Ameandika Dotto Bulendu
Unakumbuka kupindi kile?
1.Wafanyabiashara wanauawa,jeshi la Polisi linatoa taarifa ya Kuwa walikuwa Ni majambazi,Gazeti linaingia kazini na kusema "Waliouawa siyo majambazi bali wafanyabiashara wa madini" .Hakika zamani ilikuwa raha.
2.Anatekwa Kiongozi wa madaktari nchini Na kuokotwa polisi,nchi inabaki katika sintofahamu juu ya Nani alimteka kiongozi wa madaktari?Gazeti linaingia kazini Na kuibuka Na Habari inayosema "Aliyemteka Ulimboka Huyu Hapa",Hakika zamani raha.
3.Yanachotwa Mapesa Kwenye akaunti maalum,mamlaka zinasema hizo Ni pesa za mtu binafsi,Gazeti linaingia kazini Na kuanika majina ya watu waliokwapua hizo pesa Na kusisitiza Kuwa hizo Ni pesa za Umma,Hakika zamani raha.
4.Unavikumbuka vile vichwa vya Habari vya magazeti Kama "Mapya yaibuka", Ukweli kuhusu pesa za Escrow" n.k
Sasa leo
1.Tunaambiwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Tawala nchini Tanzania (CCM) amelishwa Sumu, Sasa tunabaki kujiuliza Nani kamlisha?,Kamishna wapi?,Sumu ya aina gani? Alikuwa Na akina Nani?
Je kalishwa Na Wana CCM wenzake?kalishwa Na Nani?yaani Makamu Mwenyekiti kalishwa sumu,halafu linakuwa jambo la kawaida tu?😳😳
2.Kachero mbobezi,Mwandamizi Katika Serikali za awamu mbili,moja ya wawania Urais kupitia CCM anafurushwa ndani ya Chama ,mpaka leo hatujui hasa Membe alifanya kosa gani kubwa kiasi hicho zaidi ya kuambiwa Kuwa amekiuka maadili ya Chama.
3.Wabunge kutoka Chama Kikuu cha Upinzani nchini wanapigwa Kwa madai ya kuleta Vurugu Gerezani,Jeshi linasema walileta Vurugu mpaka wakachana Sare ya Askari Magereza,hatuoneshwi hiyo Sare Kwa Picha mnato wala video.
Hivi mnakumbuka ule Mwaka IGP Mahita alijitokeza Kwenye mkutano Na waandishi akaonesha majambia aliyodai yalikuwa ya wanachama Na mashabiki wa Chama cha CUF?
Lakini Baada ya ile ripoti Vyombo vya Habari vikakosoa taarifa ile ya IGP na kusema kuna uwalakini mkubwa juu ya ukweli wa taarifa ile.
Mambo Ni mengi sana Sasa,Ila Hakika hapo zamani mambo mengi yalikuwa safi,Kinyume Na Sasa Kinyume Na Sasa.