Kwa kuwa hoja haina mikono, Mimi binafsi naunga mkono hoja kama ifuatavyo:
Watanzania wengi ni waelewa sana na wanaishi juu ya mstari wa kiwango cha Umaskini yaani above world poverty line
Hii nchi watu wote wamezaliwa kuanzia mwaka 2015 hivyo wanashuhudia Maendeleo makubwa ambayo hawajawahi kuyaona, Wewe Pascal si una miaka 4 tu tangu 2015,Mambo ya elimu bure, Reli ya Tazara, Mikakati ya elimu ya watu wazima wajue kusoma ni ya mwaka 2017 hapa juzi tu
Kabla ya 2015 hii nchi ilikuwa ya kusadikika, Nasikia kabla ya 2015 hakukuwa na Tanzania, Ila sasa imezaliwa upya hivyo ilikuwa fumbo tu, Tanzania ni giza tu hakuna umeme ila tunategemea bwawa la stigilers gorge ili kwa mara ya kwanza tutaona umeme, Huu unauona umeme Leo ni mazingaombwe na malue lue tu