Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Naona hiyo mimba inakusumbua njoo basi tukusaidie kuilea mimba yako usije ukafa na stress kwa kuhangaika na marehemu ambaye amelala na hawezi kujitetea ila tupo sisi kwa ajili ya kumtetea kwa kuonyesha mazuri aliyoiachia nchi yetu.
Hii mimba iliharibika tarehe Fulani March 2021
 
Tuachane na CCM.
 
Huo ndiwo ukweli.

Rais Samia ni laini mno lijapo suala la usimamizi wa jambo na kwake yeye huamini kusikia/kusimuliwa zaidi kuliko kufika mwenyewe ili kujionea.

Hulka ya Viongozi wengi ni wezi na mafisadi na kwayo hata mianya ya kuharibu kwa makusudi jambo lolote zuri ili tu wajinufaishe wao kwao si kazi kubwa.

Samia ni Rais wa kusimuliwa na hapo ndipo mwanya wa mafisadi kuiba na kuharibu kwa ajili ya maslahi yao huwa.

Mfano mzuri ni hayo matengenezo ya injini za Airbus zetu ukweli ni kwamba hayupo hata mtu anayefuatilia kwa maana ya mkazo na sababu ni moja tu wenye maslahi yao wameweka mkono wao ili mwisho wa siku Shirika life na wao waendelee kunufaika na miradi yao kama hapo awali.

Aminini nawaambia, Tanesco, ATCL na Mashirika yote ya UMMA yaliyoanza japo kujikongoja yatakufa yote ndani ya Utawala huu!

NB: Hata kule kwao mwanamke kwake ndani.
 
Na kwa kuzingatia kwamba vigogo wa Ufisadi Tanzania ndio wameingia kuwekeza kwenye Civil Aviation Industry.......

ATCL litahujumiwa mpaka Dakika ya kukata Roho!

Hao wakurugenzi wake wataendelea kufurahia Posho nono za Kusafiri kwenda kuiangalia Ndege pale ilipopaki.

Mwisho wa Mwaka....Mkaguzi wetu Kichere atakuja na ngonjera za kuilaumu serikali ya awamu ya Tano.

Kisha anaikabidhi ripoti ikafungiwe kabatini.
 
Yaani kwa huu mgao wa umeme...JPM kuwaumbua basi ndio kisasi tunakilamba sisi kisawa sawa...hakuna rangi tutaachaona...

Hv tumekosa viongozi majasiri wakututetea kwa hili....tunamwachia Marope ana run the show km vile nchi ya baba yake hii...mara ukame?! Sasa hv sababu imebadilika ni matengenezo mitambo imechakaa...

Mitambo imechakaa pindi marope kushika wizara tu?! Watanzania tu Wapole sana kwa kweli
 
Kazi ya Rais si kutembelea kila Shirika la umma ili kujua utendaji wake. Nchi ya Tanzania ni kubwa mno hawezi kufika kila mahali ili ajue utendaji wa kazi. URais ni tasisi- ina watu wengi wanao msaidie Rais ili atimize majukumu yake ipasavyo Kama atatembelea kila sehemu- kuna majukumu mengine yatalala. Rais anatakiwa achague timu nzuri , watu ambao si ndugu zake wa damu, watu wa dini na makabila mbali mbali. Hakuna tatizo kwa Rais kusikiliza ushauri, hakuna binadamu anayejua kila kitu. Rais ameajiliwa na wapiga kura wake.
 
Sidhani kama ulifikiria mara mbili kabla hujatuma ujumbe huu.
Mbona una hatarisha maisha yako?

Hivi kwenu hakuna watu wazima kama huyu mama uliyemtusi hapa?
Hawaheshimiwi hao watu wazima achilia mbali wadhifa wa uraisi wa huyu mama?
Mambo mengine kujitakia matatizo ila kama upo nje ya nchi unaweza kusalimika.
 
Nimeshamaliza kulingana na urefu wa kamba yangu, nihamishie sehemu nyingine ila uongeze urefu wa kamba.
 
inawezekana anaogopa kutia mguu tanesco kuna mirija minene ya wazito wenzake asije akawaudhi
 
Awamu ya JK imerejea kivingine...serikali ya hovyo na dhaifu sana kwakweli.
 
Kwani kuna nini zaidi tunaweza kufanya zaidi ya kuandika ??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…