Mfumo= Watu+Sera+Sheria+Taasisi
Hivi kwenye utawala hupimwa kwa kipimo kiitwacho PERSISTENCE METRIC ambacho huangalia kwa muda ganii na jinsi gani MFUMO (Watu+Sera+Sheria+Taasisi) huathiri maisha ya vizazi
===================================================================================
Unaweza kuhisi umeongea kitu cha maana kumbe una ufahamu finyu kuhusu utawala. Hili ndilo tatizo lako wewe. Unaamini kwasababu wewe hukifahamu hiki basi na mwingine lazima atakuwa hakifahamu. Una matatizo makubwa kichwani mwako, Bwana Denoo G.
Kiutawala, taasisi zote duniani hata kama ziko (Autonomous/Semi-autonomous) ni kama kiumbe hai kinachojiongoza chenyewe. Lakini lazima kiwe na kichwa, ambaye kitaalamu tunamuita MTENDAJI MKUU (CHIEF EXECUTIVE), ambaye huamua mwelekeo mzima wa taasisi kwa wakati huo. Hili limesemwa na wataalamu wa utawala tokea miaka ya 1600 kama Locke, Hobbes na Montesquie (In Theory of Social Contract) na hata wasomi wa miaka hii ya karibuni kama Prof Max Webber, Issa G Shivji wamethibitisha nalolisema, kwamba mifumo hutegemea sana kiongozi binafsi (CHARISMATIC SYSTEMS).
Kwenye sheria ya katiba (CONSTITUTIONAL LAW) wale waliosoma sayansi ya siasa (Political Science) na sheria (Law) hufundishwa hili mapema wakiwa mwaka wa kwanza. Hufundishwa kwamba kwenye mifumo ya utawala wa nchi (State Systems) hasahasa nchi zetu ambazo zilitawaliwa na Uingereza zinafuata THE WESTMINSTER MODEL, mfumo huwa na uwajibikaji wa aina mbili: Uwajibikaji wa Jumla (Collective Ministerial Responsibility) na Uwajibikaji Binafsi(Individual Ministerial Responsibility).
Kuna mambo kwenye mifumo ya utawala wa nchi huwa yanapimwa kwa kurunzi maamuzi ya uwajibikaji wa jumla (Collective Ministerial Responsibility) na kuna maamuzi hupimwa kwa kurunzi ya (Individual Ministerial Responsibility). Kiutawala na dunia ya sasa, MFUMO unatakiwa ufuate sana COLLECTIVE MINISTERIAL RESPONSIBILITY, kuliko INDIVIDUAL MINISTERIAL RESPONSIBILITY. Bahati mbaya mno Tanzania katiba zake zote tokea 1964 zilitengeneza kitu kinaitwa IMPERIAL PRESIDENCY (Uraisi wa Kifalme) ambao unampa Kiongozi Mmoja ndani ya mfumo nguvu kubwa za kiutendaji kuliko wengine, jambo ambalo halitakiwi.
Hata Tundu Lissu ambaye mnamshabikia amekuwa akilisema sana hili miaka. Inaonesha hukuelewa anamaanisha hata nini. Maamuzi mengi mabaya yalifanywa na Mzee Nyerere kama CHIEF EXECUTIVE OF THE COUNTRY na kutekelezwa katika ngazi za kimfumo na viongozi wake wa chini. Lakini pia tunapoongelea mfumo hatuangalii tu utendaji, bali tunaangalia SERA, SHERIA na TAASISI ambazo zilitungwa au kuanzishwa wakati wa Mzee Nyerere na namna gani mpaka leo zinaendelea kutumika kuathiri maisha ya watanzania.
Asilimia 70% ya sheria kandamizi na sera zake zilitungwa na kuanzisha taasisi zake kipindi cha Mzee Nyerere akiwa Raisi. Hivyo tutaisema serikali yake kwa haya maovu (Collective Ministerial Responsibility) na yeye binafsi (Individual Collective Responsibility).Hivi ndivyo mifumo ya dunia ya kiutawala ipo.
SASA KAMA HUKUWA UNALIFAHAMU HILI, THAT's YOUR PROBLEM........
YOU CAN GET ANGRY, THROW TANTRUMS, DRENCH IN YOUR SORROWS and WALLOW IN YOUR TEARS ila huu ndiyo ukweli wa kiutawala duniani kote, wewe MTANZANIA mmoja huwezi kuupinga hata kama unauchukia na haukubaliani nao.