Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Magufuli amearibiwa na CCM iliokaa kitapeli tapeli zaidi. Jamaa amekua bonge la LIJIZI la trillion zetu, na bonge la Rais muongo muongo sana LAGHAI na TAPELI. Hana tofauti na JAMBAZI.
 
Kusema kweli magufuli anaipeleka nchi pabaya anavuruga umoja anavuruga uchumi
Maisha yamekuwa magumu sana ajira hatoi kama waliopita haongezi mishahara kama waliopita
Kibaya zaidi maisha yanazidi kuwa magumu Leo imefika hatua unga wa sembe 1700 kilo moja wakati 2014 ilikuwa 700 hadi 1000 kilo moja
 
Wanaofanya mambo na kunena kwa unafiki watakupinga lakini walio wakweli wa nafsi zao, watakiri kwa uwazi kuwa uliyoyanena ni ukweli mtupu 100%.

Kuwa mzalendo wa kweli kwa Taifa, ni kutenda yale ambayo unatakiwa kutenda na Taifa, na kuyaacha mapenzi yako binafsi. Hii ndiyo sababu ya kumuapisha kiongpzi na kumtaka atamke chini ya kiapo kuwa atafuata katiba na sheria, na siyo matakwa yake.

Tujiulize - katika utendaji wake wote wa kazi, Rais wetu amekuwa anafuata na kulinda katiba, sheria na kanuni?

Rais na kiongozi mwingine yeyote, na hata sisi raia, tunayotakiwa kuyatenda, tunaelekezwa na katiba, sheria na kanuni. Unapotenda ambayo katiba, sheria na kanuni zinakuzuia, wewe kamwe huwezi kuwa mzalendo wa kweli bali unakuwa adui wa Taifa hata kama kila mahali neno uzalendo utalitamka.

Ni bahati sana kwake Rais ameongoza nyakati hizi, Taifa hili na aina ya watu kama sisi. Nchi nyingine, au hata watu wa kizazi kingine, isingewezekana. Ni kosa lisilo na msamaha kwa kiongozi kukiuka sheria na katiba kwa uwazi, tena katiba uliyoapa kuilinda, halafu ukaendelea kuwa kiongozi wa Taifa.

Kuwa kiongozi hakubadilishi ubinadamu wako, na wala hakukufanyi uwe binadamu kuwazidi wengine. Wewe ni binadamu yule yule, uliyepewa majukumu fulani kwa wakati fulani kwa kuzingatia maelekezo ya katiba. Wala kuwa kiongozi, iwe kwa kuchaguliwa au kuteuliwa, hakukuongezei akili wala ujuzi ambao haukuwa nao kabla ya kuwa kiongozi. Uwezo na akili uliyoongezewa ni uwingi wa watu wanaokuzunguka. Wewe kazi yako ni kutengeneza mazingira wezeshi ya watu wote kuweza kutumia ujuzi, uzoefu na akili zao katika kulipeleka Taifa mbele.

Kiongozi unatakiwa utende haki kwa kuzingatia katiba hata kama binafsi hupendi unayoelekezwa na katiba.
 
Kama alifuta watu kazi kws ajili ya vyeti fake iweje Bashite aka Makonda bado yupo kazini?
Nimekutajia mtu anaefahamika na wengi na ushahidi upo kwenye public domain.
Naam, kuna tukio moja lililo nisikitisha, nalo ni la aliyekuwa mtumishi mmoja wa umma. Huyu ndugu alipewa barua ya kustaafu alafu baada ya siku 2 akapewa barua ya kuachichwa kazi ktk grounds za vyeti feki. Barua ya pili ilimwambia kuwa hana haki yoyote.
 
Kama alifuta watu kazi kws ajili ya vyeti fake iweje Bashite aka Makonda bado yupo kazini?
Nimekutajia mtu anaefahamika na wengi na ushahidi upo kwenye public domain.
Toa mfano mwingine huo haueleweki, kwa kuwa wanasema nafasi yake si ya kitaaluma na mteuzi anachoangalia ni utendaji na alimkuta kwenye system akiwa DC.
 
Mleta hoja nadhani mwishoni ungetoa ushauri wa nini kifanyike badala ya kuishia kumlaumu tu, Je?
(i). Tuunde timu ya kumshauri?
(ii). Tumwache aendelee hivyo?
(iii). Je tutaweza kupata kiongozi mwadilifu sawa na Mtume au Yesu?

Tujipime, kisha tuwapime wenzetu
 
Huyo anatakiwa aachie nchi akapumzike chato. Hakuna cha maana anachofanya.
 
hakuna jungu dhidi ya Magufuli litakalowafanya wananchi wageuze msimamo
jingalao, hakuna nchi inajua propaganda kama Iran. Hakuna kiongozi mahiri kwa propaganda za kisiasa na kidini kama Ayatollah Khamenei.
Lakini hatimae watu wa Iran wametambua kuwa wanalishwa matango pori kwa kuambiwa siku zote kuwa adui yao ni US na wengine wakati ukweli ni adui yao yuko ndani na ni Ayatollah na wanaandamana wamtoe kama walivyomtoa Shah 1979.
Hayo ndio ya Tanzania ya 2020. Propaganda uchwara zimefika mwisho, Watz wameshajua nani ni kikwazo kwao.
Wamemjua asiye mzalendo, fisadi mkubwa nani, mtekaji na mpotezaji wa watu nani na kikwazo cha maisha bora na ya furaha duniani ni nani kama walivyogundua Iran
Screenshot_20200114-082736.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wengi tulimchagua Rais kwa matarajio mengi sana na angekuwa msaada kwa baadhi ya maeneo kwa jinsi mpiga kura alivyo ona Leo hii Rais anakamiribia kumaliza muhula wake wa kwanza kama wananchi kuna maeneo katuangusha kabisa mimi naanza na machache

1: Kwanza kuongeza makato ya loan board kutoka 8% ambayo watu waliingia kisheria na kuipandisha hapa ulituumiza wengi sana mpaka sasa maumivu yapo moyoni wengine wamekutwa na mikopo mingine wanakatwa na walipo ongezewa hili deni hakika wanaumia wakati tunakuchagua hatukuwaza haya maumivu yangetukuta

2: Kuto pandisha watumishi madaraja kwa wakati hapa uliumiza wengi sana kwani wengi walistahili kupanda kwa wakati lakini haikuwa hivyo wakati wanakuchagua hawakuwaza kama haya yangewakuta

3: Ongezeko la mishahara Mh Rais vuta picha wakati ule wewe ukiwa Mwl wa chemistry harafu Rais haongezi mishahara wala hapandishi madaraja wakati huo huo makato ya loan board yameongezwa Mara mbili yake ungepata maumivu ya namna gani? Haya ndiyo wanayo pitia watumishi wako wakati tunakuchagua hatuja tegemea haya maumivu.

4: Kuadimika kwa ajira hasa kwa wahitimu Wetu kwa kada zote hakika huu ni mwiba kwetu vijana wamemaliza vyuo tunao mtaani hawana ajira wakijiali hawakopesheki hakika tumebaki kuumia moyoni na vijana Wetu wakati tuna kuchagua hatuwaza hili kama itatokea ajira zitakuwa adimu hivi.

5: Uhamisho kwa watumishi sijui shida ni nini uhamisho kufungwa ama kuzuiwa kwa kipindi kirefu na huwa unazuiwa bila kuambiwa sababu za msingi hivi ni kweli Mhe, Rais mwanafunzi aruhusiwe kuhama ila Mwalimu wake asiruhusiwe kuhama? Hapana, wakati tunakuchagua hatukutegemea kama itatokea haya.

6: Mikopo ya Elimu ya juu kutolewa kwa wakati kwa wadogo zetu lakin tumeshudia juzi wadogo zetu wakisimamishwa vyuo kwa sababu walikuwa wanadai mikopo hapana Mh Rais hebu tuwasimamishe kazi walio chelewesha kupeleka mikopo badala wanao omba mikopo

Yapo maeneo mengi sana tukianza na hayo.
 
Mzee wa bleach alituambia atafuta madeni yote ya mkopo nikamchagua Mara moja kwanza kipindi kile CHADEMA ilikua kwenye fire isingewezekana kuchagua mtu mwingine!
 
Kukosolewa ni kitu CHANYA na anayekukosoa anasitahili pongezi na siyo risasi. Mkosoaji ni mtu muhimu sana katika jamii. Kwa hiyo hutaki kukosolewa ili uendelee kukosea mpaka lini au mpaka wapi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee wa bleach alituambia atafuta madeni yote ya mkopo nikamchagua Mara moja kwanza kipindi kile chadema ilikua kwenye fire isingewezekana kuchagua mtu mwingine !!!

Nilihisi somjo asee nikamchagua msema kwel mpz wa Mungu ila dah!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom