Jaman wale mnaopenda kulewa au kuchelewa kurudi majumbani mwenu kwa sababu za starehe kama hizi muwe mnakuwa na funguo za ziada ili ukirudi unajifungulia mwenyewe kuepusha vifo visivyo vya lazima.
Inachosha sana kuamshwa na mtu aliyetoka kwenye starehe zake ukatishe usingizi wako ili umfungulie
Huu uzi ni wa muda mrefu, lakini nimewiwa kuongea na mtu huyu...
Kwanza ninamasikitiko sana kama hii stori ni ya kweli, huyo mwanamke atakuwa amehusika moja kwa moja kumuua mumewe, na kama ilikuwa tabia yake kupita kwa kuruka, basi alijitakia kifo..
Hiyo sentensi ya mwisho kila nikiisoma najaa jazba, eti "inachosha sana kuamshwa na mtu aliyetoka kwenye starehe zake ukatishe usingizi wako ili umfungulie"
Sentensi imejaa makosa mengi ya kimantiki, na mengine ni ya ujinga tu wa kushindwa kuelewa.
1)Huyo unaemuita mtu siyo mtu tu kama watu wengine...
-Huyo ni mumeo.
-Ametoa pesa kwenu ili kukununua wewe uje umuhudumie.
-Huyo ndiyo kichwa cha nyumba kiongozi wa familia.
-Ndiye mbadala wa baba yako.
-Ndiye kachukua majukumu ya baba yako.
-Kwa hiyo huyo ni kama baba yako.
-Ndiye mwenye jukumu la kukuvisha, kukulisha unashiba mpaka unapata huyo usingizi wako.
-Hapangiwi muda wa kurudi.
-Ni jukumu lako kumfungulia mlango, kumtengea chakula ale, na kuhakikisha ameenda kulala vizuri..
Niishie tu hapa inatosha..
Mimi ukigoma kufungua mlango siku hiyo hiyo unaondoka na hautorudi kamwe..
Mwanaume ukiendekeza ujinga ujinga kwa mkeo unajitafutia kifo cha mapema, siyo hilo la kufunguliwa tu, kuna viujinga ujinga vingi. Ni bora uishi bachela, kuliko kuishi na mwanamke asiyetambua nafasi yako kama baba wa familia.