Nikiuliza nipewe sababu mhimu ya Kwa nini bei ya bidhaa imepanda Kwa kiasi kikubwa hiko hakuna sababu ya maana!
Hiyo ni moja ya dalili za kushindwa! Kwa nini mgao wa umeme, sababu hazijitosherezi, Kwa nini kipindi cha nyuma gharama ya kuingiziwa umemw ilikuwa 27000, na sasa 300000+ hakuna sababu ya msingi!
Kwa nini tumeongeza tozo lakini zimefanya nini, labda kuna jambo jipya ambalo halikuwa likifanywa kipindi cha nyuma tozo imefanya, napo hakuna!
Hizo ndizo dalili za kishindwa!
Na sababu Moja wapo ya yeye kushindwa, amekaa kirafiki sana hata mahali pasipostahili kukaa kipendwa kama Amiri Jeshi mkuu wa Tanzania
Urafiki katika kazi sio mmbaya, ila wateule wanapoharibu na kumharibia, urafiki wa nini hapo?
Kwa nini kuwa na urafiki na mtu anayeharibu kazi yake?
Mawaziri kibao wapo wapo tu hapo kumharibia Rais, Kwa nini urafiki nao.?
Badala yake sasa tunaanza kuungana nao kuombea kila kitu kisifanikiwe chini yake Kwa sababu yeye Mh anataka hivyo,
Kwani watu wazuri, wazalendo, wachapakazi na wasomi wameisha kwenye Taifa hili ili hali kila kitu kinaenda ndivyo sivyo?