Anayekuja pasi na hodi, huondoka pasi kuaga. Kuzuiwa bila kifungu, kuruhusu bila Kifungu. Ni hisani ya Rais Samia. Haki kuhisaniwa hadi lini?

Wabongo wengi wamelala usingizi wa pono kwenye masuala ya siasa, sayansi, na uchumi.

Ndiyo maana watawala wanawaviringa na kuwafanya chochote wanachotaka.
 
Bila Katiba Mpya, mambo mengi nchi hii tumekuwa tukifanyiwa kwa hisani tu, na kama hatujui kupigania haki zetu, basi ni vyema tukashukuru kwa hisani tunazopewa na watawala, kinyume na hapo ni kukosa shukrani tu, kwasababu hata wakitunyima hatuwezi kuwafanya chochote zaidi ya kulia lia mitandaoni, na kutoa pole mitandaoni kwa wale wanaoumizwa wakipigania haki zetu.
 
Hizo ni neema za mwaka mpya na funzo la kutoigeuza haki kuwa hisani tena.
 
Mimi sijaelewa wameridhiana kuendesha mikutano ya kisiasa? kwanini wasinge maliza mambo yote ndiyo wake kwenye Camera.Maana ishu nyeti ni katiba na tume ya uchaguzi!sasa mambo ya kutueleza mipasho kuwa sheria zipo kwenye pipeline inasaidia nini!!
CCM hawapo tayari kwa maridhiano,Mama angekaa kimya tu,lile kokololo haliwezi.
 
ALIYEIZUIA ALIVUNJA KATIBA MAMA KARUHUSU ILI KATIBA IHESHIMIWE WALA SIO HISANI
Ilipovunjwa alikuwepo wapi au ughaibuni?

Aliyemkamata Mbowe na kumuachia ni huyo huyo aliyemruhusu kufanya mikutano bila kutueleza behind the scene.

Ukweli wa haya yote anajua Mbowe na mama said ila wanatuletea michezo ya kaole...

Mbowe kuwa kimya na kuweka mikono nyuma kuomba mikutano ambayo ni haki yake kikatiba sio bure, kuna kitu wanatuficha...

Ngoja tuone Mbowe atakuwa kama Kabwe wa ACT,tusubirie muda ndio kila kitu, amekuwa compromised.
 
Tanzania imeshachoka kufanya siasa kilichopo ni maigizo na ushenzi tu.

Vyama vya siasa havipo tena yaliyopo ni magenge ya wahuni tu.
 
Utapewa kesi kama Mbowe....nenda taratibu.
 
Mkuu Paskali
Kisheria, haikuwa sahihi kuzuia shughuli za kisiasa awamu ile na ilipaswa kabla ya kuruhusu ziendelee rais alipaswa kuweka bayana kuwa katiba na sheria ndiyo mwongozo wa shughuli zote za serikali.

Najua watawala wetu hawawezi kuomba radhi kwa makosa ya makusudi wanayoyafanya lakini kuliweka bayana kuwa katiba na sheria ni mwongozo sahihi na tunapaswa kujikumbusha wakati wote ktk hilo.

Amefanya vyema yes lakini vyema from where? Was it legitimacy decision to ban political activities in Tanzania? Sheria ipi ilitumika na Katiba imeruhusu wapi maamuzi hayo?
 
Mkuu Paskali
Kisheria, haikuwa sahihi kuzuia shughuli za kisiasa
Mkuu Msanii , hii ni kweli, haikuwa sahihi kuzuia mikutano ya siasa, ila pia it's very unfortunately hatuna any serious opposition inayojua wajibu wake!.

Baada ya mikutano kuzuiliwa ukawa wakapanga maandamano nchi nzima, nikamshauri Lissu Hoja ya Udikteta wa Magufuli: Tundu Lissu isn't Right. Haupingwi kwa kupaza sauti kupiga tu Kelele!

Kuna siku nilikutana na Zitto nikamuuliza

View: https://youtu.be/A_YPEHtM9WM?si=d1GNsfSaX6LaWDox
awamu ile na ilipaswa kabla ya kuruhusu ziendelee rais alipaswa kuweka bayana kuwa katiba na sheria ndiyo mwongozo wa shughuli zote za serikali.
Naunga mkono hoja
Najua watawala wetu hawawezi kuomba radhi kwa makosa ya makusudi wanayoyafanya lakini kuliweka bayana kuwa katiba na sheria ni mwongozo sahihi na tunapaswa kujikumbusha wakati wote ktk hilo.
Naunga mkono hoja
Amefanya vyema yes lakini vyema from where? Was it legitimacy decision to ban political activities in Tanzania? Sheria ipi ilitumika na Katiba imeruhusu wapi maamuzi hayo?
Hili ndio hoja kuu ya bandiko hili, Watanzania tutaendelea kunyamaza hadi lini wakati haki zetu zikigeuzwa ni hisani?.

Uchaguzi Huru na wa haki ni haki sio hisani!.
Kuchagua viongozi unaowataka ni haki sii hisani!.

Ili wananchi wawachague viongozi wanaowataka lazima haki ya kugombea uongozi iwepo, ili mtu kugombea uongozi, haki hii ya kugombea imehisaniwa kwenye chawa cha siasa!.
P
 
Naona majibu unayoyaandika yananisogeza kuwa mwanasheria ama mwanasiasa wa msimamo fulani.

Anyways. Ndo narejea kutoka event ya kutoa zawadi kwa washindi wa Strories of Change.

Nitarudi kujenga hoja hapa
 

Hii ni zawadi yangu kwa Birthday ya Mama leo, nilipanga kumpa wiki ya mwisho ya October 2025,

Ili zawadi hii iwe na manufaa kwake, nikisubiri mpaka hiyo 2025, it might be a bit too little too late, kuna ubaya hiyo zawadi, kutolewa mapema mwaka huu ili iweze kutumika mwaka kesho?.

Zawadi yenyewe ni Salaam tuu za Birthday zenye ki parcel fulani!

HBD Mhe. Rais Samia kwa kutimiza miaka 64!, nakupongeza sana na kukuombea afya njema!.

Mwakani 2025 utakuwa unatimiza umri wa miaka 65 na 2030 utakuwa na umri wa miaka 70, hivyo zawadi yangu ya pekee kwako ni HII na kukusisitizia, sio lazima kuizingatia saana kivile, ila ni muhimu kuisikiliza na kujisikilizia kama na wewe pia uliambiwa kama nilivyoambiwa mimi, kwasababu yule YEYE, sometimes ana tabia na mtindo wa kuwaambia watu wake, kupitia kwa watu wengine!, hivyo just listen and try to make sense of this, a think about it, if makes any sense to you, ikitokea it doesn't make any sense to you, then dismiss it as just another set of crap!.

Ila ikitokea na wewe pia uliambiwa, but you are not very sure kama ni YEYE au ni yeye, then don't take a chance!, usipuuze!, maana hicho kitu chenyewe, is nothing compared!.

If this being the case, then tunakuomba sana sana sana, ututekelezee haya mambo tunayokulilia nayo tangu umeingia kwenye usukani, tekeleza tuu yale yaliyomo ndani ya uwezo wako, maana kusubiria post 2025, it might be too little too late!. Please Mama!.

Na ikitokea wewe hujaambiwa mpaka 2025 inaingia na hujawahi kuambiwa na mtu mwingine yeyote, then ipuuze HII itakuwa sio sauti yake YEYE bali itakuwa ni sauti ya yeye tuu ambaye sio YEYE!.

Hivyo endelea na ule mpango wako wa 2025!, na Watanzania wanaolitakia mema taifa letu hili, wote tutakuwa Tuko nyuma yako,
Tuko pamoja nawe,
Tuko nawe!.

Mungu Akubariki Sana!.
HBD Mamaa!.
Paskali
 
Tanzania tunapaswa kufanya mambo yetu kwa taratibu za kikatiba, sio utashi wa mtu mmoja mmoja hata kama mtu huyo ndio Raisi wa nchi, au waziri,au IGP au Katibu mwenyezi wa CCM nk. Namna hiyo ya uongozi haitatufikisha popote.
Mkuu @Sythesizer, naunga mkono hoja. Siku mikutano ya siasa na maadamano yaliporuhusiwa nilisema mikutano ya vyama na maandamano ni haki na sio hisani!, haki ni kitu stahiki na sio hisani!, karibu mitaa hii
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…