How comes unasema nchi inaongozwa na mifumo halafu unamlaumu Nyerere!
Umejielewa kweli?!
Au kwako Nyerere ndie alikuwa mfumo wenyewe?!
Ujuaji ukizidi ni tatizo.
Yule ambaye hakuwahi kuwa na kashfa ya ufisadi ndie chanzo cha umaskini wetu!.yule mzee ndiye chanzo cha umasikini Tanzania katikati ya utajiri mwingi. Ndiye mhusika mkuu wa kuiua Tanganyika yetu. Alikuwa mshirikina kupindukia,
Acheni hizi ngonjera zenu.Nyerere ndiye aliyesuka Mifumo
1. Mifumo ya kisheria na taratibu. Kupitia Katiba na Sera za nchi
2. Mifumo ya kimawazo na kifikra.
Ukisikia zidumu fikra za mwenyekiti. Na mila nyingi za ccm na nchi hii basi muasisi wake ni Nyerere
Ingawaje yapo mazuri aliyoyafanya lakini mabaya yapo.
Yule ambaye hakuwahi kuwa na kashfa ya ufisadi ndie chanzo cha umaskini wetu!.
Kosa lake kuyaacha madini ardhini kisha nyie mkaja kuyachezea, halafu mnarudi kumlaumu yeye!
Huu ujinga wenu ni next level.
Acheni hizi ngonjera zenu.
Nyerere licha ya Urais wake, nae alikuwa mwanadamu kama mimi na wewe.
Ni ujinga kumlaumu Nyerere leo kwa mnachodai makosa yake, ikiwa hata sisi tunaweza kuyarekebisha.
Huo ni ukemavu au niseme udumavu wa akili, kwamba Nyerere alitakiwa kurekebisha kila kitu ndani ya hii nchi kwasababu aliowaachia wanafikiria ufisadi tu!.
Nyerere ndie aliwachorea ramani muibe mali za umma mjilimbikizie mali, wakati yeye hakufanya hivyo!Yeye ndiye aliyechora ramani. Aliyeweka mfumo.
Waliofuata walipita kwenye njia aliyoichonga yeye mwenyewe.
Nyerere ndie aliwachorea ramani muibe mali za umma mjilimbikizie mali, wakati yeye hakufanya hivyo!
Nyerere akawaambia muuze nyumba za serikali kwa bei rahisi, wakati yeye hakuwahi kuuza hata moja!.
Nyerere akayaacha madini ardhini mpaka tuwe na uwezo wetu kuyachimba, kisha nyie mkaja kuwapa wazungu kwa bei rahisi mkihongwa 10%!
Watakwambia Nyerere aliondoka madarakani miaka arobaini iliyopita. Huku wakijitoa ufahamu kwamba nchi inaongozwa na mifumo. MIFUMO ndiyo kila kitu.
Leo hii taifa kama Marekani limefika hapa lilipo kwasababu ya katiba iliyoandanikwa mwaka 1787, na waasisi wa taifa lile. Wangajichanganya tu na kujenga msingi mbovu, Marekani isingevuka 1864.
Ila ndiyo hivyo UFAHAMU ni tatizo kubwa mno kwa Watanzania!
Unajua hili sijui... unajua lile sijui....!Wanafikiri ufisadi kwa sababu ya mfumo na sheria alizoziweka.
Wewe utafanya ufisadi kwa namna ipi wakati sheria inakubana?
Unajua nchi hii wapo wanaofanya ufisadi kwa Mujibu wa sheria na katiba ya Nyerere?
Najua hili hulijui.
Unajua utekaji na mauaji kikatiba kuna watu wanaweza kuyafanya, yaani wanaruhusa ya kufanya?
Najua hujui.
Unalaumu wezi na mafisadi wakati wanafanya hayo kikatiba, wanalinda katiba
Nyerere aliunda vipi mfumo wa kuwalinda mafisadi, ikiwa yeye binafsi hakuwa fisadi?!Ndio alichora hiyo ramani.
Na nikuhakikishie ndiye aliyeunda mfumo wa kulinda mafisadi, wezi na wauaji
Unachotakiwa kuuliza ni kivipi?
Kumtoa Nyerere kwenye yanayoendelea ni kazi sana.
Unajua hili sijui... unajua lile sijui....!
Nyerere ndie alifufuka akawaambia mbadilishe sheria ya usalama wa taifa iki waanze kututeka na kutuua hovyo?!
Naacha vipi kumtoa mtu asiyekuwepo!Hizo sheria zinatungwa kwa mujibu wa Katiba sijui kama unajua hilo.
Hizo sheria wanausalama katika majukumu yao zinavunja katiba ya Nyerere? Jibu ni hapana hazivunji.
Sasa kipi kinakufanya umtoe Nyerere?
Nyerere aliunda vipi mfumo wa kuwalinda mafisadi, ikiwa yeye binafsi hakuwa fisadi?!
Sijui unaandika vitu gani.
How comes unasema nchi inaongozwa na mifumo halafu unamlaumu Nyerere!
Umejielewa kweli?!
Au kwako Nyerere ndie alikuwa mfumo wenyewe?!
Ujuaji ukizidi ni tatizo.
Naacha vipi kumtoa mtu asiyekuwepo!
Kwani leo mkiwa mnafanya amendment ya sheria kule bungeni ili ziwalinde Nyerere yupo?!
Nioneshe kwenye hiyo Katiba ya 1977, ni wapi imeruhusu UTEKAJI, DHULMA, WIZI, MAUAJI, WIZI WA KURA na UFISADI??Yes,wengi wanamsifia na kumuona mzalendo na aliyekuwa na nia ya dhati kwa Taifa,nakubari katika uzalendo lakini si katika nia ya dhata kuhusu mustakabali wa kesho wa taifa hili.
Mambo mengi yanayotokea katika taifa hili kwa sasa chanzo chake kikubwa ni katika sheria mbovu zilizopo tangu mwanzo zilizo athiri mfumo wa utawala bora,haki na usawa.
Katiba ndio sheria ya kwanza iliyoharibu mfumo wa utawala bora wa Taifa hili kwa kutoa madaraka makubwa kwa mtu ambaye alidhaniwa hawezi kukosea na ikampatia kinga.
katiba ni ya mwaka 1977,wakati inaundwa Mwl.Nyerer alikuwepo madarakani,maana yake mchakato mzima uliasisiwa na kusimamiwa na yeye kutokana na nafasi yake kwa wakati huo,maana yake vifungu vyote alivijua kabla katiba haijapitishwa,na bila shaka alijua madhara ya ya baadhi ya ibara hususani ile ya 46,ilikuwaje hakutaka irekebishwe kabla haijapitishwa ili hali alijua madhara yake?,yamkini alitaka kujilinda.
Mara kadhaa alisikika katika mikutano akilalama kuhusu katiba na mamlka makubwa ya Rais,najiuliza iliwekanaje mtu aliye husika kwa kiasi kikubwa kuipitisha katiba hiyo ndio alalamike mapungufu yake ?,kwamba hakuyaona wakati huo akayaona sasa?,ni uzindukaya wa hovyo sana.
Huyu mzee na genge lake mzee Chenge ndio chanzo cha haya yote haya,mzee Warioba naye najiuliza alishindwa kumshauri mchonga meno au alishauriwa akashupaza shingo?
Haya Taifa linapitia chanzo ni huyu mzee ndio wakulaumiwa ,asingeruhusu mambo ya ajabu katika katiba haya mambo yasingefikia hapa yalipo.
Hawakujua kwamba hata ZUMBUKUKU anaweza kuwa Rais wakashindwa kutengeneza sheria zenye kumtia hofu?,leo anaibuka mtu mmoja na kusema "katiba ni kijitabu tu".
Sioni sababu ya kumpraise alidhamiria Taifa kuja kunajisiwa.