtu vdogo tu ilu kutoa hitimsho pa uongoz mbaya,sjui yale mazur mnayaona ama hamuyaon???? Kila kitu mathalan maswala ya uongoz kuna uimara wake na udhaifu wake katka shabaha ya maendeleo.Msiendeshwe na itikad zenu wakuu

Mazuri yapi hayo?!
 
Kama neno baadhi limekushinda kutafasiri basi "wewe ni choo tuu kama lowassa". Dr. Slaa
Vyema,kwa nn hilo neno baadhi hukulitumia kwa naadhi ya Watanzania na badala yake ukaenda specifically jwa Wachagga...achana tabia za kuzimu ww!
 
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, "Hatuwezi kuwa na Rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli, hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya Rais au Waziri Mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.

Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.

Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu.

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je, anajua jinsi ya kututoa?! Anajua anakotupeleka?

Nimejitahidi kuangalia Bunge ili nione labda Mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.

Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!
Tangu Mei 2016, mpaka leo 2018 mkuu mi sijui anatupeleka wapi.

Anayejua rais Magufuli anatupeleka wapi watanzania aje atuambie..
 
Wasaalam, wana jamvi naomba mwenye kujua anijuze nini sera ya serikali ya wanyonge ya ccm? Maana nimetafakari ile sera ya viwanda naona ipo Kama haipo, maana huwezi kuongelea viwanda Tanzania ukaacha kuongealea taasisi Kama SIDO na VETA. Nasema hivyo kwa sababu cjaona juhudi za serikali katika kuimarisha taasisi hizo.

Kikubwa ninachoona sasa kwa serikali hii sikivu ya wanyonge ya ccm ni utawala usiozingatia Sheria na mifumo yake yaani Katiba ya jamhuri ya muungano ya mwaka 1977 Kama ilivyofanyiwa marekebisho Mara kwa mara. Serikali hii kipaumbele chake ni kupambana na chadema na kuhakikisha uhuru wa kujieleza kwa raia wake unafutiliwa mbali na yeyote mwenye mawazo tofauti na mwenyekiti wa ccm anashughulikiwa ikiwemo kupotezwa.

Wote tu mashahidi awamu hii nchi inaongozwa Kwa mawazo ya mtu mmoja, mtu huyo kaliweka bunge letu mfuko wa kulia wa koti na mahakama kaiweka mfuko wa kushoto wa koti.

Swali langu ni je hiki ndicho kipaumbele cha ccm Kwa awamu hii? Au ccm nayo imewekwa mfukoni?

Haki huinua taifa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom