Anayepaswa kulaumiwa kwanza katika haya yanayoendelea katika Taifa ni Hayati Mwl. Nyerere

Usiseme anaweza, andika Nyerere hakuwa fisadi, kama una ushahidi wowote wa ufiasadi wake tuwekee hapa.

Mtu ambaye hakuwa na tone la ufisadi, kusema aliunda mfumo wa kifisadi kwasababu aliacha sheria ya Rais kutoshtakiwa, ni hoja dhaifu.

Jiulize, kwanini leo marais wanaogopa kupelekwa mahakamani?

Mostly wanajua ni kwasababu ya ufisadi wao, mara wameuza bandari, mara wametoa gesi ya Mtwara, hii ndio sababu kwao kuogopa kushtakiwa.

Nimeshakwambia Nyerere hakuwa malaika atufanyie kila kitu, pale alipoacha na mapungufu, tuyarekebishe sisi, kuendelea kumlaumu ni ukemavu.
 

Hawezi kukuelewa.
 
kuna mtu niliwahi mwambia ulichosema hapa ndo kama ufahamu ukamjia na kuelewa kwamba chanzo cha matatizo tunayopitia leo ni ile awamu ya kwanza
 
Unamaanisha Magufuli na hata Samia siku akifa tusiwalaumu kwa yaliyotokea oktoba 29, na vifo vya kina Ben Saanane?

Hakuna nyumba inayojengwa bila msingi, ukikosea msingi umeharibu mfumo mzima.

Yule mzee alikuwa na tabia za kimasikini si ajabu ndio maana hata familia yake ipo ipo tu leo. Anakubalika kwa mababy boomers GenX na millennials tu, maana hawa ni kizazi chenye uoga,mafisadi na akili za kupelekeshwa
 

Rais kama hashtakiwi huoni kwamba amepewa mamlaka ya kufanya chochote na bila kuwajibishws na yeyote?,

Hujui msingi mkuu wa ufisadi, utekaji, wizi wa uchaguzi, na mambo mengine unatoka kwenye mamlaka ya urais? Hujui hili kumbe?

Wewe unapoambiwa maelekezo kutoka juu unafikiri hayapo kikatiba?😂😂
 
Ukisema namtetea sikuelewi.

Pale juu umetaja sheria mbovu ambazo unaamini Nyerere ndie alisababisha zikawepo.

Mimi nikakuuliza, hata kama Nyerere aliziacha, mbona bado mnaendelea kuziboresha wakati Nyerere hayupo?!

Sasa hapo naacha vipi kumtoa Nyerere, au kwako Nyerere bado anaishi mpaka leo!.
 

Nimetumia neno anaweza hakuwa fisadi kwa sababu siwezi kutoa hakiksho la asilimia 100.

Ninachojua yeye ndiye msingi Mkuu wa ufisadi kupitia mfumo na Katiba aliyoiweka.

Huenda wakati anaweza hiyo mifumo na katiba hakukumbuka mifumo hiyo pia inawapa nguvu watu ambao watakuja kuongoza wakawa mafisadi.

Ukitaka kujua ninachokisema na watu wenye mtazamo kama wangu.
Nyerere alishawahi kukiri kuwa Katiba na Mfumo aliouweka unamuweza mtawala kuwa mungumtu au Dikteta. Na hakutaka ubadilishwe.

Unajua maana ya udikteta na umungu mtu?
 
Matatizo ya leo chanzo chake ni makosa ya jana, na shida sio makosa ya jana bali kiburi cha leo.

Mwl Nyerere hawezikwepa lawama, hata yeye mwenyewe binafsi alijilaumu kama ulivyosema. Lakini pamoja na hilo, lawama juu yake haziwezi kutusaidia. Mzee kuna sehemu alikwama ni kama alidhani atakuwa on the chair forever 🤔
 
Umeandika, mfumo = watu, sasa Nyerere ni watu au mtu!.

Kama yeye hakuja na hilo wazo, kwanini hao watu wengine hawakumshawishi abadilishe huo mfumo?!

Nyerere wasn't ana angel kama mnavyotaka kuiweka hapa.
 

Nani abadilishe sasa?

Waliopo madarakani ni watoto na wajukuu wa Nyerere kiutawala na kimfumo. Inaweza kuwa sio kibaolojia

Wao mfumo waliourithi kwa Baba na Babu yao, Nyerere. Unawafavour kama ulivyom-favour Nyerere.
Sijui kama unaelewa jambo hilo.

Kama nyerere angekuwa mtakatifu kuliko Waliopo madarakani ninakuhakikishia huu mfumo na katiba waliyoirithi kwa Baba na Babu yao haviendani na mawazo na maslahi yao.

Hawabadilishi huo mfumo na Katiba ya Nyerere kwa sababu wao ni Nyerere wadogo
 
Huwezi kumuita Nyerere ndie msingi mkuu wa ufisadi, ikiwa yeye "msingi" hakujihusiha na hilo jambo.

Nyerere hakuwa malaika, kama aliacha mifumo iliyokuwepo kwa nia njema, kisha nyie mkaja kuitumia kwa nia ovu, hilo haliwezi kuwa kosa lake.
 
Kwanini alaumiwe babu wa Mwitongo? Hii nchi watu wa kwanza kuwalaumu ni nyie nyie watendaji wa Rais maana hamfuati mama anachosema huwa mnajiamlia mambo tu
 
Kubadilisha mfumo sio kazi ya watawala kwasababu unawanufaisha wao, hiyo ni kazi yetu.
 
Huwezi kumuita Nyerere ndie msingi mkuu wa ufisadi, ikiwa yeye "msingi" hakujihusiha na hilo jambo.

Nyerere hakuwa malaika, kama aliacha mifumo iliyokuwepo kwa nia njema, kisha nyie mkaja kuitumia kwa nia ovu, hilo haliwezi kuwa kosa lake.

Hakujihusisha kivipi wakati aliunda mfumo na katiba inayoweza kulinda mafisadi, madikteta na wauaji?

Hivi unajua msingi wa utawala ulipo kweli?
 
Rais hashtakiwi kwa mambo aliyofanya yaliyoko ndani ya mamlaka yake kisheria na kikatiba.

Huwezi kusema Rais hashtakiwi kwa KUCHUKUA MUME wa mtu.

Utakuwa una akili ndogo kama NYUMBU.

Lakini pia hukumu yake inaweza kuwa KURA, kama inaheshimika lakini.
 
Kubadilisha mfumo sio kazi ya watawala kwasababu unawanufaisha wao, hiyo ni kazi yetu.

Pole sana Mkuu.

Kazi yako na nani? Wewe ni mwananchi wa kawaida huna uwezo wa kubadilisha chochote kwenye serikali achilia mbali mfumo.
Labda siku utoke kwenye uananchi uwe Rais hapo sawa.

Sidhani hata kama unajua mifumo inajengwa na kina nani?

Mwananchi wajibu wake sio huo. Na hapo ndipo ilipo tofauti ya mwananchi na Kiongozi.
Sio kila mwananchi ni Kiongozi.
 

Unachekesha kweli

Kwamba Rais ukamshtaki kwa kukuibia mkeo/mumeo?
Mtu anaweza kuagiza watu wakukamate hapo na akatoa maelekezo bila kujali sheria ukamshtaki kwa makosa kama hayo?

Hapo wengi ndipo mnafeli.

Ukishakuwa Rais kwa Tanzania wewe ni zaidi ya binadamu wa kawaida. Ni mungumtu kwa mujibu wa sheria.

Na hapo ndipo lilipo kosa la Nyerere. Alifikiri kila mtu atakuwa Mwema, au atakuwa na busara, au atakuwa mwerevu.

Wapo watu ni Wakali, wakorofi, wahalifu na hawana busara kwa katiba yetu watu aina hiyo wakipata madaraka watatesa sana na hawatakuwa na makosa kwa sababu hawavunji katiba
 
Huwezi kujua gharama nilizolipa,mimi inawezekana nisingekuwa naandika uzi huu hapa sababu ya MO29,mimi ni millenial,lakini niliwajibiki kama Gen-Z,nililipa gharama,,yawezekana wewe ulishuhudia kwenye clips na picha yale mauaji,lakini mimi nilishuhudia kwa macho yangu, na nilibeba majerua na hata maiti,usiandike kwa hisia hatujuani,mimi nina ushuhuda wa wazi.Namaanisha nilichokiandika.
 
Kama ni mifumo kwa nini msiifumue sasa muweke yenye akili nyie wenye ufahamu tangu kafa? Miaka 40 ni michache kuunda mifumo mipya??
Mfumo unatokana na SOCIAL CONTRACT baina ya watawala na watawaliwa: Uko hivyo ulivyo ni kwasababu ya mambo yale yote yaliyofanywa na wahenga wako kipindi nchi hii inasisiwa. NDIYO, kitaalamu mifumo huwa inabadilishwa. Inaweza kubadilishwa kupitia CONSTITUTIONAL and UNCONSTITUTIONAL MEANS.

CONSTITUTIONAL MEANS huwezekana endapo tu jamii itakuwa ni ya kidemokrasia na iliyoendelea sana. Wasomi wengi wakiwepo na watu wa uchumi wa kiwango cha kati (Robust Middle-Class) ambao ndiyo wenye uchumi wa nchi na wanalazimika kulinda mfumo mpya ili kutunza maslahi yao. Mfano, ni The Glorious Revolution in England 1688, mapinduzi yalifanywa na wasomi ambao ni Middle-Class (The Bourgoiusie). Hii njia mbali na kuleta mabadiliko, huwa na tabia ya kwenda taratibu. Mabadiliko yake hayaji ndani ya usiku mmoja kwasababu hufanywa na kundi kubwa la watu.

Jambo jingine kubwa ambalo ni la kiusalama na kitaalamu, ni kwamba watu wengi wa mfumo wanashika hizo nafasi kutokana na kujuaja (Family Connection). Leo hii CCM wengi wanaoshika nafasi kubwa ni kwasababu wazazi wao walishawahi kuwa na nafasi kubwa serikalini miaka ya nyuma. Hata jeshini, polisi na usalama iko hivyohivyo. Hivyo kubadilisha mfumo huwa ni ngumu kwasababu waendesha mfumo huwa wanakuwa na tamaduni za zamani.

Hivyo tunaweza kutengeneza katiba mpya leo hii, lakini tamaduni (Customs) ambazo zimekuwepo haziwezi kubadilika ndani ya usiku mmoja. Mpaka kizazi kimoja kipite ndiyo mambo yatabadilika. Mabadiliki ya kimfumo hayatokei tu kwenye vitabu, bali kiutamaduni, na huchukua vizazi vingi mpaka zitokea na kujengeka tamaduni mpya. Marekani ilipitisha katiba mpya 1788 lakini faida walikuja kuzipata kizazi kingine baada ya miaka 100 (The Gilded Age) huko.

UNCONSTITUTIONAL MEANS hii ni njia ya pili, ambapo kikundi cha watu kinakuwa kimekereka na mfumo uliopo na kinaamua kutumia nguvu kupindua kabisa Mifumo ya nchi. Siyo tu mifumo ya kiutawala, bali mifumo ya kiutamaduni na taasisi zake. Hivyo watapindua serikali, lakini watapiga marufuku baadhi ya tamaduni za nchi ambazo ziliwezesha serikali dhalimu kutawala kwa muda mrefu. Mfano hai ni huu: French Revolution 1789, ilifanywa na The Jacobins, na haikupindua serikali ya kifalme tu, bali ilizifuta taasisi za kitamaduni ambazo zilisaidia mfumo wa ufalme kuwepo nchini Ufaransa.

The Clergy (Kanisa Katoliki) lilishughulikiwa vilivyo kwasababu ndilo lilikuwa linasaidia kuhalalisha utawala wa kifalme (Legitimized The Divine Right). Hivyo wahuni kina Robespierre walivyoshika nchi, wakachinja Louis, lakini wakaanza kuua MABWANYENYE (FEUDAL LORDS) na Mapadre (Priests) kwa maelfu. Baada ya kuwachinja, ndiyo mfumo ukabomoka na wakatengeneza THE FIRST REPUBLIC.
=================================================================================

Hili suala nalolisema limefanyiwa tafiti za kisomi duniani kote. Vinara wa hizi tafiti kuhusu kupindua mifumo na kujenga mipya ni wayahudi Prof Hans Kelsen na Karl Marx. Kelsen amezungumzia Revolution and The Constitution, huku Marx akizungumzia Revolution vs BASE+SUPERSTRUCTURE.

=======================================================================================

SASA NINYI WATANGANYIKA na akili zenu: Kwanza kabisa mnataka mabadiliko ya kimfumo kwa kupitia KATIBA, jambo ni jema, lakini halitachukua mwaka mmoja kuleta mabadiliko kama mnavyotarajia. KATIBA mpya itabadilisha muunda wa kitaasisi, kugawanya madaraka na kuondoa baadhi ya sheria. Lakini haitaondoa taasisi zote, sheria zote na tamaduni zote. Kuna taasisi ambazo zimeanzishwa na CCM zitaendelea kubaki na zitakuwa na ushawishi mkubwa, mpaka muda utakapopita na watu kuondoka ndipo zitabadilika. Huu ndiyo ukweli mchungu ambao hamuambiwi, wala hamtaki kuusikia.

Leo hii CHADEMA wakapewa nchi, bado wataendelea kutegemea taasisi ambazo kifalsafa zimekuwa za CCM. Mfano, TPDF + TISS + PT. Lakini pia hata matajiri walioshika uchumi wengi wao ni watu wa CCM, ambao CHADEMA itatakiwa aidha iwavumilie, au iwafilisi na kuhatarisha uchumi wa nchi. Mwaka 2012 Mizengo Pinda aliwahi kusema maneno machungu mbele ya ummah "Tukiwakamata mafisadi, uchumi wa nchi utayumba" na hili lilithibitika kipindi cha utawala wa JPM. Mafisadi wengi ndiyo walipa kodi wakubwa, ndiyo waagiza bidhaa wakubwa, ndiyo watoa ajira wakubwa na ndiyo wazalishaji wakubwa wa chakula.

=======================================================================================
MAPINDUZI WA MFUMO KWA FUJO, hakuna mwenye uwezo kufanya kati ya wale wanaopiga makelele mitandaoni. Wewe mwenyewe uliona tu kilichotokea 29 Oktoba 2025. Sasa ile ndiyo gharama ambayo mnatakiwa muilipie ili kubadulisha mfumo wote kwa haraka. Mnapindua serikali, mnafutilia mbali katiba, mnatangaza nchi kutawaliwa kijeshi (Rule by Marshal Law) huku mkishughulikia walinda mfumo kwa maelfu. Kiufupi nchi itakuwa imejaa mifereji ya damu.

========================================================================================
YOTE HAYA MAWILI, hayatawezeka.

NDIYO MAANA tunasema unapokuwa kiongozi usipende kuamua kana kwamba nchi ni mali yako binafsi. Maamuzi ya leo ya Samia yatakuja kuiathiri Tanzania ya miaka 90. Mfano uuzwaji holela wa bandari yetu, madhara watayaona baada ya miaka 50. Wewe huwezi kuyaona. Mwinyi aliuza Loliondo na maeneo mengi ya mbugani kwa waarabu mnamo miaka ya 80's ila chamoto wanakiona Wamasai wa miaka ya 2026.

UKIJENGA MFUMO MBAYA, unakiachia kizazo kijacho BAD OPTIONS: Revolution/Gradual Change/Dissolution of State.

=================================================================================
ENIWEI since you are committed to misunderstanding me, I'll live you at it.

Ila ukweli ni kwamba Tanzania haiko tofauti na mataifa mengine ya jirani kwamba Mzee Nyerere afanya makosa halafu yasiathiri vizazi vijavyo. Wanaoamini hivi ndiyo maadui wakubwa wa maendeleo.
​
 
Kuleta porojo za kiwaki kwenye mambo ya msingi ni uponjoro wa hali ya juu,wewe huna tofauti na mtu yule aliyeambiwa flani kapasua ndoa na hiyo ndoo ilikuwa na maziwa halafu unauliza "maziwa yamemwagika?".

Nini chanco cha nguvu yakuwa na watawala waovu?,unachojaribu kusema ni kwamba sheria si kitu katika kufanya utawala uwe bora ama mbovu,SHERIA,MIFUMO,UTAWALA.

Mimi sio mjinga wala Mpumbavu, ila nina uhakika wewe si mjinga ila ni MPUMBAVU.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…