Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Wananchi kwa umoja wetu tunaishi na viongozi wa taifa Kama c majirani zetu ni ndugu au maswahiba!

Hebu tuwaulize hao watu kwa upole na unyenyekevu Nini ambacho tumewakosea!

Swali hili liwe la mwisho katika mioyo yetu kabla ya kuchukua hatua binafsi.

Wengi tutaenda kushtaki kwa mizimu. Ila Kuna watakao kuwa majaji wenyewe kuamua hatma Yao kwa mikono yao.

Sijataja nchi yoyote hivyo sitegemei Uzi kufutwa au kupigwa ban labda muovu mzandiki katili na dikteta awaye yote ajishtukie.

Wasalaam. .....!
15843370432411077694098.jpg

Toka asubuhi hakuna Bus iliyopita kwenda bars.
 
Wananchi kwa umoja wetu tunaishi na viongozi wa taifa Kama c majirani zetu ni ndugu au maswahiba!

Hebu tuwaulize hao watu kwa upole na unyenyekevu Nini ambacho tumewakosea!

Swali hili liwe la mwisho katika mioyo yetu kabla ya kuchukua hatua binafsi.

Wengi tutaenda kushtaki kwa mizimu. Ila Kuna watakao kuwa majaji wenyewe kuamua hatma Yao kwa mikono yao.

Sijataja nchi yoyote hivyo sitegemei Uzi kufutwa au kupigwa ban labda muovu mzandiki katili na dikteta awaye yote ajishtukie.

Wasalaam. .....!

Wananchi mvumilie tu, zoezi la kuwanyoosha linaendelea!
 
Wananchi kwa umoja wetu tunaishi na viongozi wa taifa Kama c majirani zetu ni ndugu au maswahiba!

Hebu tuwaulize hao watu kwa upole na unyenyekevu Nini ambacho tumewakosea!

Swali hili liwe la mwisho katika mioyo yetu kabla ya kuchukua hatua binafsi.

Wengi tutaenda kushtaki kwa mizimu. Ila Kuna watakao kuwa majaji wenyewe kuamua hatma Yao kwa mikono yao.

Sijataja nchi yoyote hivyo sitegemei Uzi kufutwa au kupigwa ban labda muovu mzandiki katili na dikteta awaye yote ajishtukie.

Wasalaam. .....!

Magufuli ndio anayeagiza wanacdm wateswe, kunyanyaswa na kudhihakiwa. Na sababu hasa ni kwakuwa ana chuki binafsi na nongwa dhidi ya cdm. Hivyo anatumia madaraka yake vibaya kuwafanyia ukatili. Hata kama watu wanamuonea aibu au kuogopa kumwambia, lakini yeye hasa ndio anayeaagiza ukatili huu dhidi vya cdm.
 
Tafuta kitabu kinaitwa "The dictator" au Dictator's mind" utayapata majibu.Dictator's cares nobody only himself with fully inner selfness.
 
Hakuna dikteta yeyeto duniani aliyewahi wahurumia au kuwajali maskini Zaid ya kuwatumia kama daraja.
Haijawahi tokea dictator kushughulika Na maendeleo ya watu Bali vitu
 
Ameandika Dotto Bulendu
Unakumbuka kupindi kile?
1.Wafanyabiashara wanauawa,jeshi la Polisi linatoa taarifa ya Kuwa walikuwa Ni majambazi,Gazeti linaingia kazini na kusema "Waliouawa siyo majambazi bali wafanyabiashara wa madini" .Hakika zamani ilikuwa raha.

2.Anatekwa Kiongozi wa madaktari nchini Na kuokotwa polisi,nchi inabaki katika sintofahamu juu ya Nani alimteka kiongozi wa madaktari?Gazeti linaingia kazini Na kuibuka Na Habari inayosema "Aliyemteka Ulimboka Huyu Hapa",Hakika zamani raha.

3.Yanachotwa Mapesa Kwenye akaunti maalum,mamlaka zinasema hizo Ni pesa za mtu binafsi,Gazeti linaingia kazini Na kuanika majina ya watu waliokwapua hizo pesa Na kusisitiza Kuwa hizo Ni pesa za Umma,Hakika zamani raha.

4.Unavikumbuka vile vichwa vya Habari vya magazeti Kama "Mapya yaibuka", Ukweli kuhusu pesa za Escrow" n.k

Sasa leo

1.Tunaambiwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Tawala nchini Tanzania (CCM) amelishwa Sumu, Sasa tunabaki kujiuliza Nani kamlisha?,Kamishna wapi?,Sumu ya aina gani? Alikuwa Na akina Nani?

Je kalishwa Na Wana CCM wenzake?kalishwa Na Nani?yaani Makamu Mwenyekiti kalishwa sumu,halafu linakuwa jambo la kawaida tu?😳😳

2.Kachero mbobezi,Mwandamizi Katika Serikali za awamu mbili,moja ya wawania Urais kupitia CCM anafurushwa ndani ya Chama ,mpaka leo hatujui hasa Membe alifanya kosa gani kubwa kiasi hicho zaidi ya kuambiwa Kuwa amekiuka maadili ya Chama.

3.Wabunge kutoka Chama Kikuu cha Upinzani nchini wanapigwa Kwa madai ya kuleta Vurugu Gerezani,Jeshi linasema walileta Vurugu mpaka wakachana Sare ya Askari Magereza,hatuoneshwi hiyo Sare Kwa Picha mnato wala video.

Hivi mnakumbuka ule Mwaka IGP Mahita alijitokeza Kwenye mkutano Na waandishi akaonesha majambia aliyodai yalikuwa ya wanachama Na mashabiki wa Chama cha CUF?

Lakini Baada ya ile ripoti Vyombo vya Habari vikakosoa taarifa ile ya IGP na kusema kuna uwalakini mkubwa juu ya ukweli wa taarifa ile.

Mambo Ni mengi sana Sasa,Ila Hakika hapo zamani mambo mengi yalikuwa safi,Kinyume Na Sasa Kinyume Na Sasa.
 
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, "Hatuwezi kuwa na Rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli, hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya Rais au Waziri Mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.

Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.

Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu.

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je, anajua jinsi ya kututoa?! Anajua anakotupeleka?

Nimejitahidi kuangalia Bunge ili nione labda Mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.

Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!
dereva lori kaweka gia namba nne, abiria tunapiga kelele yeye anasema mpka 2025
 
Ameandika Dotto Bulendu
Unakumbuka kupindi kile?
1.Wafanyabiashara wanauawa,jeshi la Polisi linatoa taarifa ya Kuwa walikuwa Ni majambazi,Gazeti linaingia kazini na kusema "Waliouawa siyo majambazi bali wafanyabiashara wa madini" .Hakika zamani ilikuwa raha.

2.Anatekwa Kiongozi wa madaktari nchini Na kuokotwa polisi,nchi inabaki katika sintofahamu juu ya Nani alimteka kiongozi wa madaktari?Gazeti linaingia kazini Na kuibuka Na Habari inayosema "Aliyemteka Ulimboka Huyu Hapa",Hakika zamani raha.

3.Yanachotwa Mapesa Kwenye akaunti maalum,mamlaka zinasema hizo Ni pesa za mtu binafsi,Gazeti linaingia kazini Na kuanika majina ya watu waliokwapua hizo pesa Na kusisitiza Kuwa hizo Ni pesa za Umma,Hakika zamani raha.

4.Unavikumbuka vile vichwa vya Habari vya magazeti Kama "Mapya yaibuka", Ukweli kuhusu pesa za Escrow" n.k

Sasa leo

1.Tunaambiwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Tawala nchini Tanzania (CCM) amelishwa Sumu, Sasa tunabaki kujiuliza Nani kamlisha?,Kamishna wapi?,Sumu ya aina gani? Alikuwa Na akina Nani?

Je kalishwa Na Wana CCM wenzake?kalishwa Na Nani?yaani Makamu Mwenyekiti kalishwa sumu,halafu linakuwa jambo la kawaida tu?😳😳

2.Kachero mbobezi,Mwandamizi Katika Serikali za awamu mbili,moja ya wawania Urais kupitia CCM anafurushwa ndani ya Chama ,mpaka leo hatujui hasa Membe alifanya kosa gani kubwa kiasi hicho zaidi ya kuambiwa Kuwa amekiuka maadili ya Chama.

3.Wabunge kutoka Chama Kikuu cha Upinzani nchini wanapigwa Kwa madai ya kuleta Vurugu Gerezani,Jeshi linasema walileta Vurugu mpaka wakachana Sare ya Askari Magereza,hatuoneshwi hiyo Sare Kwa Picha mnato wala video.

Hivi mnakumbuka ule Mwaka IGP Mahita alijitokeza Kwenye mkutano Na waandishi akaonesha majambia aliyodai yalikuwa ya wanachama Na mashabiki wa Chama cha CUF?

Lakini Baada ya ile ripoti Vyombo vya Habari vikakosoa taarifa ile ya IGP na kusema kuna uwalakini mkubwa juu ya ukweli wa taarifa ile.

Mambo Ni mengi sana Sasa,Ila Hakika hapo zamani mambo mengi yalikuwa safi,Kinyume Na Sasa Kinyume Na Sasa.
Mambo mengi uda mchache.
Mangua kalishwa sumu na watu wa kamati kuu alafu polisi wanasea hata kama ni mtu wa upinzani.
Hakuna mwandishi anasdhubutu kuhoji,
Kila habari kwa sasa ni "nampongeza mheshi,iwa raisi"

Mtu kakimbilia dodoma kukwepa corona , ila mgonjwa wa corona anampongeza, tena alipangiwa maneno ya kuongea ile asubuhina Usalama wa Taifa
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom