Upinzani ni kioo cha serikali jinsi inavyofanya kazi zake.
Lakini Magufuli amewaona wapinzani kama maadui wa serikali. Ameanzisha misheni ya kuteketeza upinzani , hususani CHADEMA chama chenye nguvu kubwa, hili liko wazi. Lakini asilolijua Magufuli ni kwamba hatafanikiwa kuuwa upinzani, anajipa tu moyo na kujidanganya ktk misheni yake chafu ya ukandamizaji kwa upinzani. Aangalie mfano wa Ethiopia ambako waziri mkuu wa zamani Haile Mariam alifanya kama yeye lakini leo yuko wapi; alishindwa na sasa waziri mkuu mpya ameanza kurudisha demokrasia iliyoumizwa na dikteta Mariam.
Chadema imejipanga kupambana hadi tone la mwisho la damu, auwe, afunge magerezani kama alivyodai , vyovyote vile mapambano ya kutetea haki, demokrasia, na utawala wa sheria yataendekea.
Kwa MAKAMANDA: "Never give up, when you want to give up ask yourself why you started", waache hao wachumia tumbo waende kujiunga na watesi wetu, ccm, mwisho wa siku watapata malipo yake.