Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi,
Baada ya Rais Samia kuruhusu mikutano ya siasa, sasa ni nderemo na vifijo nchi mzima!. Na mimi kama Mtanzania mzalendo wa taifa letu, pale linapofanywa jambo jema lolote la kheri kwa mustakabali mwema kwa taifa letu, sina budi kujiunga na wengine wote wanaolitakia mema taifa hili kwa kumpongeza Rais wetu, Mama Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu mikutano ya siasa, kukubali kurekebisha sheria mbalimbali kandamizi na kubwa kuliko, kukubali kuendeleza mchakato wa katiba mpya.
Kwenye hili la kuzuiwa mikutano ya hadhara, kwa vyàma vya siasa
, kwa vile mikutano hiyo ya vyama vya siasa ni kitu ambacho kimeruhusiwa na katiba, kitendo kile cha kuzuia mikutano hii, hakikuwa sawa!, huu ilikuwa ni ukwiukwaji wa wazi kabisa wa katiba ya JMT mchana kweupe!.
Kufanya mikutano ni miongoni mwa haki za vyama vya siasa zilizoainishwa na katiba, hata lile swali langu la Ikulu, kumuuliza rais wa JMT, ametumia mamlaka gani kwenye kifungu kipi cha sheria, kuzuia jàmbo lililoruhusiwa na katiba?, naamini wengi mnajua nilijibiwa nini!.
Sasa leo Rais Samia, alichokifanya kwa kuruhusu mikutano ya siasa, ni kama leo ndio lile swali liameljibiwa kwa mtindo ule ule wa "anayekuja pasi na hodi, huondoka pasi kuaga!", jambo linalozuiliwa kwa utashi tuu wa mtu bila kifungu chochote, cha katiba au sheria, siku ya kuliruhusu jambo hilo, pia ni kwa utashi tuu, wa kiongozi aliyepo, bila kutumia kifungu chochote au sheria yoyote!. Jambo lolote lililozuiliwa, (regardless lilizuiwaje), linaporuhusiwa, hatua ya kwanza ni kushukuru kwa jambo hilo kurusiwa, hivyo Watanzania wote tujiunge pamoja na kusema kwa kauli moja, "Asante Sana Mama".
Baada ya kushukuru, sasa twende ndani kidogo zaidi ya jambo lenyewe lililoruhusiwa, kwa vile mikutano ya siasa ilizuiliwa kwa utashi tuu, na sasa imeruhusiwa kwa utashi tena, tukishukuru na kusema tuu asante bila kutia neno jingine lolote, hii inapelekea suala la mikutano ya siasa kuonekana ni kama jambo la hisani tuu ya rais aliyepo madarakani, JPM alizuia mikutano kwa utashi tuu, na leo Rais Samia ameruhusu mikutano hii kwa utashi na kwa hisani tuu!, swali linabaki ni jee mikutano ya vyama vya siasa ni haki ya vyama kufanya mikutano au ni hisani ya Rais wa JMT aĺlye madarakani?
Kitu kama ni haki, then haki ni stahili sio hisani!, Je sisi Watanzania tutaendelèa kusubiri hadi lini wakati haki zetu na stahili zetu zikigeuzwa kuwa hisani?.
Tena afadhali ya hili la haki ya mikutano ya siasa, limefanywa kwa utashi tuu kwa kutumia kauli tuu, yaani mikutano ilizuiliwa kwa kauli, na sasa imeruhusiwa kwa kauli, lakini kuna na haki nyingine mbili ambazo ndizo haki kuu za kiraia zilizotolewa na katiba yetu, haki za kuchagua na kuchaguliwa, nazo zimegeuzwa hisani!. Haki ya kuchagua yenyewe bado ipo, ila haki ya kuchaguliwa, haipo!, imenyofolewa na kufinyangwa finyangwa hivyo kuonekana kama ipo ila kiukweli ni haipo na mimi mwenyewe ni shahidi wa hili!.
Kwenye issues za haki zetu za msingi za kikatiba, jee Watanzania tutaendelea kusubiri kuhisaniwa mpaka lini?.
Naendelea kusistiza mwaka huu wa 2023, Watanzania lazima tuamke tufanye kitu.
Watanzania tuendelee kuwa watu wa shukrani kwa kushukuru kwa yote, hata kama ni madogo ili tuweze kupatiwa makubwa, hivyo tuendelee kusema
asante sana Mama Samia kwa a good political will la kuruhusu mikutano ya siasa, kwa utashi tuu hivyo vyama na Watanzania kukushukuru kwa hisani yako hii, tunakuomba tumia a political will kama hii hii kuwaruhusu Watanzania wote kuchagua na kuchaguliwa!.
Wakati tukisubiria hisani ya Mama Samia kwenye hili, kupitia marekebisho ya sheria mbalimbali na kumruhusu kila Mtanzania kuchagua na kuchaguliwa, should we just sit and wait kusubiria hisani ya Mama kama vyama vya siasa vilivyosubiri hadi leo vilipohisaniwa, or should we do something?. Hiki ndicho nilicho anza nacho mwaka huu Watanzania ni maneno maneno na kulialia, Vitendo 0. Katiba ni maneno tu! Je, 2023 tuendeleze maneno matupu na kulialia au tubadilike tufanye kitu?
Haki ni stahiki sio hisani!, haki haiombwi na kutegemea hisani, wala haki haihitaji vikao, mikutano na majadiliano kuzijadili haki, na haki hauletewi kwenye kisahani cha chai kama hisani, fadhila au zawadi, haki ni stahiki inayopaswa kutolewa unconditional not as a favour, hisani au fadhila!. Haki is a right, inayopaswa kutolewa unconditional na isipotolewa, haiombwi, bali hudaiwa, na katika kuidai huku kukishindikana kuidai kwa amani na kisheria, ndipo nguvu hutumika kuipigania, but only pale inapobidi, na ni katika kuipigania huku sometimes machozi, jasho na damu huweza kumwagika!.
Kwa vile Rais wetu Mama Samia, keshaonyesha utashi, kwa kauli na matendo, tuzidi kumuombea ili Mungu amuwezeshe ayaweze yote haya kabla hajamaliza awamu yake hii ya kwanza, ili hata ikitokea akaendelea kwa awamu ya pili, then hiyo itakuwa ni awamu ya shukrani na kumpa asante kwa aliyotatenda, na sio awamu ya kukamilisha ambayo hayakumamilika.
Mungu Mbariki Rais Samia
Mungu Ibariki Tanzania
Happy New Year.
Paskali