Anayepaswa kulaumiwa kwanza katika haya yanayoendelea katika Taifa ni Hayati Mwl. Nyerere

Hata tukimlaumu haibadilishi chochote. Ameshakufa, na huenda mpaka leo ameshaoza kabisa. Kuna hawa wengine waliofanya uteuzi wao wa kutatanisha ile 2015! Madhara yake mpaka leo yanaendelea kulitafuna Taifa. Tunafanyaje?
 
Kwanini unahangaika na marehemu, hivi kina nchi ilikuwa na mfumo kama USSR lakini ilianguka, gen Z wameonyesha njia lakini wewe kazi yako ni kulalamika mtandaoni.
Mabadiliko yanaanzia kwako mwenyewe, hawa tunaowalaumu , wanaotumiwa tunaishi nao ndani ya jamii kwanini usikae na kufikiri njia mbadala ya kuwashugulikia.
Kipimo cha akili ni pale unapokabiliwa na tatizo na kutafuta njia ya kulitatua, kwa kipimo hicho akili yako ni zero.
 
How comes unasema nchi inaongozwa na mifumo halafu unamlaumu Nyerere!

Umejielewa kweli?!

Au kwako Nyerere ndie alikuwa mfumo wenyewe?!

Ujuaji ukizidi ni tatizo.

Nyerere ndiye aliyesuka Mifumo

1. Mifumo ya kisheria na taratibu. Kupitia Katiba na Sera za nchi

2. Mifumo ya kimawazo na kifikra.
Ukisikia zidumu fikra za mwenyekiti. Na mila nyingi za ccm na nchi hii basi muasisi wake ni Nyerere

Ingawaje yapo mazuri aliyoyafanya lakini mabaya yapo.
 
yule mzee ndiye chanzo cha umasikini Tanzania katikati ya utajiri mwingi. Ndiye mhusika mkuu wa kuiua Tanganyika yetu. Alikuwa mshirikina kupindukia,
Yule ambaye hakuwahi kuwa na kashfa ya ufisadi ndie chanzo cha umaskini wetu!.

Kosa lake kuyaacha madini ardhini kisha nyie mkaja kuyachezea, halafu mnarudi kumlaumu yeye!

Huu ujinga wenu ni next level.
 
Acheni hizi ngonjera zenu.

Nyerere licha ya Urais wake, nae alikuwa mwanadamu kama mimi na wewe.

Ni ujinga kumlaumu Nyerere leo kwa mnachodai makosa yake, ikiwa hata sisi tunaweza kuyarekebisha.

Huo ni ulemavu au niseme udumavu wa akili, kwamba Nyerere alitakiwa kurekebisha kila kitu ndani ya hii nchi kwasababu aliowaachia wanafikiria ufisadi tu!.

Somebody pale juu kaja na msemo mabadiliko yanaanza na wewe, nyie kwenu mabadiliko yalitakiwa yatoke kwa Nyerere!.
 
Yule ambaye hakuwahi kuwa na kashfa ya ufisadi ndie chanzo cha umaskini wetu!.

Kosa lake kuyaacha madini ardhini kisha nyie mkaja kuyachezea, halafu mnarudi kumlaumu yeye!

Huu ujinga wenu ni next level.

Yeye ndiye aliyechora ramani. Aliyeweka mfumo.

Waliofuata walipita kwenye njia aliyoichonga yeye mwenyewe.
 

Wanafikiri ufisadi kwa sababu ya mfumo na sheria alizoziweka.


Wewe utafanya ufisadi kwa namna ipi wakati sheria inakubana?

Unajua nchi hii wapo wanaofanya ufisadi kwa Mujibu wa sheria na katiba ya Nyerere?

Najua hili hulijui.

Unajua utekaji na mauaji kikatiba kuna watu wanaweza kuyafanya, yaani wanaruhusa ya kufanya?
Najua hujui.

Unalaumu wezi na mafisadi wakati wanafanya hayo kikatiba, wanalinda katiba
 
Yeye ndiye aliyechora ramani. Aliyeweka mfumo.

Waliofuata walipita kwenye njia aliyoichonga yeye mwenyewe.
Nyerere ndie aliwachorea ramani muibe mali za umma mjilimbikizie mali, wakati yeye hakufanya hivyo!

Nyerere akawaambia muuze nyumba za serikali kwa bei rahisi, wakati yeye hakuwahi kuuza hata moja!.

Nyerere akayaacha madini ardhini mpaka tuwe na uwezo wetu kuyachimba, kisha nyie mkaja kuwapa wazungu kwa bei rahisi mkihongwa 10%!
 

Ndio alichora hiyo ramani.
Na nikuhakikishie ndiye aliyeunda mfumo wa kulinda mafisadi, wezi na wauaji

Unachotakiwa kuuliza ni kivipi?

Kumtoa Nyerere kwenye yanayoendelea ni kazi sana.
 

Kama ni mifumo kwa nini msiifumue sasa muweke yenye akili nyie wenye ufahamu tangu kafa? Miaka 40 ni michache kuunda mifumo mipya??
 
Unajua hili sijui... unajua lile sijui....!

Nyerere ndie alifufuka akawaambia mbadilishe sheria ya usalama wa taifa iki waanze kututeka na kutuua hovyo?!
 
Ndio alichora hiyo ramani.
Na nikuhakikishie ndiye aliyeunda mfumo wa kulinda mafisadi, wezi na wauaji

Unachotakiwa kuuliza ni kivipi?

Kumtoa Nyerere kwenye yanayoendelea ni kazi sana.
Nyerere aliunda vipi mfumo wa kuwalinda mafisadi, ikiwa yeye binafsi hakuwa fisadi?!

Sijui unaandika vitu gani.
 
Unajua hili sijui... unajua lile sijui....!

Nyerere ndie alifufuka akawaambia mbadilishe sheria ya usalama wa taifa iki waanze kututeka na kutuua hovyo?!

Hizo sheria zinatungwa kwa mujibu wa Katiba sijui kama unajua hilo.

Hizo sheria wanausalama katika majukumu yao zinavunja katiba ya Nyerere? Jibu ni hapana hazivunji.

Sasa kipi kinakufanya umtoe Nyerere?
 
Hizo sheria zinatungwa kwa mujibu wa Katiba sijui kama unajua hilo.

Hizo sheria wanausalama katika majukumu yao zinavunja katiba ya Nyerere? Jibu ni hapana hazivunji.

Sasa kipi kinakufanya umtoe Nyerere?
Naacha vipi kumtoa mtu asiyekuwepo!

Kwani leo mkiwa mnafanya amendment ya sheria kule bungeni ili ziwalinde Nyerere yupo?!
 
Nyerere aliunda vipi mfumo wa kuwalinda mafisadi, ikiwa yeye binafsi hakuwa fisadi?!

Sijui unaandika vitu gani.

Anaweza kuwa hakuwa fisadi lakini hiyo haiondoi ukweli kuwa yeye ndiye aliyeunda mfumo wa kifisadi.

Nitakupa mfumo mmoja ambao utakupa picha kamili kwa nini yeye ni sehemu ya tatizo.

Unafikiri kwa nini Rais wa Tanzania hatakiwi kushtakiwa?

Kama Nyerere alikuwa ana ona mbali na hataki mafisadi, wezi na wauaji unafikiri kwa nini hiyo sheria ipo ya kumfanya Rais kuwa Mungu?

Then leo Rais akifanya wajibu wa kimungu mnapiga kelele kanakwamba yeye ndiye aliyeunda hizo sheria.

Unavyomuona Samia pale, yeye kwa mujibu wa katiba anasifa za mungy. Anaweza kuamua lolote hapo ulipo na asiwepo mtu wa kumzuia.
Kwa sababu anafanya mambo kwa mujibu wa katiba.

Hashtakiwi na kisheria na kifalsafa mtu asiyetakiwa kushtakiwa ni yule asiyefanya makosa na ambaye hafanyi makosa.
 
How comes unasema nchi inaongozwa na mifumo halafu unamlaumu Nyerere!

Umejielewa kweli?!

Au kwako Nyerere ndie alikuwa mfumo wenyewe?!

Ujuaji ukizidi ni tatizo.
Mfumo= Watu+Sera+Sheria+Taasisi

Hivi kwenye utawala hupimwa kwa kipimo kiitwacho PERSISTENCE METRIC ambacho huangalia kwa muda ganii na jinsi gani MFUMO (Watu+Sera+Sheria+Taasisi) huathiri maisha ya vizazi
===================================================================================

Unaweza kuhisi umeongea kitu cha maana kumbe una ufahamu finyu kuhusu utawala. Hili ndilo tatizo lako wewe. Unaamini kwasababu wewe hukifahamu hiki basi na mwingine lazima atakuwa hakifahamu. Una matatizo makubwa kichwani mwako, Bwana Denoo G.

Kiutawala, taasisi zote duniani hata kama ziko (Autonomous/Semi-autonomous) ni kama kiumbe hai kinachojiongoza chenyewe. Lakini lazima kiwe na kichwa, ambaye kitaalamu tunamuita MTENDAJI MKUU (CHIEF EXECUTIVE), ambaye huamua mwelekeo mzima wa taasisi kwa wakati huo. Hili limesemwa na wataalamu wa utawala tokea miaka ya 1600 kama Locke, Hobbes na Montesquie (In Theory of Social Contract) na hata wasomi wa miaka hii ya karibuni kama Prof Max Webber, Issa G Shivji wamethibitisha nalolisema, kwamba mifumo hutegemea sana kiongozi binafsi (CHARISMATIC SYSTEMS).

Kwenye sheria ya katiba (CONSTITUTIONAL LAW) wale waliosoma sayansi ya siasa (Political Science) na sheria (Law) hufundishwa hili mapema wakiwa mwaka wa kwanza. Hufundishwa kwamba kwenye mifumo ya utawala wa nchi (State Systems) hasahasa nchi zetu ambazo zilitawaliwa na Uingereza zinafuata THE WESTMINSTER MODEL, mfumo huwa na uwajibikaji wa aina mbili: Uwajibikaji wa Jumla (Collective Ministerial Responsibility) na Uwajibikaji Binafsi(Individual Ministerial Responsibility).

Kuna mambo kwenye mifumo ya utawala wa nchi huwa yanapimwa kwa kurunzi maamuzi ya uwajibikaji wa jumla (Collective Ministerial Responsibility) na kuna maamuzi hupimwa kwa kurunzi ya (Individual Ministerial Responsibility). Kiutawala na dunia ya sasa, MFUMO unatakiwa ufuate sana COLLECTIVE MINISTERIAL RESPONSIBILITY, kuliko INDIVIDUAL MINISTERIAL RESPONSIBILITY. Bahati mbaya mno Tanzania katiba zake zote tokea 1964 zilitengeneza kitu kinaitwa IMPERIAL PRESIDENCY (Uraisi wa Kifalme) ambao unampa Kiongozi Mmoja ndani ya mfumo nguvu kubwa za kiutendaji kuliko wengine, jambo ambalo halitakiwi.

Hata Tundu Lissu ambaye mnamshabikia amekuwa akilisema sana hili miaka. Inaonesha hukuelewa anamaanisha hata nini. Maamuzi mengi mabaya yalifanywa na Mzee Nyerere kama CHIEF EXECUTIVE OF THE COUNTRY na kutekelezwa katika ngazi za kimfumo na viongozi wake wa chini. Lakini pia tunapoongelea mfumo hatuangalii tu utendaji, bali tunaangalia SERA, SHERIA na TAASISI ambazo zilitungwa au kuanzishwa wakati wa Mzee Nyerere na namna gani mpaka leo zinaendelea kutumika kuathiri maisha ya watanzania.

Asilimia 70% ya sheria kandamizi na sera zake zilitungwa na kuanzisha taasisi zake kipindi cha Mzee Nyerere akiwa Raisi. Hivyo tutaisema serikali yake kwa haya maovu (Collective Ministerial Responsibility) na yeye binafsi (Individual Collective Responsibility).Hivi ndivyo mifumo ya dunia ya kiutawala ipo.

SASA KAMA HUKUWA UNALIFAHAMU HILI, THAT's YOUR PROBLEM........

YOU CAN GET ANGRY, THROW TANTRUMS, DRENCH IN YOUR SORROWS and WALLOW IN YOUR TEARS ila huu ndiyo ukweli wa kiutawala duniani kote, wewe MTANZANIA mmoja huwezi kuupinga hata kama unauchukia na haukubaliani nao.
​
 
Naacha vipi kumtoa mtu asiyekuwepo!

Kwani leo mkiwa mnafanya amendment ya sheria kule bungeni ili ziwalinde Nyerere yupo?!

Unamtetea πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜„
Lakini utetezi wako hauna nguvu.

Ungekuwa kwenye Power yaani umerithi utawala kwa Babu yako Nyerere ungefanya hizo Amendments hasa zinazogusa maslahi ya Utawala wako?

Hivi unajua Kina Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli na sasa Samia ni Watoto na wajukuu wa utawala wa Nyerere? Unalijua hilo?

Au unataka kusema siku hizi Nyoka anazaa Jongoo?

Wewe ambaye sio mtoto wa Nyerere kimamlaka ndio utaona matatizo ila wenye familia wanaishi maisha ya Babu yao, Nyerere. Na wanafuata mfumo aliouacha Nyerere.
 
Nioneshe kwenye hiyo Katiba ya 1977, ni wapi imeruhusu UTEKAJI, DHULMA, WIZI, MAUAJI, WIZI WA KURA na UFISADI??

Hiyo katiba mpya itakuwa inashika bunduki kulazimisha watu KUITII???

Kwa akili zenu za kijinga, mnadhani MTAWALA MUOVU anafuata Katiba hata iwe nzuri???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…