Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Kweli ni heri kuwa mjinga, kuliko mpumbavu. Wewe unamsifia huyo muuaji kwa lipi? Uwizi wa T 2.4, kufanya serikali, bunge na mahakama viko chini yake au? Acheni kusifia huku mkijua ni uongo, hukumu yenu ni kifo.
Wanaomsifia Magufuli ni wanafiki sana, mtu anayejimwambafy na kujiona yeye ni Bora kuliko wengine, mtu asiyeheshimu mihimili mingine, mtu anayejiona yeye ndiye mzalendo zaidi ya wengine, mtesaji na muuaji, unaanzaje kumsifia mtu huyu.

Najua #UVCCM na wazee wao hawawezi kumkemea Magufuli maana hawa watu wananjaa na familia zao zinamtegemea mtesaji huyu, kwahiyo kitu pekee ambacho ningependa hawa watu wa CCM kutusaidia sie wananchi wengi ni kukaa kimya wakati tunashughulika naye!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanaomsifia Magufuli ni wanafiki sana, mtu anayejimwambafy na kujiona yeye ni Bora kuliko wengine, mtu asiyeheshimu mihimili mingine, mtu anayejiona yeye ndiye mzalendo zaidi ya wengine, mtesaji na muuaji, unaanzaje kumsifia mtu huyu.

Najua #UVCCM na wazee wao hawawezi kumkemea Magufuli maana hawa watu wananjaa na familia zao zinamtegemea mtesaji huyu, kwahiyo kitu pekee ambacho ningependa hawa watu wa CCM kutusaidia sie wananchi wengi ni kukaa kimya wakati tunashughulika naye!

Sent using Jamii Forums mobile app
Una point sana na kipaji,MATAGA aka CCM-MPYA ambao pia ndio UVCCM-POLICE wao wanasifia tu , hata wakijambiwa mdomoni wanasifia tu.
Just imagine huyu kiongozi waziri mkuu anamuogopa makonda na anazunguka kwenye hotuba yake ya kibaha anasema wapuuzeni watakaowapa taarifa za korona kama siyo ummy, magufuli, Majaliwa, ila hasemi nani apuuzwe na mwenye kutoa taarifa ni BASHITE tena akasema ana mamlaka hayo maana ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama,alafu JIWE anaangalia tu hamgusi, zero brain.
 
Kweli Mungu kaumba watu na nungu nungu, wakati watu tuko busy na maendeleo wengine wanawaza kuchezea pesa kwenye Katiba ambayo JK alihangaika nayo akiwalipa shilingi 300'000, Kwa siku na bado walichukua posho na kukimbia wakiachilia mbali Katiba[emoji3526] sasa mnakuja kwa mlango wa nyuma yaani tuache hii miradi mikubwa pesa tupeleke kwenye posho za Katiba?
Endeleeni kubwata kwa kweli hatuwezi kuwasikiza labda baada ya miaka mingine ijayo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanaomsifia Magufuli ni wanafiki sana, mtu anayejimwambafy na kujiona yeye ni Bora kuliko wengine, mtu asiyeheshimu mihimili mingine, mtu anayejiona yeye ndiye mzalendo zaidi ya wengine, mtesaji na muuaji, unaanzaje kumsifia mtu huyu.

Najua #UVCCM na wazee wao hawawezi kumkemea Magufuli maana hawa watu wananjaa na familia zao zinamtegemea mtesaji huyu, kwahiyo kitu pekee ambacho ningependa hawa watu wa CCM kutusaidia sie wananchi wengi ni kukaa kimya wakati tunashughulika naye!

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna mwingine naye anaona wanaompinga Magufuli ndiyo wanafiki hasa ukizingatia wengi wao hushambulia zaidi haiba (personality) yake badala ya kujikita kwenye wajibu wa serikali yake vs vile inavyofanya.

Pia wanaonekana wanafiki wasiomaanisha wanachohubiri kwani wao hupinga au kutukana yeyote mwenye maoni tofauti ilhali wanajitambulisha kama waumini wakubwa wa demokrasia. Yaani unajiita mwanademokrasia halafu mtu mwenye maoni tofauti unamwona adui asiyefaa. Sasa hiyo ni demokrasia au domoghasia?

Mimi nadhani kila mtu awe huru kutoa maoni yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
April 11, 2020

ZITTO KABWE AICHAMBUA RIPOTI YA CAG 2018/19
Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Mh. Zitto Kabwe (Mbunge Kigoma Mjini), akichambua ripoti ya CAG kwa mwaka 2018-19 na Ripoti za CAG kwa miaka 5 ya serikali ya awamu ya tano .
Hivyo uchambuzi huo unalenga ktk maeneo makubwa kumi muhimu :



Source: Mwanahalisi TV
  1. Kuporomoka kwa makusanyo ya kodi : hivyo serikali kushindwa kukidhi mahitaji ya bajeti na hivyo bajeti kukosa maana inayo kusudiwa ya uwiano wa makusanyo dhidi ya matumizi pia ufanisi wa kukusanya kodi.
  2. Deni la Taifa ktk awamu ya tano ya serikali ya CCM linakuwa kwa kasi kubwa yaani asilimia 12% kuliko kasi ya ukuaji wa uchumi wa nchi ulio ktk wastani wa asilimia. Serikali imeanza kushindwa kulipa madeni ya ndani mfano kulipia Hati Fungani yaani Government Bonds jambo lililo hatari maana yake wananchi na wanunuzi wengine wa hati fungani kukosa imani ya serikali kuweza kulipwa amana zao. Serikali inadaiwa kiwango kikubwa na watoa huduma ikiwemo wakandarasi, makampuni na watu binafsi. Wakala wa Barabara yaani TANROADS ni mdaiwa sugu mwenye deni kubwa yaani Bilioni 900. Serikali pia inaficha kipande cha madeni ya Hifadhi za Jamii yanayofikia trilioni 3 shilingi za kiTanzania na wastaafu kuwa ktk hatihati ya kushindwa kulipwa malipo yao.
  3. Ufisadi umerudi nchini kupitia transit goods kwenda nchi jirani umeongezeka sana kufuatana na taarifa ya CAG. Kiasi cha bilioni 300 ni kimepotea ktk awamu ya 5 huku awamu ya Jakaya Kikwete upotevu ulikuwa bilioni 45 tu.
  4. Kesi dhidi ya serikali yaani contingent liability kimefikia trilioni 1.8 za shilingi za kiTanzania kutokana na kutotii mikataba na wadai kukosa imani ya kulipwa.
  5. Manunuzi yasiyofuata sheria yafikia Shilingi Trilioni moja kwa unapproved suppliers.
  6. Serikali inaendelea kutumia fedha za umma bila kufuata katiba ibara ya 135 yaani kupitia mfuko Mkuu wa serikali yaani Consolidated fund bila idhini ya Controller and Auditor General.
  7. Ukaguzi wa Benki Kuu ya Tanzania umefanywa na GAG bila kutumia kampuni za Ukaguzi za binafsi Deloitte, KPMG n.k hivyo kukosa uwazi na uhuru wa kufanya ukaguzi huru unaoaminiwa na IMF, WORLD BANK na wabia wengine.
  8. Korosho zanunuliwa na fedha kutoka Benki Kuu na fedha hizi hazijarejeshwa Benki Kuu
  9. Ndege kununuliwa bila taratibu za kifedha zilizo wazi.
 
April 9, 2020

RIPOTI YA CAG YAWASILISHWA KWA WANANCHI KWA AJILI YA MJADALA MPANA

SERIKALI YAKUSANYA MAPATO KUTOKA SERIKALI ZA MITAA NA KUZITUMIA BILA KUZIPITISHA KWENYE MFUKO MKUU



Source : Chadema Media

https://chadema.or.tz › 2018/03/01
SERIKALI YETU NA UVUNJWAJI WA KATIBA YA NCHI - Chadema

1 Mar 2018 · Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 135(2) inaeleza kwamba , nanukuu “Fedha ambazo hazitawekwa Mfuko Mkuu wa Serikali Consolidated Fund.....
 
Huyu jamaa Bure kabisa!
Kabla ya UCHAGUZI 2015 tulimuongelea huyu mtu nyumbani nyumbani nakumbuka tulikuwa tunakula chakula Cha usiku . conclusion.hafai kuwa raisi .anafaa kuwa chini ya mtu , aambiwe hiki fanya hiki acha.hafai kuwa mtu wa kutoa maamuzi ya mwisho
 
Nimekuwa nikifuatilia mambo kadha wa kadha ambayo yanajitokeza katika taifa, nimeona tuna Rais anayetumia muda mrefu sana kufanya maamuzi makubwa na ya maana.
Kwa mfano hili janga la Covid-19 tangu limeanza hadi sasa hakuna hatua za msingi zilizochukuliwa kudhibiti maambukizi ya kuenea kwake.
Watu mbalimbali wamekuwa wakitoa mapendekezo mbalimbali kuhusu kulikabili jambo hili kama vile kufunga mipaka, kuifunga (lock down) Dar es salaam kwa muda, Benki kuu kuuhami uchumi, kusambaza vifaa vya kupima ugonjwa nchi nzima, n.k.
Yeye anawaza kukusanya kodi tu ndio maana hata tamko la mkuu wa mkoa wa Mbeya la kufunga baa mapema amelifutilia mbali. Hadi sasa amepumzika tu anasubiri hadi mambo yaharibike ndio achukue hatua.
Jambo pekee analoweza kulifanya kwa haraka ni KUFUKUZA WATU KAZI isipokuwa Makonda pekee.
Mlio karibu naye hata kama mnamwogopa kwenye hili pigeni moyo konde mumwambie.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wastaafu nao kimya!!

Mitandao tu ndio kwa sasa inasaidia kukosoa na kushauri vinginevyo hata baadhi ya hatua zinazochukuliwa huenda zisingekuwepo pasipo kelele za watu mitandaoni.

Bunge kwa sasa nalo msaada wake ni mdogo sana katika kuishauri na kuisimamia serikali.
 
Ngoja birika lichemke kwanza octobar tutakaposema hakuna uchaguzi Hadi 2025 muelewe
 
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, "Hatuwezi kuwa na Rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli, hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya Rais au Waziri Mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.

Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.

Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu.

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je, anajua jinsi ya kututoa?! Anajua anakotupeleka?

Nimejitahidi kuangalia Bunge ili nione labda Mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.

Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!
Hii ni hoja ya mwaka 2016, mpaka leo inaishi.
Wenye akili na hekima wasome na kuelewa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom