Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Kweli Mkuu jamaa anachotamani si kitu kizuri,msongo wa mawazo,masumbufu ya maisha,kutokufikia malengo binafsi,kukatishwa tamaa,kushindwa kutimiza mahitaji na hali mbaya ya kisiasa(political instability) mara nyingi hutusababisha watu wengi na hasa sisi vijana kufikia hatua ya kuwaza haya. Hatufikirii wahanga wakuu Mara chache sana huwa si sisi(maana tuna nguvu, bali)
- Wanawake
- Watoto
- Wazee
Tujitahidini kuifanya dunia iwe sehemu salama,hata kama wengine hawafanyi sisi tufanye kwa nafasi yetu!!.


Sent using Jamii Forums mobile app
MANENO kuntu walahi!
Kitu kikubwa kwa vijana ni kuacha kabisa kuishi kwa mazoea!
Mimi nina machimbo ya mawe na niko na wachina, yaani ndugu yangu sikufichi, mimi mwenye mali na na contractors wa kichina tunaamka saa 11 asubuhi!
Vijana waajiriwa ni kukaa na kunywa pombe usiku mzima, asubuhi wako hoi, focus zero.
Alafu hao hao ndio wanalalamika!
Waache uvivu wa fikra na kila kitu chao kitanyooka tu!
Shida iko kwenye ku focus na responsibilities!
That’s all!
 
Hoja za msingi zimewakaukia kweli kweli. Yamebaki matamko, vitisho na maigizo yasiyomsaidia hata huyo mnyonge mnaemuimba kila kukicha. Yabidi kuvunja katiba na kutegemea Polisi na NEC ili kulazimisha "kuonekana" mnakubalika.
NDIVYO walivyofanya makaburu walokuwa na maguvu mara 1,000,000 kuliko nyie nao pamoja vibaraka wao walokuwa wanaimba mapambio na kusifu ukandamizaji wao, walitoka.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa hiyo unataka upige,eeh.
 
Mzee msoga hana shida aliyajua haya alizidiwa kete Na machinga ndo mwenye kubeba lawama zote Na madhila wayapatayo wanyonge.Msoga atalaumiwa Kwa kutokujeshimu makubaliano yao na mzee waiti ea, dhiki kuu na ukame usingekuwepo,mvua ingenyesha nyakati zote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
tu
Bila shaka hata wewe mwenyewe unaona jinsi hali ilivyo mbaya. Mtu uliyemkabidhi kijiti haukumpa uelekeo. Anaenda na mbio zake, anaelekea anakokujua yeye. Hali hii inaogofya sana. Uvumilivu umefika ukingoni. Mhe. rais mstaafu unatusaidiaje? Au tuambie tufanye nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
tulikipenda wenyewe....hakutuachia. wewe pambana na hali yako na mimi nipambane vikari naloo
 
Taifa hupata kiongozi aliye stahili yake.. We needed a mild dictator. Na hapa tuseme tumepata kiongozi tuliyemhitaji. Sasa kama ukali umezidi basi tuvumilie , lakini bila unafiki ndiye roho zetu ndiye tuiyemtaka. Binadamu kweli ni kigeugeu likiwaka jua anatamani mvua na ikinyesha mvua anataka jua. Tumshukuru Mungu Mheshimiwa amesema hataongeza hata sekude moja miaka yake 10ikipita MUNGU amlinde atimize ndoto zake. Hivi wachina wanasonga mbele sana wanayo demokrasia . Let us experience the other side of the coin. Siasa za majukwaa tuzipumzike ingawa Democracy ni jambo adimu na adhimu na inafurahisha nafsi ya MTU anayejithamini. Mimi naipenda democracy , lakini kama wengi tulipenda mkali Mimi ni nani niwe kinyume na wengi? Tutafika tu kwa uwezo wa Mungu. Amina.

Sent using Jamii Forums mobile app
Watu wanataka tija ukali hata simba anao.China hakuna achezeaye hela za umma,kule democracy ipo kuna maamuzi ya wanachama na sio maamuzi ya MTU mmoja ndo Sheria.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jitume fanya kazi acha kulalamika unataka maisha mepesi? Subiri baba yako akiwa Rais utaletewa kila kitu nyumbani. Unamuhusisha Rais Kikwete na uvivu wako wa fikra? Wenzio tunaponda kokoto na maisha yanaenda.

Sent using Jamii Forums mobile app
We endelea kuponda tu kokoto, sijui unamuuzia nani wakati maduka ya vifaa vya Ujenzi yanafungwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa ni wakati muafaka wa kujiuliza kama Mtanzania umeifanyia nini Tanzania , Sio vinginevyo ukishahoji nafsi yako ukaridhika ndipo utakapotambua umuhimu wa mchango wako kwenye nchi hii hautegemei ni nani yuko pale juu ila wewe kama wewe, umefanyia nini Nchi hii kwa uwezo wako . Vinginevyo tutabaki tu watu wa kulaumu tu miaka inaenda . Tujitambue
 
Huyu mtu tumepewa na Mungu sio Kikwete. Kwa uweza wa Mungu was Mbinguni ndoto za kuhamishia makao makuu Dodoma imetimia. ATC imefufuliwa. Reli ya kisasa ndiyo inajengwa. Mradi was umeme nchi nzima ndio hivyo umeanza. Mungu ni mkuu mno.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom