Anayeweza kutabiri Rais Samia atakakotupeleka kuanzia 2025-2030 wasome uzi huu

Anayeweza kutabiri Rais Samia atakakotupeleka kuanzia 2025-2030 wasome uzi huu

Ni ndoto tu, wananchi wengi watanzania wamekusanyika, mara nikaingia sehemu nikakuta ulinzi mkubwa sana. Mhe. Alokaa pale ni Ndugu mmoja hivi alikuwa mpole. Nikaambiwa unaenda wapi huyo ndo Rais. Ni kashituka nikaguna! Huyu? Kivipi! Nikaambiwa ondoka hii sehemu ya VIP, muda wowote huyu anatakiwa kuondoka hapa. Nenda kawaandae wananchi.

Basi nikarudi kwenye eneo la uwanja lilofurika watanzania wengi. Mara yule Mhe. Nilieelezwa ni Rais, akawa amepakiwa ktk gari la jeshi na ikatangazwa ndo Rais! mizinga ikapigwa, vifaru na magari ya jeshi hayo! Wananchi walijawa na furaha kubwa. Nderemo na vifijo, nikajiuliza tu nini kinaendelea? Mbona yule mkuu wetu simuoni? Yu wapi?

Cha ajabu baadae kuna bendera zilipepea pale sasa sijielewi nimechanganyikiwa! Rangi ya zile bendera Mmmh! wananchi waligawiwa sare za kuvaa, zile sare mmmh! na hivyo viatu Mmmmh!

Ni ndoto tu!

Ila hii ni mara ya nne mwendelezo wa ndoto hii! Najiuliza kulikoni! Mara ya mwisho niliota kunaubishani wa Katiba ya nchi. Nini kifanyike! Nchi ilijawa na ukimya, kulikuwa na utupu wa utawala! Kulikuwa na ubishano mkubwa. Nchi ilikuwa imetulia saaana! Hakukuwa na furaha!
Noted
 
Back
Top Bottom